Ndeanka na wenzake wanahitajika majimbo yote Tanzania Bara na Zanzibar kufanya 'fujo' kama kwa Mbowe

Isike Moses

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,789
4,243
Katika anga ya siasa za Tanzania, tukio kubwa na linaojadiliwa kwa sasa ni FUJO zilizo jitokeza kwenye mkutano wa Mh. Freeman Mbowe alipokuwa akihutubia wananchi jimboni kwake. Kundi la 'vijana' liliibuka na kuanza kupiga kelele na kutoa maneno yenye mlengo wa kutokubaliana na uongozi wa Mh. Mbowe. Madai yao yanaangukia kwenye umasikini wa jimbo, miundombinu mibovu na kukosekana kwa mikutano ya Mbunge mara kwa mara.

Katika ukurasa wa Facebook, ukienda kutafuta jina la Ndeanka Wa Mwalimu Urassa, ukifungua picha zake utakutana na picha ya kijana ambaye ndiye mmoja wapo aliohojiwa na kutoa malalamiko kuhusu Mh. Mbowe. Huyu ni kijana wa Chama Cha Mapinduzi (ngazi ya vijana), na aliyekuwa pia analalamika baada ya Ndeanka pia ni kijana wa Chama Cha Mapinduzi.

Sina tatizo na wao kuwa wanachama vijana wa CCM maana katika majimbo kuna wenye vyama na wasio na vyama, Viongozi wanao wajibu wa kuwahudumia wote. Ikiwa kuna masuala ya maendeleo hayapo sawa, ni HAKI ya wananchi kutoa malalamiko yao kwa Viongozi/Kiongozi wao.

MAJUKUMU YA MBUNGE NI YAPI?

Pamoja na kwamba kwa Tanzania mbunge analazimika kuwajibika kwa chama chake, ni vyema kujua kuwa majukumu ya msingi ya mbunge jimboni ni pamoja na kuwawakilisha wananchi wake bungeni katika masuala yote yenye masilahi yao, ikiwa ni pamoja na kuwa kiungo kati ya Serikali na wananchi katika masuala yote ya maendeleo.

Haya ndiyo majukumu ya msingi ya mbunge kwa wananchi, pia mbunge huyu pamoja na kwamba ana majukumu hayo jimboni, awapo bungeni hutekeleza majukumu ya kiujumla ya kibunge ambayo ni kushiriki kutunga sheria, kuisimamia na kuishauri Serikali, kupitisha bajeti na kulinda na kutetea masilahi ya ilani ya chama chake bungeni.

Baada ya kutaja majukumu hayo, lazima sasa tuelewe Mh. Mbowe na wabunge wote jukumu kuu jimboni ni kuwa kiungo cha uwakilishi kati ya Wananchi na Serikali. Suala la ujenzi wa miundombinu (Shule, barabara, madaraja, hospitali n.k), ulinzi na usalama wa wananchi, masoko ya mazao n.k siyo jukumu kuu la Mbunge la moja kwa moja.

Mbunge anashiriki kushauri Serikali katika kuleta maendeleo jimboni, anashiriki kujadili bajeti itayotengwa na serikali kuu kupeleka maendeleo kwa umma. Je Mbowe na wabunge wengine hawatekelezi jukumu kuu la kushauri serikali na kuitaka ipeleke maendeleo kwa kutenga bajeti chanya? Hawashauri vyanzo vya mapato ili kuongeza makusanyo yanayojaza bajeti yetu?

Mtajibu maswali haya kwenye comments zenu.

MDAU WA MAENDELEO NI NANI?

Mfumo wa kiutendaji katika kufanikisha maendeleo ngazi ya Mkoa/Wilaya kuna Mbunge, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Madiwani, ofisi za Halmashauri na watendaji wa serikali wenye majukumu tofuati lakini yote lengo ni kuleta maendeleo kwa umma. Lakini mdau muhimu ni WANANCHI wenyewe. Je, Ndeanka na wenzake wamewahi kwenda kwenye ofisi hizi za kiserikali KUPIGA KELELE na KUDAI MAENDELEO? Au wamewahi kuanzisha FUJO kwenye mikutano ya watumishi wa Serikali tofuati na mkutano wa Mbowe? Ndeanka na wenzake wanaweza kutuambia wao kama wananchi wadau wa maendeleo wametekeleza kwa kiwango gani jukumu la kueleta maendeleo?

TUIGE HUU KUWA NI MTINDO MPYA WA KUDAI MAENDELEO?
Kwa kuwa majimbo mengi sana kama siyo yote nchini yana HALI MBAYA sana kwenye maendeleo, na CCM ndiyo inaongoza kwa kuwa na majimbo mengi Bara na Zanzibar, tuwatake Ndeanka na wenzake waanze kuhamasisha FUJO na KELELE kwenye mikutano ya Wabunge,Madiwani, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya viongozi wa serikali, ili kudai maendeleo yetu. Tuvamie mikutano ya Mwenyekiti wa CCM Mh. Magufuli, mikutano ya Katibu Mkuu na Mwenezi wa CCM tufanye FUJO kuwashinikiza watupatie maendelo maana Chama Chao ndiyo wanaongoza Serikali na ILANI inayotekelezwa ni ya CCM.

Twendeni kwenye ukurasa wa Ndeanka Wa Mwalimu Urassa tumuombe ahamasishe hili kwenye kila mikutano ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa. Naamini ma-OCD na Askari watatumia busara kama za wale wa Hai kutuacha tupige kelele na tuvuruge mikutano.

Picha zimeambatanishwa.

1583323190253_adobe.jpeg
1583323061088_adobe.jpeg
1583323154911_adobe.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanahitaji kuanikwa hadharani maana vyombo vya habari vya kiuchunguzi Tanzania hakuna, vyombo vya habari bila kujua au kwa makusudi kwa kushirikiana na CCM wanatumika bila ufahamu kuwa wanaeneza hatari kubwa ya fujo inayoumiza inayofadhiliwa na CCM

Source:
Global TV online

N.B: Vyombo vya habari huu ndiyo wakati wa kuandika au kuweka hadharani habari za kiuchunguzi kama JF inavyofanya kazi nzuri kuweka ukweli hadharani kuonesha mchezo mchafu na wahatari wa CCM.
 
bagamoyo,
mkuu Tanzania ya leo haina waandishi wa habari,au vyombo vya habari ,wengi wao ni waoga,hawajui taaluma yao,hawana misimamo,njaa zinawasumbua,,kipindi nchi ina heshima na adabu kulikuwa na gazeti linalotoka kila jumamosi.

Mfanyakazi(lilikuwa chini ya jumuiya ya wafanyakazi)hili gazeti kama hukulinunua kabla ya 10am asubuhi ya jumamosi huwezi kuliona mitaani linauzwa,because waandishi wake walikuwa ni waandishi wenye utafiti(ninamkumbuka STAN,RIP),gazeti linguine ni motomoto hili nalo lilikuwa gazeti makini sana;sasa tuna Nipashe ambalo linaamua kujifungia lenyewe baada ya kuachapisha habari hasi kuhusu serikali ya chama dola!!!;bila ya JF nchi yetu imedumaa katika freedom of press.
 
Katika anga ya siasa za Tanzania, tukio kubwa na linaojadiliwa kwa sasa ni FUJO zilizo jitokeza kwenye mkutano wa Mh. Freeman Mbowe alipokuwa akihutubia wananchi jimboni kwake. Kundi la 'vijana' liliibuka na kuanza kupiga kelele na kutoa maneno yenye mlengo wa kutokubaliana na uongozi wa Mh. Mbowe. Madai yao yanaangukia kwenye umasikini wa jimbo, miundombinu mibovu na kukosekana kwa mikutano ya Mbunge mara kwa mara.

Katika ukurasa wa Facebook, ukienda kutafuta jina la Ndeanka Wa Mwalimu Urassa, ukifungua picha zake utakutana na picha ya kijana ambaye ndiye mmoja wapo aliohojiwa na kutoa malalamiko kuhusu Mh. Mbowe. Huyu ni kijana wa Chama Cha Mapinduzi (ngazi ya vijana), na aliyekuwa pia analalamika baada ya Ndeanka pia ni kijana wa Chama Cha Mapinduzi.

Sina tatizo na wao kuwa wanachama vijana wa CCM maana katika majimbo kuna wenye vyama na wasio na vyama, Viongozi wanao wajibu wa kuwahudumia wote. Ikiwa kuna masuala ya maendeleo hayapo sawa, ni HAKI ya wananchi kutoa malalamiko yao kwa Viongozi/Kiongozi wao.

MAJUKUMU YA MBUNGE NI YAPI?

Pamoja na kwamba kwa Tanzania mbunge analazimika kuwajibika kwa chama chake, ni vyema kujua kuwa majukumu ya msingi ya mbunge jimboni ni pamoja na kuwawakilisha wananchi wake bungeni katika masuala yote yenye masilahi yao, ikiwa ni pamoja na kuwa kiungo kati ya Serikali na wananchi katika masuala yote ya maendeleo.

Haya ndiyo majukumu ya msingi ya mbunge kwa wananchi, pia mbunge huyu pamoja na kwamba ana majukumu hayo jimboni, awapo bungeni hutekeleza majukumu ya kiujumla ya kibunge ambayo ni kushiriki kutunga sheria, kuisimamia na kuishauri Serikali, kupitisha bajeti na kulinda na kutetea masilahi ya ilani ya chama chake bungeni.

Baada ya kutaja majukumu hayo, lazima sasa tuelewe Mh. Mbowe na wabunge wote jukumu kuu jimboni ni kuwa kiungo cha uwakilishi kati ya Wananchi na Serikali. Suala la ujenzi wa miundombinu (Shule, barabara, madaraja, hospitali n.k), ulinzi na usalama wa wananchi, masoko ya mazao n.k siyo jukumu kuu la Mbunge la moja kwa moja.

Mbunge anashiriki kushauri Serikali katika kuleta maendeleo jimboni, anashiriki kujadili bajeti itayotengwa na serikali kuu kupeleka maendeleo kwa umma. Je Mbowe na wabunge wengine hawatekelezi jukumu kuu la kushauri serikali na kuitaka ipeleke maendeleo kwa kutenga bajeti chanya? Hawashauri vyanzo vya mapato ili kuongeza makusanyo yanayojaza bajeti yetu?

Mtajibu maswali haya kwenye comments zenu.

MDAU WA MAENDELEO NI NANI?

Mfumo wa kiutendaji katika kufanikisha maendeleo ngazi ya Mkoa/Wilaya kuna Mbunge, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Madiwani, ofisi za Halmashauri na watendaji wa serikali wenye majukumu tofuati lakini yote lengo ni kuleta maendeleo kwa umma. Lakini mdau muhimu ni WANANCHI wenyewe. Je, Ndeanka na wenzake wamewahi kwenda kwenye ofisi hizi za kiserikali KUPIGA KELELE na KUDAI MAENDELEO? Au wamewahi kuanzisha FUJO kwenye mikutano ya watumishi wa Serikali tofuati na mkutano wa Mbowe? Ndeanka na wenzake wanaweza kutuambia wao kama wananchi wadau wa maendeleo wametekeleza kwa kiwango gani jukumu la kueleta maendeleo?

TUIGE HUU KUWA NI MTINDO MPYA WA KUDAI MAENDELEO?
Kwa kuwa majimbo mengi sana kama siyo yote nchini yana HALI MBAYA sana kwenye maendeleo, na CCM ndiyo inaongoza kwa kuwa na majimbo mengi Bara na Zanzibar, tuwatake Ndeanka na wenzake waanze kuhamasisha FUJO na KELELE kwenye mikutano ya Wabunge,Madiwani, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya viongozi wa serikali, ili kudai maendeleo yetu. Tuvamie mikutano ya Mwenyekiti wa CCM Mh. Magufuli, mikutano ya Katibu Mkuu na Mwenezi wa CCM tufanye FUJO kuwashinikiza watupatie maendelo maana Chama Chao ndiyo wanaongoza Serikali na ILANI inayotekelezwa ni ya CCM.

Twendeni kwenye ukurasa wa Ndeanka Wa Mwalimu Urassa tumuombe ahamasishe hili kwenye kila mikutano ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa. Naamini ma-OCD na Askari watatumia busara kama za wale wa Hai kutuacha tupige kelele na tuvuruge mikutano.

Picha zimeambatanishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo dogo ni muumini wa kitu cha Arusha
 
Wanahitaji kuanikwa hadharani maana vyombo vya habari vya kiuchunguzi Tanzania hakuna, vyombo vya habari bila kujua au kwa makusudi kwa kushirikiana na CCM wanatumika bila ufahamu kuwa wanaeneza hatari kubwa ya fujo inayoumiza inayofadhiliwa na CCM

Source: Global TV online

N.B: Vyombo vya habari huu ndiyo wakati wa kuandika au kuweka hadharani habari za kiuchunguzi kama JF inavyofanya kazi nzuri kuweka ukweli hadharani kuonesha mchezo mchafu na wahatari wa CCM.

Unadhani viko huru kama social media
 
Hao vijana hata ukiwatazama sura zao wameshakata tamaa na maisha, ndio maana wameamua kujiunga CCM ili waleweshwe pombe kama makatuni watumike kuwadhuru watanzania wenzao, hawana tofauti na wale vijana wanaojiunga Al Shabab, wote ni wauaji tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ccccm mpya haina tofauti na criminal gangs kama mafia,alshababu tofauti yenyewe ni certified terrorist gang
 
Back
Top Bottom