Nape: Hatutakabidhi nchi kwa wahuni

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Muda mfupi uliopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amefungua Baraza la UVCCM Wilaya ya Missenyi na kusema kuwa CCM haitakubali kukabidhi nchi kwa wahuni waliojificha katika makundi ya wanaharakati.
 
Kwa hiyo amekubali kuwa 2015 hawashindi lakini hawataondoka madarakani !
 
Inaonekana bado hajajua maana ya NGUVU YA UMMA. Ukweli ni kuwa watakabodhi bila kupenda. Hawatakuwa na kufanya. mwambieni kuwa wakati ni ukuta, ukipigana nao utaumia bure.

AMA KWELI 'SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA'.
 
Kwa hiyo amekubali kuwa 2015 hawashindi lakini hawataondoka madarakani !

Nyie hamjamuelewa Nape, wahuni anaowasema ni ccm ya m.k.w.e.re. Hivi hamkumbuki Mkapa aliposema: "Sitaki ccm ifie mikononi Mwangu"? Hata Che Nkapa alishajua CCM imeshageuka ccm na kwa maana hiyo lazima ife!
 
kati ya wahuni na majambazi wapi afadhali..........?
fikra za aliye ndani ya boksi hutegemeana sana na ukubwa wa boksi alilomo.....

huyo yumo ndani ya matchbox. hajui alinenalo. mwache aendelee ku masterb..te. Fikra potofu ziwe juu yake.

aliyempa hicho cheo cha kueneza pumba zake, amemmaliza kisiasa. yy hilo hajalitambua kwa sasa. poor young boy.
 
Muda mfupi uliopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amefungua Baraza la UVCCM Wilaya ya Missenyi na kusema kuwa CCM haitakubali kukabidhi nchi kwa wahuni waliojificha katika makundi ya wanaharakati.

Hapo kwenye red ndiko kunanipa wasiwasi. Hawatakubali? Watafanya nini? mabomu?
 
Muda mfupi uliopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amefungua Baraza la UVCCM Wilaya ya Missenyi na kusema kuwa CCM haitakubali kukabidhi nchi kwa wahuni waliojificha katika makundi ya wanaharakati.

kwanza Nape na wana ccm wajue hii nchi si yao. Hii nchi ni ya watanzania wote na kwenye ballot box ndio watanzania watachagua wanayetaka awe kiongozi wao. Hata siku moja husikii america or europe chama tawala kinatoa matamko ya namna hiyo...that shows how low level these guys are. Nape atakayeamua nani anachukua nchi 2015 sio nyie ccm bali ni wananchi wote wa tanzania kupitia haki yao ya msingi ya kupiga kura.
 
Huyu simshangai maana haitanishangaza kesho akaikataa kauli yake! Si alishawahi kuikataa id yake alipotangaza matokeo ya Igunga hapa jf? Hata itakapofika wakati wa kukabidhi nchi kwa "wahuni", atapinga hakuwahi kukataa!
 
Jamani nani kamdangaya dogo hii nchi mali yake binafsi kwa hivo anayo hiari ya kuikabidhi au kutokabidhi? Hajui wenyenchi? Ni mimi na wewe and certainly not CC , NEC or CCM for all i know. Disabuse your mind Nape.
 
mawazo mgando nataendelea kusema siku zote Mungu anapotaka kufanya jambo lazima huwa anafanya vitu vya kukwamisha jambo fulani ili lile alilopanga likapate timia kwa maana hyo ccm wamepigwa upofu kwa hyo awajui wapi wanakwenda ndo maana wanatoa matamshi ya hatari sana kwenye mikutano yao, wahuni ni wao
 
Muda mfupi uliopita Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amefungua Baraza la UVCCM Wilaya ya Missenyi na kusema kuwa CCM haitakubali kukabidhi nchi kwa wahuni waliojificha katika makundi ya wanaharakati.

Mie niliisha waambia humu ndani nchi haikabidhiwi kwa vikaratasi vinavyo tumbukizwa kwenye masanduku, ni zaidi ya hapo. Hicho ndicho wengi wenu hamjui na hamta kaa mjue hata siku moja
 
Ukishakuwa na Laana lazima inatembea vizazi na vizazi kwa hiyo hapa Nape hajui hata anachoongea ila yeye anaona yuko perfect
 
Tatizo la Nape ni uelewa mdogo juu ya mmiliki wa nchi ni nani!! Kwa mawazo ya Nape anafikiri Tanzania ni ya ccm,"u Young boy Nape sikia Tanzania siyo ya CCM ni ya Watanzania wote,tuliwapa dhamana ccm muiongozenchi yetu mmeshindwa,na sasa watanzania ndio tutakuwa na maamuzi ya kuwanyang'anya nchi yetu na kuikabidhikwenye nguvu ya UMMA wa Watanzania,siyo kwa kupewa na ninyi ccm Nape"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom