NAPE: Dk. Slaa ameikimbia Mwanza mapema

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Friday, September 28, 2012


*Asema Dk. Slaa ameikimbia Mwanza mapema baada ya kunusa Chadema kugaragazwa

*Awapongeza madiwani wa CCM wa Nyamagana kwa kuwezesha ushindi wa Menya na Naibu Meya Nyamagana

NA MWANDISHI WETU, MWANZA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema dalili za kubwagwa kwa CHADEMA ndizo zilizomkimbiza mapema jijini Mwanza, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroard Slaa.

Amesema kushindwa kwa Chadema katika kinyang'anyiro cha Meya na Naibu Meya, ni mavuno ya ubabe wa viongozi wa chama hicho ambao baadhi wanazeeka vibaya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Nape (pichani) alisema kwamba, Slaa alikimbia baada ya kuona maji yamezidi unga.

Nape aliyetumia fursa hiyo pia kuwapongeza Madiwani wa CCM wa wilaya ya Nyamagana na Chama kwa ushindi wa Viti vya Meya na Naibu wake, alisema Dk. Slaa anazeeka viba ndiyo maana naongoza chama hicho kwa ubabe na maandamano ya kila mara.

"Babu (akiwa na maana ya Dk Slaa) alisema CCM Mwanza itaondoka madarakani, imejidhihirisha wazi katika uchaguzi wa leo kuwa CCM bado ina nguvu na ni Chama kikongwe kisiasa, vingine vinaiga."

"Chadema wameona mavuno ya ubabe wao japo kura za CCM ni ndogo…., Babu ajiulize kwa nini ameshindwa kwenye uchaguzi huo wa Meya na Naibu Meya." Alisem Nape na kuongeza kwamba, kutokana na dalili za kushindwa zilizoonekana mapema, ndiyo maana Dk Slaa alikimbia Mwanza mapema.

Akiwapongeza madiwani hao kwa ushindi alisema kwamba wamefanya kazi kubwa na ya ziada kuhakikisha CCM inarejesha Halmashauri ya jiji hilo mikononi mwake baada ya kushikwa na Chadema kwa kipindi kifupi na hivyo kuwataka wana Mwanza wawe na mshikamano na kuwapa ushirikiano viuongozi wao.

"Nawasihi wananchi wa Mwanza wawe na mshikamano na kuacha maandamano yasiyokuwa na msingi, badala yake wafanye maandeleo, waimamini CCM sasa inachokuja kufanya ni cha uhakika." Alieleza Nape.


POSTED BY: BASHIR NKOROMO AT FRIDAY, SEPTEMBER 28,







 

CHADEMA waache kufanya kazi kwa kufuata popularity stings... Lazima wafanye kazi kwa AKILI

Wangeangalia ni kazi GANI Mkuu wa MKOA MPYA wa Mwanza nia yake ilikuwa ni kuwalainisha Wana

Chadema
Madiwani wasio na MSIMAMO; Kama VIONGOZI wa CHADEMA MAKAO MAKUU wasipokuwa

Waangalifu
CCM itawachezea kila MAHALI...
 

chadema waache kufanya kazi kwa kufuata popularity stings... Lazima wafanye kazi kwa akili

wangeangalia ni kazi gani mkuu wa mkoa mpya wa mwanza nia yake ilikuwa ni kuwalainisha wana

chadema
madiwani wasio na msimamo; kama viongozi wa chadema makao makuu wasipokuwa

waangalifu
ccm itawachezea kila mahali...

sijakuelewa tafadhali. Ufafanuzi
 
sijakuelewa tafadhali. Ufafanuzi

Mkuu wa MKOA wa MWANZA ndie alieyeanza kuwapa hongo MADIWANI WA CHADEMA wa Kuchaguliwa ili

Wabadilishe kura zao kuchagua Mwana CCM as MAYOR... na tatizo walilonalo CHADEMA Mwanza na ILEMELA
 
Nape VUVUZELA la ccm, mmefanya UMAFIA wa hali ya juu kwa kukiuka sheri kuhamisha wabunge wa Ilemela na diwani wa viti maalumu, halafu bila ya aibu unafunua domo lako pana kubwabwaja na kumwita Slaa Babu yako kakuzalia marehemu Babako? We Nepi subiri kipindi kipindi kifupi 2015 afya yako hiyo kama boga la Isimani itakwisha kama vile umetolewa upepo kwenye tube. Utatupwa kwenye jalala liwakalo moto wakati wote.
 
CDM ni maafa kanda ya ziwa, pongezi zipokeeni wana Nyamagana kwa kugundua udhaifu wa chama kilijichokita kwenye misingi ya ukanda na ubabe
 

CHADEMA waache kufanya kazi kwa kufuata popularity stings... Lazima wafanye kazi kwa AKILI

Wangeangalia ni kazi GANI Mkuu wa MKOA MPYA wa Mwanza nia yake ilikuwa ni kuwalainisha Wana

Chadema
Madiwani wasio na MSIMAMO; Kama VIONGOZI wa CHADEMA MAKAO MAKUU wasipokuwa

Waangalifu
CCM itawachezea kila MAHALI...

Uangalifu ni pamoja na kuwatimua viongozi wasio waadilifu,
tuko radhi kukosa hata jimbo zima kuliko kuwa na viongozi mamluki.
Nawapongeza viongozi wa chadema kwa kufanya maamuzi magumu bila kuogopa athari.
Ni bora usalama kuliko hatari.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
CDM ni maafa kanda ya ziwa, pongezi zipokeeni wana Nyamagana kwa kugundua udhaifu wa chama kilijichokita kwenye misingi ya ukanda na ubabe
Idadi ya madiwani iko wazi,
Hapa pongezi wape wale madiwani waliosaliti chadema na kufukuzwa na kufanya idadi ya ccm na cuf kuongoza.
Ila cha msingi ni kwamba cdm ni chama pekee kinachofanya maamuzi magumu, tuko tayari kupoteza hata jimbo zima kuliko kuwa na viongozi mamluki ndani ya chama chetu makini.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Bora kuwa na balozi pekee lakini mwamifu asiye msaliti kuliko kuwa na madiwani watakao tenda kwa maslahi yao binafsi na kupelekea kuondoa imani ya wananchi kwa chama.
 
... i real doubt, the same thing is going to happen in 2015 Elections!
which ever reason it might be, ccm will continue outwitting the oppositions .... (wazee wa fitina na zengwe!).
 
Idadi ya madiwani iko wazi,
Hapa pongezi wape wale madiwani waliosaliti chadema na kufukuzwa na kufanya idadi ya ccm na cuf kuongoza.
Ila cha msingi ni kwamba cdm ni chama pekee kinachofanya maamuzi magumu, tuko tayari kupoteza hata jimbo zima kuliko kuwa na viongozi mamluki ndani ya chama chetu makini.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Porojo zingine sasa kama mlikuwa mnayajua hayo kwa nini Dr Slaa alienda Mwanza.
 
Nawapongeza CDM kwakuwa timua madiwani wasio waaminifu ni bora kutokuwa na diwani hata mmoja kuliko kulea fedheha ya utovu wa nidhamu na kukosa uadilifu.
 
Back
Top Bottom