Nape: Dr. Slaa anaiua CHADEMA

Poloni wana CHADEMA hawa ndo wa Tanzania msiwa underestimate. Wanaona wanasikia na wanajua pumba na mchele. Pumba zikizidi ni mgogoro. Tusubiri kauli za kujipa matumaini na kulia lia na visingizio vya nchi inakwenda nakadhalika lakini habadi ndo hiyo. Twishamaliza sisi. CCM ndo SISI
 
Nape swala la kupoteza kata halioni. Nape ana muogopa sana Dr slaa kila leo aanaota ahaache siasa!

Cha kushangaza zaidi Nape ana penda kujipima kwa Dr slaa wakati hata hamuwezi hata chembe!

Nape ni mjanja wa kutoa matamko tu lakini swala la rushwa kwenye chama chake lilimshinda kabisa hadi wenzie wanapigana!

Ukitaka kujua issue ya jk na mwanae ni ukweli angalia Nape alivyo kanusha!
 
movement for dealth.........nape kama huwez kuandika ki-MULUGO uache...ki-MULUGO ni kigumu sana kijana
 
uvumilivu sasa basi. Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete afungue mashtaka dhidi ya Slaa. Uzishi kuwa mtoto wa Rais alikamatwa na madawa ya kulevya China na Rais kwenda huko kunusuru umeenea sana hapa Chuo kikuu Cha Dar-es-Salaam. Unaenezwa na wahadhiri wa chache ambao wote ni makada wa CHADEMA. Hatujawahi kuuchukulia umakini. Lakini kama Slaa amekwenda mbali na kuutumia kwenye kampeni za udiwani basi ni wakati muafaka familia ya Kikwete kutafuta haki yao mahakamani. Tulikuwa tunamheshimu sana Dr Slaa lakini amekuwa na tabia ya kuzusha mambo makubwa yanayoweza kuleta vurugu nchini
 
Hawatarudia. Hii ni sawa na kuambulia asilimia chini ya ishirini kama sikosei. Na kwa ccm huu ni ushindi wa zaidi ya asilimia 75. Sasa kati ya vyama 18 vingine vikifadhiliwa na wazito wa berlin conference
 
Nape hizo ni asira zako za wewe kushidwa vibaya na lowasa huko magambani na kama usipo angalia jamaa watakukolimba
 
Hakuna sababu ya kuwatukana CCM. Nape ana kila sababu ya kujivunia ushindi. Kumekuwa na uzishi na kuwaminisha wa Tanzania eti Slaa anasubiri tu kuapishwa 2015. Hata wana diriki kusema kuwekwe utaratibu wa kuwakabidhi nchi. Sasa una viti vitano tu kati ya 29 ndo umekamata nchi??? Acha bana siasa za kale. Upinzani baado. Hatujaona sababu na haitatokea mpaka tuwe makini na watu wanaojinadi
 
Don't ague with a foolish.
Naishauri sana CHADEMA wasijibu chochote dhidi ya hili tamko la kiuwendawazimu la Nape.

Kama CHADEMA wataongea na vyombo vya habari wajikite zaidi kwenye facts na sio propaganda kama za huyu Chiliku.
 
Mambo ya lowasa na ccm ni ya ndani ya ccm. Chadema kwani mambo ya ndani ya zito ya shubuda ya mdee na sasa ya wale wazee wawili kwani wa tanzania hawayafahamu?? Tusubiri muda si mwingi tutashuhudia hilo tofali la barafu likiyeyuka kama samli kwenye moto
 
Nape ni vuvuzela la CCM,mnajipa matumaini,lakini ujue,mabadaliko huwezi kuyazuia ni kama upepo.Najua unajaribu kujipa matumaini,jiandaeni kukumbana na mkono wa sheria mkishaondolewa madarakanu.Hapa ni mapambano kati ukweli na uongo,mafisadi na wananchi maskini.
 
chadema wakajibu ni i kwenye vyombo vya habari acha waugulie maumivu. Hata ITV nadhani sasa itawachoka maana wanaipakazia na kamwe hawataisaidia kwenye mambo yake mengine huko. Usione Simba kaloa ukadhani paka utaumbuka tu akinyanyuka
 
Nape mmoja ni sawa na mavuvuzela yoote ya chadema. Kijana mmoja anawanyima usingizi wazee. Walikuwa wakimpamba wakidhani angeingia chadema. Huyoo akaula na kuwa bosi wa ccm. Ghafla wakaanza siasa za sizitaki mbichi hizi. Nape unatisha endelea kuwachezesha magirigiri hawa wanamaandamano yasiyo na ajenda.
 
Kama ningekuwa chadema ningeomba mwongozo wa mzee edwin mtei. Haiwezekani chama kimefanya kampeni za nguvu nchi nzima. Tangu mwaka 2010 chadema hawakusimamisha kampeni. Wamekuwa kwenye majukwaa na kwenye magazeti na kwenye nkrumah hall wakiamasisha sasa hii ya tano ya ishirini kwa waliopiti chuo kikuu koz work haijatosha hii ni disco. Poleni ndo siasa hizo msijiamini sana
 
Ni kichaa tu au mtu mwenye mtindio wa ubungo anaweza kutoa tamko la kipumbavu kama hili.Chonde CDM msijibu huu ujinga!
 
Anachokifanya Nape ni kutaka kukwepesha kwa makusudi hoja ya msingi kuhusu mwenendo mzima wa chaguzi za ndani za CCM kwa namna zilivyogubikwa na kila namna ya vituko.

Nitashangaa sana kama wanaCCM watakaa kimya kwa hili.
 
Hawa ndiyo wapiga kura na wala siyo hao vijana wa mjini wanaopiga vuvuzela kwenye mikutano ya hadhara ya Chadema.

Kama Chadema mnashindwa kuwa-convince hawa kuwapigia kura then, msitegemee kuchukua nchi. Tukana lakini ndiyo ukweli wenyewe.

11.+Wazee+wakifuatilia+kwa+makini+hotuba+ya+Nape+Kata+ya+Bugarama,+Kahama+mkoani+Shinyanga.jpg


13.+Mzee+wa+miaka+98,+Nickson+Toma+akifuatilia+kwa+makini+mkutano+wa+kampeni+za+udiwani+Kata+ya+Bugarama+mkoani+Shinyanga+uliohutubiwa+na+Nape.jpg
 
Back
Top Bottom