NAPE: Kikao kijacho CCM kuja na maamuzi mazito

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,229
Nape asema waliokiuka maadili ya CCM kukiona,kikao kijacho tutatoa maamuzi mazito



SOURCE:BLOG YA ISSA MICHUZI NA YOUTUBE.
 
Last edited by a moderator:
Aaache unafiki, maamuzi mazito mwaka unaisha na verse ni hio hio, wanamtishia nyau nani? labda this time watakuja na kujivua govi!!!!! Haya ngoja tusubiri tuone, yetu macho
 
Hakuna cha maamuzi magumu kwa hawa magamba wanachofanya nikutudanganya tu (usanii), mara siku 90, mara siku 120, kazi yao ni kumtuma huyu vuvuzela Nepi kupiga kelele tu.
 
Wameshatuuzi na kusitasita kwao, wasipofanya kweli tunachukua CCM yetu kuanzia shinani, miaka mitatu siyo mingi,porojo tumezivumilia na tunaanza kuchoka.
CCM Taifa (NEC) imeitupa sana jumuiya yake ya wafanyakazi ambayo ndiyo msingi wa TAA, TANU na sasa CCM-magamba.You guys made the biggest mistake of all, by disrespecting Trade Unions. Wafanyakazi wa Tanzania ndiyo uti wa mgongo wa Chama, kila familia ya Mkulima Tanzania ina mtoto au mjomba ambaye ni mfanyakazi, ambaye zamani ndiyo alikuwa kinara wa familia au ukoo, na ambaye moja kwa moja alikuwa ndiyo kada wenu. Leo hii mmetutupa kabisa kama hatuna maana yeyote ile, mmewakumbatia matajiri na mmeuza viwanda vyetu bila sababu ya muhimu.
Pre- SAP balance of payments was lower than the now post-SAP balance of payments, even after selling all our stuff and getting debt relief from your masters. We want our country back!!, and it better start from the top - down, cause if it starts from the grassroots, hapatakalika.
Wasalaam.
 
Nape tangu upewe hiyo nafasi ya Ukatibu mwenezi, sijakusikia ukiongelea hoja za msingi za kuwaletea Watanzania Maendeleo na kuwatoa katika janga la Umasikini, zaidi wewe na chama sijui kitafanya nini kujiimarisha, sijui kujisafisha kwani haujui chama chako ni kichafu tena kinanuka.
Nakuomba uongee mambo ya msingi Watanzania tunapigika tumechoka kusikia kila wakati kukisifia chama chako, hatukatai ila tunataka maendeleo kwa hii nchi.
 
Nape tangu upewe hiyo nafasi ya Ukatibu mwenezi, sijakusikia ukiongelea hoja za msingi za kuwaletea Watanzania Maendeleo na kuwatoa katika janga la Umasikini, zaidi wewe na chama sijui kitafanya nini kujiimarisha, sijui kujisafisha kwani haujui chama chako ni kichafu tena kinanuka.
Nakuomba uongee mambo ya msingi Watanzania tunapigika tumechoka kusikia kila wakati kukisifia chama chako, hatukatai ila tunataka maendeleo kwa hii nchi.
Huyu jamaa ni majungu tu na kejeli ndo anaziwezea
 
Labda ndo wameamua kufanya maamuzi magumu baada ya kumsikia Sitta kwenye ITV jana
 
Walengwa wapya ndo watakaofukuzwa ccm, CDM tujiandae kupata majimbo muda si mrefu, maana watakao tolewa hawatakuwa kama mnafki Rostam! hawa watahakikisha CCM haishindi kwenye majimbo yao
 
Sasa hivi kibao kimebadilika, Nape kasema magamba si mafisadi bali wanaokiuta maadili ya chama. Goodbye Mr Six.
 
Back
Top Bottom