Akiongea leo mkoani Dodoma katika mkutano wa hadhara,katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,bwana Nape Nnauye , amekielezea kikundi cha Red Brigade kama kikundi cha kigaidi kinachoweza kuvunja amani ya nchi na kuwataka wananchi kuwa macho na vikundi vya aina hiyo.
CHANZO:ITV
My take;
Hivi kati ya Red Brigade na watuhumiwa wa Escrow,nani anahatarisha amani ya nchi hii?!
He is more than kilaza!
ha ha ha thread zako zinanifurahisha sana, zimejaa kila aina ya unafiki, sijui ulisomea wapi
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM-Taifa, Nape Nnauye amechoka. Amechoka kimwili,kiakili,kimaneno na kimatendo. Kila uchao na kila apitapo,Nape anasema yale yale na kwa namna ile ile. Sasa Nape ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana huko Dodoma. Nape ana ngekewa ya kupewa jukwaa na kuhutubia. Viongozi wa kitaifa waamuamini na kumpa nafasi.
Nape amechoka.Uchovu wake sasa u wazi kabisa. Anarudiarudia yale yale palepale na kwingineko.Yeye ni CHADEMA tuuuuuuuu...basi.Hana hoja za haja za kuwaambia wananchi na kuiuza vyema Ilani yetu ya CCM ya 2010-2015. Kuonesha Ilani ilivyotekelezwa kwa vitendo na vitengo kumemshinda Nape. Nape anang'ang'ania ugaidi,utapeli wa CHADEMA na mgogoro wa CHADEMA.
Nape habadili santuri. Hana jipya.Hapaswi kuendelea kupewa jukwaa na kuendelea kuwaboa na kuwakera wananchi. Apumzishwe. Kurudiarudia maneno na matendo ni uchovu wa dhahiri kwa Nape Nnauye. Nafasi adhimu anayopewa Nape apewe mwingne chamani. Kama vijana tunao wengi tu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
magaidi mnakazi nape kawagusa nape kapiga msumari wa moto.
ha ha ha thread zako zinanifurahisha sana, zimejaa kila aina ya unafiki, sijui ulisomea wapi
Kwa kiwango cha Division IV ya point 29 katika mtihani wa kidato cha Nne aliyoipata Nape Nnauye hawezi kuwa na uwezo wa kufanya hicho unachotarajia Mzee Tupatupa.
Katika hili wala siwezi kumlaumu kwakuwa hicho ndio kipeo chake cha uelewa na hata ccm wamfanyeje hawezi kufanya zaidi ya hapo kwakuwa akili hiyo hana. Apeche alolo...
Wewe kila siku unawadanganya wanaJf kuwa ni kiongozi wa CCM Makao Makuu.
Sasa unawaomba kina nani wampumzishe wakati wewe ndiyo unatakiwa umpumzishe?.
Au umesahau kama wewe ni kiongozi wa CCM makao Makuu.
Vijana wa BAVICHA mnafurahisha sana.
Unakuja kwa unafiki wa kutoa ushauri baada ya kupata kipigo cha hoja.
Mingoi nijalie hali ya afya ya Naibu Spika Job Ndugai. Nasikia mmemwakyembe, je taarifa hizo zina ukweli kiasi gani?Mkuu Mwita Maranya naona umefufuka kuongeza nguvu katika homa ya October.
Hawezi kujibu hoja zozote zaidi ya kuumiza masikio ya wananchi kwa kelele kwenye mic tu
Naona boss mwenyewe umeamua kuja ili kumhami kijana wenu.
Mbona mbunge wa Kongwa Job Ndugai hatujamuona jana katika mapokezi na ziara ya Kinana Mkoani Dodoma? au hizi taarifa ya kwamba mmemwakyembe ni za kweli?
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM-Taifa, Nape Nnauye amechoka. Amechoka kimwili,kiakili,kimaneno na kimatendo. Kila uchao na kila apitapo,Nape anasema yale yale na kwa namna ile ile. Sasa Nape ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana huko Dodoma. Nape ana ngekewa ya kupewa jukwaa na kuhutubia. Viongozi wa kitaifa waamuamini na kumpa nafasi.
Nape amechoka.Uchovu wake sasa u wazi kabisa. Anarudiarudia yale yale palepale na kwingineko.Yeye ni CHADEMA tuuuuuuuu...basi.Hana hoja za haja za kuwaambia wananchi na kuiuza vyema Ilani yetu ya CCM ya 2010-2015. Kuonesha Ilani ilivyotekelezwa kwa vitendo na vitengo kumemshinda Nape. Nape anang'ang'ania ugaidi,utapeli wa CHADEMA na mgogoro wa CHADEMA.
Nape habadili santuri. Hana jipya.Hapaswi kuendelea kupewa jukwaa na kuendelea kuwaboa na kuwakera wananchi. Apumzishwe. Kurudiarudia maneno na matendo ni uchovu wa dhahiri kwa Nape Nnauye. Nafasi adhimu anayopewa Nape apewe mwingne chamani. Kama vijana tunao wengi tu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Wewe siasa zako ni Jamiiforums.
Hufahamu hata kushika mic kwenye mkutano wa kisiasa wa hadhara achilia mbali kuongea na kueleweka.
Uenyekiti wa Bavicha uliota mbawa.
Tisha toto ya kwenda mahakamani ikaishia kwenye mitandao.
Ujumbe wa Kamati Kuu ukaishia kwenye makaratasi.
Kwa sasa unasubiri hisani ya Katibu Mkuu wa CHADEMA.