Nape: CHADEMA wajiandae kuingia msituni

Green guard Ndo kikundi cha ugaidi tanzania
 
Hata ANC (Umkhoto we Sizwe) iliwahi kuitwa kikundi cha magaidi.....a freedom fighter to one is a terrorist to the other!
 
Nape anakazana kutoka povu wakati Rais wake ana omba mungu miezi iende haraka aachana na hatari iliyopo.Siasa za kinafiki nafiki zimepitwa na wakati, utakwenda kumdanganya Mtanzania yupi kwa wakati huu ambaye haelewi kwamba mnazunguka zunguka kwa maslahi binafsi. Hebu jifunzeni kidogo kwa yaliyojiri kwenye msiba wa MR Komba .
 

Unajua ndugu mtu akiwa na hulka ya UMBEA au KISEBENGO ama NGEBE (maneno ya zamani kidogo) mtu huyo huwa ni mwepesi wa kusikiliza na kusikia hata ukiwa unanong'oneza! na mara nyingi watu wanamna hiyo kwa bahati mbaya huwa hawafanikiwi kuyapata maneno yote sawasawa hivyo huwa na PEPO la UONGO linalowatia HASHIK ya kujazia maneno ya UONGO ambayo kimsingi hata wao hawakumbuki tena waliyatoa wapi! so ukiwauliza lazima wakimbie. Njia nzuri na nyepesi ya kumshinda mtu MUONGO ni wewe kusema UKWELI TU na usiwe mtu wa maneno MENGI.Pia nachelea kusema ELIMU haipo ndani ya SERIKALI inayotuongoza kwa sasa na kama ipo basi WANAHESABIKA NA HAWAPEWI NAFASI,(najua kuna PHD na MADEGREE YA ZAWADI hizo sizitambui kama ni ELIMU na zitambua kama ZAWADI BINAFSI) MAANA HAKUNA PENYE ELIMU PAKAWA NA USTAARABU WA UMASIKINI. Nimefurahia sana maelezo yako ndugu.
 

Mkuu salary slip unaweza kujenga hoja zako bila kunitaja...!!??

Nitashukuru sana
 
Last edited by a moderator:
Kumbe kazi ya katibu uenezi na itikadi CCM ni kutafuta kipi kinafanyika kwa wapnzani wako kisha kukipakapaka mafuta na kukibeba kama Agenda ya kuzunguka nayo mikoani.Aaah Kumbe ndiyo hivyo.Nilikua sielewi ila ndo naanza kuelewa sasa.
 
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye amerusha kombora kwa Chama cha Demokrasia na Maendekeo (CHADEMA) akidai makundi ya vijana wa ulinzi vya chama hicho (Red Brigade) yameandaliwa kwa ajili ya kuingia msituni kwa shughuli za ugaidi. Kauli hiyo aliitoa juzi wilayani Mpwapwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, inayoendelea mkoani Dodoma.

"CHADEMA wanaandaa vijana kupitia Red Brigade ili kuingia msituni na kuchukua madaraka ya nchi kwa mabavu. Wanafanya hivyo kwa sabababu wanajua hawawezi kuchaguliwa kwa njia ya kura wakati wa uchaguzi mkuu," alisema Nape na kuongeza: "Hawa wanaopiga kelele huko mitaani eti Red Brigade wanaandaliwa kwa ajili ya kulinda kura, naomba niwaulize hizo kura wanazotaka kulinda nani atawapigia? Hata hizo kura za kuiba zitatoka wapi," alisema.

Nape alidai kwamba tayari CCM wamepata taarifa nyeti za mpango ovu unaoandaliwa na CHADEMA kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwamba kuna mpango wa kuwatumia vijana wa Red Brigade.

"Taarifa tulinazo ni kwamba Red Brigade ni vikosi vinavyoandaliwa kwa ajili ya vitendo vya ugaidi na shughuli nyingine za ovyo. Taarifa ni kwamba hili ni kundi la kigaidi, wataanzishaje kundi la usalama wakati tunavyo vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi yetu?" alihoji Nape.

Nape alikituhumu pia chama hicho kwa kujihusisha na vitendo vya kuvunja amani katika matukio mbalimbali nchini ikiwamo yale yaliyotokea kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga na maeneo mengine kama Morogoro na kusababisha kuuawa kwa kijana muuza magazeti.
 
Anapaswa kujibiwa kisawasawa anaonyesha ujinga usio kifani anapoongea ujinga kama huo ili kutisha wananchi
 
Anapaswa kujibiwa kisawasawa anaonyesha ujinga usio kifani anapoongea ujinga kama huo ili kutisha wananchi

Nilishawahi kupigwa ban kwa kumjibu Huyu Nape. Sitaki tens yanikute, ila Nina mashaka sana na uelewa wa huyu jamaa
 
Kumbe FUTUHI huwa wanamuigiza yeye, mzee wa kukurupuka

Kwahiyo anataka kuonyesha kwamba dhaifu ni dhaifu kweli kweli. Unawezaje kuwa na vikundi vya kigaidi nchini mwako huku una sheria ya kuzuia ugaidi halafu huvichukulii hatua? Huyu nape anafikiri kwa kutumia mnduku.
 
Nape rudi kwa Mama yako Ngudu ukamsaidie kazi za nyumbani hiyo ya uenezi umeishindwa. kungekuwa na serikali makini wewe sasa hivi ungeombwa ushaidi wa hicho unacho ropoka ila kwa kuwa serikali iko likizo endelea.

Pia kwetu sisi wakina mami motto wa nje ya ndoa kama wewe hatumii jina la baba bali la mjomba wake mkubwa au babu, hivyo kwa kutumia jina la mzee Nnauye ni kutafuta umashuhuri na maslahi tu!!! Angalia tangazo la kumbukumbu ya kifo cha Mzee Nnauye jina lako halipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…