Nape fanya upembuzi wa kiakili

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
3,216
988
Nimeshanga kuona katibu mwenezi wa CCM Bw. Nape Nnauye akidai CCM kimeshinda kwa asilimia 75 (75%) wakati ni dhahiri shahiri kimsingi angesema CCM kimeshindwa kwa asilimia kadhaa badala ya kutumia hesabu za kudanganya umma tena akidai eti vyama vya upinzani vimeendelea kupuuzwa. Angalia hapa Nape;

Viti vya chaguzi wa udiwani kabla na baada ya matokeo ya jana nazingatia viti vilivyogombewa tu

Kabla ya uchaguziBaada ya uchaguzi
CCMCHADEMATLPCUFCCMCHADEMATLPCUF
2921022511

Hapa kwa hesabu za haraka kila aliyeenda japo darasa la pili la masomo ya shule ya msingi atakubali CUF toka zero wamepata kiti kimoja, TLP wamebaki na kiti chao kimoja na CDM wamengeza viti 3 juu ya viwili. Sasa niambia CCM wamepeteza vingapi? Kwanini kutumia lugha laini ya kwamba tumeshinda badala ya kusema tumepoteza viti?

Haya ndiyo yanatufanya sisi tuliokuwa mashabiki wa CCM kuendelea kukosa ari ya kuwashabikia maana tunaendelea kudanganywa achilia mbali kuumizwa na tabaka la uongozi wa CCM uliojikita katika misingi ya mitandao na ufujaji wa mali za umma.

Napingana na Nape ila pia namwambia CCM imeshindwa badala ya kushinda na imepoteza viti kwa asilimia kama 25 (24.1%)

Nawasilisha
 
Nape alisoma historia, haya mambo ya mahesabu hakuwahi kuwa nayo karibu.
 
Not aware of political ethics (nape)

naanda anguko pevu na endelevu magamba (nape)
 
Back
Top Bottom