NAPE: Kikao kijacho CCM kuja na maamuzi mazito

mimi naona kaongea vizuri tu hata kama kawalenga baadhi ya watu lakini kwa nafasi ya Nape ndani ya chama ni muhimu kuyatolea maelezo matukio ya hivi karibu. Ni mapema sana kumpuuuza.
 
Nape ni kijana mdogo ukilinganisha na nafasi aliyopo na hii ni jitihada ya Rais kuwapa vijana uongozi wa chama tusimvunje nguvu
sikujua kwamba rais ameanza kuwapa vijana nafasi kama anavyofanya kwa wanawake.kama ndio hivi tutarajie taifa kuangamia soon.
 
Hata katika kuongea Nape ameonyesha japo ujasiri wa kukemea ni dalili njema endapo atakomaa vema anaweza kufanya vizuri kuliko sasa
 
Wameshatuuzi na kusitasita kwao, wasipofanya kweli tunachukua CCM yetu kuanzia shinani, miaka mitatu siyo mingi,porojo tumezivumilia na tunaanza kuchoka.
CCM Taifa (NEC) imeitupa sana jumuiya yake ya wafanyakazi ambayo ndiyo msingi wa TAA, TANU na sasa CCM-magamba.You guys made the biggest mistake of all, by disrespecting Trade Unions. Wafanyakazi wa Tanzania ndiyo uti wa mgongo wa Chama, kila familia ya Mkulima Tanzania ina mtoto au mjomba ambaye ni mfanyakazi, ambaye zamani ndiyo alikuwa kinara wa familia au ukoo, na ambaye moja kwa moja alikuwa ndiyo kada wenu. Leo hii mmetutupa kabisa kama hatuna maana yeyote ile, mmewakumbatia matajiri na mmeuza viwanda vyetu bila sababu ya muhimu.
Pre- SAP balance of payments was lower than the now post-SAP balance of payments, even after selling all our stuff and getting debt relief from your masters. We want our country back!!, and it better start from the top - down, cause if it starts from the grassroots, hapatakalika.
Wasalaam.

nyie si ndio mliotumika kama makuwadi? Leo mnajifanya wazalendo upuuzi bin wizi mtupu sh.n.z. zenu
 
Nape chanja mbuga umeanza vizuri umekuta mambo mazito sio rahisi kuyamaliza yote kwa siku moja tuko nyuma yako Roma haikujengwa kwa siku moja
 
Nashauri mafisadi waliopo JF kwa majina bandia wasitupeleke kusiko kila analosema Nape halina maana
 
Nashauri mafisadi waliopo JF kwa majina bandia wasitupeleke kusiko kila analosema Nape halina maana
upupu wake kila siku anaomwaga lipi ametekeleza?upo fofofo kweli
 
nyie si ndio mliotumika kama makuwadi? Leo mnajifanya wazalendo upuuzi bin wizi mtupu sh.n.z. zenu
Ni watu kama wewe wanayoifanya Dar ibaki mikononi mwa CCM, dharau, kejeli na matusi is a sign of immaturity.
What a fkn looser!
 
Ni watu kama wewe wanayoifanya Dar ibaki mikononi mwa CCM, dharau, kejeli na matusi is a sign of immaturity.
What a fkn looser!
Dar ndo mkoa ambao una watu wasiopenda mabadiliko
 
Dar ndo mkoa ambao una watu wasiopenda mabadiliko
Dar is a melting pot, a cosmopolitan city even in the world's standards. Mji wa Dar una cultures nyingi na ethnicities nyingi zaidi ya miji mikuu mingi tu duniani. Sasa niambie kwanini CDM inashindwa kuchukua Dar?.. Unafikiri ni kwa sababu ya kuipenda CCM au vihuni kama hicho kilichonitukana hapo juu?
I don't want you to think outside of the box my brother!... I want you to realize that, THERE IS NO BOX!!!
 
Nape tangu upewe hiyo nafasi ya Ukatibu mwenezi, sijakusikia ukiongelea hoja za msingi za kuwaletea Watanzania Maendeleo na kuwatoa katika janga la Umasikini, zaidi wewe na chama sijui kitafanya nini kujiimarisha, sijui kujisafisha kwani haujui chama chako ni kichafu tena kinanuka.
Nakuomba uongee mambo ya msingi Watanzania tunapigika tumechoka kusikia kila wakati kukisifia chama chako, hatukatai ila tunataka maendeleo kwa hii nchi.
.........Na hutamsikia, aliteuliwa kwa ajili ya kuvua watu magamba, baada ya singo hiyo kuchuja kwa ama kukosa mvuto kwa kupigwa sana au vinginevyo, naye atapotea
 
Hakika siasa za zama hizi ni ubabe wa MATUSI.Anaejua kutukana ndie anaejua siasa.Matusi ndio yatakayokiangamiza chama CDM.Bila kutukana unaonekana hujui kujenga hoja.Vijana wenzangu kutukana watu tena hata hawakujui na hawajakutukana ni matumizi mabaya ya uhuru wa kutoa maoni na ndio maana matatizo hayaishi coz ya laana.
Inawezekana una hoja lakini baada ya kuangamia CCM
 
Ni agharabu baadhi ya wanaJF kuonyesha angalau kwamba Nape ashauriwe anaweza kuwa kiongozi mzuri badala ya kumkatisha tamaa ni kama tunaombea turudi tuliko toka. Chini ya Uongozi wa Nape amejitahidi sana kuwapa wananchi taarifa ukilinganisha na waliomtangulia hii peke yake ni sifa nzuri ya kiongozi bila kujali ni nini anatueleza.
Utamshauri nini mtu ambaye mawazo yake yapo utumwani? mtu ambaye anatumika kaseme hiki mara kile kichwa chake anatumia kwa kufugia nywele tu na kuvaa kofia, ushauri wako ukimpa unahitaji afikiri, lakini ona matumizi ya kichwa chake, ushauri utaenda bure mkuu heri kukaa kimya
 
Nape ni kijana mdogo ukilinganisha na nafasi aliyopo na hii ni jitihada ya Rais kuwapa vijana uongozi wa chama tusimvunje nguvu
Kuwa kijana mdogo sio tiketi ya kuvurunda, ana tofauti gani na akina Nyerere wakati wanachukua nchi, unataka kutuaminisha nini kwamba vijana hatuwezi?
 
Back
Top Bottom