Vijana wa CHADEMA mmepeleka wapi akili yenu?

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
Na Thadei Ole Mushi

Nimefuatilia kwa karibu sana tukio lililotokea Hai la Mbunge kuzomewa. Baada ya tukio lile vijana wa Chadema wametuletea picha za vijana walioongea na vyombo vya habari wakielezea sababu za kuzomea.

Nimegundua kuwa vijana wa Chadema wengi wanafanana tu na wale wa Lumumba katika thinking yao. Wameacha Hoja za msingi zilizotolewa na vijana hawa wanakimbilia kutuonyesha kuwa vijana hawa walikuwa ni wa CCM. Kuwa wa CCM au sio wa CCM ni hoja nyepesi sana, kama tungetumia robo tu ya elimu zetu tungejadili hoja zao zaidi kuliko itikadi wanazoshabikia.

HOJA ZAO NI ZIPI

1. Mbunge toka amechaguliwa kwa miaka yote Mitano hajawahi kufika kwao na kufanya hata mkutano mmoja. Wao wanahoji alikuwa wapi muda wote? Hii Ni Hoja ya Kwanza ambayo nilitamani vijana wasomi wa Chadema wangeijibu au hata katibu wa Mbunge angeijibu au hata Mbunge Mwenyewe.

Tuelezeni Mbunge alifanya mikutano mingapi kabla ya mkutano wake wa kuzomewa katika hilo eneo. Mikutano ya wabunge kwenye majimbo iliruhusiwa kuwepo yeye alitokea kufanya mkutano hata mmoja?

2. Agenda zake zote Mbunge si agenda za maendeleo bali ni za kuishambulia Serikali. Je, haya yana ukweli kiasi gani? Je wananchi kuelezwa habari za malalamiko tu bila kujadili kero ya maji, barabara, elimu, afya n.k ni sawa? Je, wananchi wa eneo hili mgogoro wa Chadema na Serikali unawanufaisha vipi? Hii nayo ilikuwa agenda ya msingi sana ambayo nilitamani vijana wasomi wa Chadema kuijibu kwa weledi badala ya kukimbilia kuungaunga picha za waliotoa malalamiko.

3. Kabla ya vurugu kutokea kwa mujibu wa video inayosambaa kuna sauti ya kijana inahoji kwa kusema "Kwa miaka mitano umetufanyia nini mheshimiwa". Kwangu mimi hili ni swali la msingi sana ambalo linapaswa kujibiwa na vijana wasomi wa chadema. Waeleze kwa mifano Mbunge kawafanyia nini, hili la kuunganishwa picha sioni kama lina logic sana.

MWISHO
Nilidhani mnaweza kujitofautisha na sisi wa CCM katika kujenga Logic na Reasoning. Tokeni mjibu hizo Hoja acheni kuunga unga picha. Kitu ambacho hamjui hata hao vijana wangelikuwa ni wa CCM au ACT au hata Chadema haiwaondolei haki ya kumhoji Mbunge wao. Haiwaondolei haki ya kupata maendeleo. Mbowe si Mbunge wa wanaChadema tu, anahusika pia kwa wanaCCM waliopo kwenye Jimbo lake. Haihitaji rocket science hapa kujua kuwa mnakurupuka.

Kama wananchi hawasikii agenda za maendeleo lazima wakuletee fujo, kama wananchi wanaona huwasaidii lazima wakuletee fujo. Tuwabane viongozi wetu watuletee maendeleo. Sio Mbowe tu wote hata wale wa CCM. Hai mmeonyesha njia wengine tufuate.

Tuendelee kusema kweli kuiponya Tanzania yetu. Acheni kukabidhi akili yenu viongozi wenu huku mkitembea na vichwa vitupu, jitofautisheni na waimba pambio za Lumumba.

Mbowe si malaika, acheni ajibu maswali ya wananchi wake.

Ole Mushi
0712702602


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother watu wapo smart sana tofauti na wewe unavyofikiria. Ukijiweka mjuaji unaanikwa chap then watu wanakupotezea.

By

Mtoto wa mjini

Nyamagana stand up.
 
Back
Top Bottom