Sijaipenda sana hutuba yake kwa wanahabari.Kwanza kwa muda huo huo ka-contradict mambo,halafu kawa Mwepesi kutoa maneno mabaya kwa Dr Slaa.Nadhani hukumu ya Leo haijamfundisha Kitu.Hukumu ya leo ni kua CCM haiwezi kila Kitu na ikitokea kajiweka Pabaya inaweza kuwa ndio mwisho wake kisiasa.Angalau ingekuwa ingekuwa mwisho huku ukiwa na mihela kibao isiyoweza kuletea shida.Ni msemaji wa CCM ila busara itamlipa kuliko Lusinde.Ingawa Anapata upinzani ila hakuwa akisikika katika matusi,na hiyo ndio ingekuwa ndio nguvu pekee ya kumpatia masikio ya watu ili amwage sera.
-Kwanza kakanusha.
-Kashutumi CMD kuwa ni waongo.
-Halafu kakubali kuwa huwa wanapiga Kambi,katoa maelezo haraka haraka kuhusu hizo Kambi, halafu kahamia kumkejeli slaa.kejeli zake zimeenda mbalia sana kwa kiasi kinachoweka ukuta mkubwa zaidi yake na CDM.Na itapelekea kuwafanya CDM wajikite katik kutoa proof kwa hasira na popote .
-Nape katoa sababu nyepesi za utetezi kuwa vijana wapo katik chaguzi.Ila anasahau kuwa raia wa kawaida atajiuliza ?Kwani vyombo vya ulinzi na usalama navyo si vina vijana?Halafu pia vijana si lazima wote wawe Dodoma.Pia kauli ya Dr. Dlaa haijaweka wazi mchakato ungefanyika vipi na hivyo kutoa Nafasi ya CDM wa kauli ya slaa anauwezo wa kuthibitisha kuwa Morogoro na Dodoma si mbali.
-Nape katoa shutuma kwa njia dhaifu sana, hata kama CDM walikuwa na hilo lengo,ingawa kwa record CDM bado hawajaonyesha leta fujo wakiwa peke yao.CDM wapo katika better position kujitetea na kusikilizwa na wananchi.Sasa kinachofuatia ni majibizano kwa staili ambayo ,kama mheshimiwa Nape angekuwa kapunguza haraka na kuongeza umakini asingejiweka katika nafasi ya kupigana yeye kama yeye na CDM.Ila angacha CCM na CDM.Yeye kama yeye ajue kuwa anavyojiweka katika hali kama hizo si salama sana,kwani kama CCM ni kutoka,itatoka tuu napengine kufa kabisa.Yeye bado ni kijana na atakauwepo hata baada ya hayo matukio,sasa angejua tuu kusimama kwake jukwaani na kutoa maneno ambayo siku nchi inaangukia katika vita mbaya.Hata kama na CDM kuna watakaotakiwa katika mahakama ya kimataifa, yeye nae atakuwepo.
Kwa ujumla bila kutoa hukumu kama alichosema yeye,au alichosema dr. Slaa ndio kweli, au wote waongo, ama wote wana ukweli nusunusu, Mh.Nape hajanifurahisha, kaonekana kuwa na ujasiri wa sauti na sura ila kauli dhaifu saana na zinamshitaki kuliko hata anavyoshutumu Dr.Kaongea kwa kauli dhaifu sana na zinazokaribisha m4C imgeukie yeye badala ya Chama chake.Kwa mwana siasa makini makini huwa hakupaswa jiweka kuwa target au hata kumfanya mpinzani atumie makomboro makubwa.Huku wangeweza tumia mepesi wakifanya mizaha huku wakiamini kuwa wanakujua kuwa ndivyo ulivyo.Sasa hili la kuwaambia polisi wakalazishe toa ushahidi ni kuthibitish aliyosema dr. kuwa kuna mengi hawajayafanyia kazi na kuwa kazi yao ni kulinda serikali na si raia.
Kwa ujumla nilitegemea mheshimiwa Nape angepangilia sana hotuba yake, angetoa maneno yenye kujiepusha kuwasha moto, moto ambao si mzuri kwake kisiasa.Kwani jamaa wakiwaka nae hatakuwa tena thamani jukwaani.