Nape: CCM imeweza kuzuia "mafuriko" kwa mkono

Nape: CCM imeweza kuzuia "mafuriko" kwa mkono

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,787
Reaction score
165,481
Chama cha Mapinduzi(CCM) kimewatakila kila la kheri wanachama wake waliotangaza kutogombea,wanaotaka kuhama na waliohama chama hicho.

Pia,Nape amesema CCM imeweza kuzuia mafuriko kwa mkono ila anashangaa wanahabari hili hawalisemi wakati mtia ni mmoja aliposema huwezi kuzuia mafuriko kwa mkono wanahabari waliandika sana ila baada ya CCM kuzuia mafuriko kwa mkono waandishi wa habari hawasemi.

Chanzo: Nipashe

My take:

Lowassa,kwa kauli hizi,ni wazi CCM huna thamani tena licha ya kukaa kwako kimya wakati wa kashifa ya Richmond ili kuikoa serikali ya chama chako isianguke.

Mr. Lowassa,be bold and do the right thing now and not tomorrow or even the day after tomorrow.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejigamba kwamba kimeweza kuzuia ‘mafuriko' kwa mikono huku kikiwatakia kila la kheri baadhi ya makada wake waliotangaza kutogombea kupitia chama hicho pamoja na wale waliokihama na wanaotaka kukihama.

Mwishoni mwa wiki iliyopita waliokuwa madiwani jimbo la Monduli kupitia CCM mkoani Arusha, walitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku wabunge wa viti maalum, Ester Bulaya na James Lembeli aliyekuwa Mbunge wa Kahama wakitangaza kutogombea kupitia chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na NIPAHE jana alisema CCM hakina uwezo wa kuzuia mtu anayetaka kukihama kwa sababu hiyo ndiyo demokrasia.

Aidha, Nape alisema vyombo vya habari vilimnukuu aliyekuwa mgombea urais kupitia CCM, Edward Lowassa akisema kuwa watu hawawezi kuzuia ‘mafuriko' kwa mikono na kwamba CCM imeweza kufanya hivyo, lakini habari hizo haziandikwi.

Alisema wanachama wanaotaka kuhama hawawezi kuzuiwa kwa namna yoyote na kwamba hilo ni jambo la kawaida kufanyika kwa kada yoyote.

Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea urais, ulivyokuwa ndani ya CCM, alisema ulifuata utaratibu na kanuni zote na kwamba kama maneno mengi yataendelea kusemwa atatoa video inayoonyesha kila kitu kilivyokuwa ndani ya kikao cha Kamati Kuu (CC).

Kuhusu makada waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM, Nnauye alisema baada ya Baraza la Madiwani kuvunjwa hapakuwa tena na wawakilishi wa aina hiyo.

Alisema watu waliojiunga na Chadema huko Monduli mkoani Arusha hawakuwa Madiwani kwa kuwa Baraza la Madiwani likishavunjwa hakuna tena nafasi hizo za uwakilishi.

Chanzo: Nipashe
 
Lowassa awe bold ili iweje,kwanini wapambe mnapenda kumshurutisha huyu mzee aseme yasiyo stahili,nafikiri mungekuwa mumeyashika maneno ya busara aliyosema Amani Abeid Karume,alisema mkizidi kudai maelezo yatolewe kwanini mtu wetu kakatwa ,basi yatatoka ambayo hata hamuyajui na ambayo yatamkosesha staha hata hiyo aliyonayo huyo aliyekatwa,watu sio wajinga kama mnavyodhani,hata Lowassa naye sio mjinga kama mnavyodhani,wapambe huu ni muda wa kuangalia shughuli nyingine,mambo ya kumtegemea Lowasa awape kiki kwa sasaishakuwahistoria mwacheni Lowasa apumzike,Tanzania bila Lowasa inawezekana,pia msisahau miluzi mingi hupomtezea mbwa timing,atawasikiliza wangapi?
 
Eti wamezuia mafuriko kwa Mkono.......Mwenezi kwa kuongea hajambo, nashangaa vile asivyoona wanachama wake wakupukutikia Upande mwingine.......mbona hawazuii, au alitegemea mafuriko gani zaidi ya hayo?
 
nape aache mipasho, ajenge hoja za maslahi ya chama na taifa kwa ujumla....
hii inaonyesha ni hamna jipya kutoka ccm.
 
Lowassa...come out...speak out..loudly...

Be fast...ushatukanwa, onewa, fedheheshwa vya kutosha, hama CCM sasa, na UWE UKAWA rasmi, na huyu mtoto mdogo sana Nape, hawezi kukudharau kiasi hiki, umkomeshe ktk jukwaa la kampeni na kuibomoa CCM..

Lowassa, ukimya ukizidi SIO BUSARA NI UJINGA, kuna wakati wa kukaa kimya, ila sio ktk hali hii yako tunayoona...!!!

Sema sasa, ingiwa ukawa, sio huoni huyu mtoto Nape kashasema, wanaotaka kuhama waondoke...

Please Lowassa, unajipanga nn...? Time is
running out..!!
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejigamba kwamba kimeweza kuzuia ‘mafuriko’ kwa mikono huku kikiwatakia kila la kheri baadhi ya makada wake waliotangaza kutogombea kupitia chama hicho pamoja na wale waliokihama na wanaotaka kukihama.

Mwishoni mwa wiki iliyopita waliokuwa madiwani jimbo la Monduli kupitia CCM mkoani Arusha, walitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku wabunge wa viti maalum, Ester Bulaya na James Lembeli aliyekuwa Mbunge wa Kahama wakitangaza kutogombea kupitia chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na NIPAHE jana alisema CCM hakina uwezo wa kuzuia mtu anayetaka kukihama kwa sababu hiyo ndiyo demokrasia.

Aidha, Nape alisema vyombo vya habari vilimnukuu aliyekuwa mgombea urais kupitia CCM, Edward Lowassa akisema kuwa watu hawawezi kuzuia ‘mafuriko’ kwa mikono na kwamba CCM imeweza kufanya hivyo, lakini habari hizo haziandikwi.

Alisema wanachama wanaotaka kuhama hawawezi kuzuiwa kwa namna yoyote na kwamba hilo ni jambo la kawaida kufanyika kwa kada yoyote.

Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea urais, ulivyokuwa ndani ya CCM, alisema ulifuata utaratibu na kanuni zote na kwamba kama maneno mengi yataendelea kusemwa atatoa video inayoonyesha kila kitu kilivyokuwa ndani ya kikao cha Kamati Kuu (CC).

Kuhusu makada waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM, Nnauye alisema baada ya Baraza la Madiwani kuvunjwa hapakuwa tena na wawakilishi wa aina hiyo.

Alisema watu waliojiunga na Chadema huko Monduli mkoani Arusha hawakuwa Madiwani kwa kuwa Baraza la Madiwani likishavunjwa hakuna tena nafasi hizo za uwakilishi.

CHANZO: NIPASHE
 
KuNa watu wanasema Kikwete kazuia mafuriko kwa Pen ya 200
 
Bora ametambua kuwa kuna mafuriko,lakini je ni kweli mafuriko yamezuiwa kwa mkono au ni mafuriko yenyewe yameinama kama kobe anaetunga sheria?na je hayo mafuriko yatakapomaliza kutunga sheria na kuinuka hiyo mikono itamdu kuendelea kuyazuia?.
 
* Kwa nje anasema kila kitu kipo sawa...lakini kwa ndani hali ya chama tawala ni mbaya....
 
Acha akae kimya tu atakapokuja kusema ashakuwa kama mrema na hakuna atakaemsikilza watu tutajua anastres,mda muafaka kwake ni huu
 
mkuu kweli Nape ni kajamaa na unene wote ule?! bac wewe utakuwa umempita mbali Wasira kwa unene ukianza na tumbo.
11755248_505491269598852_1669477192270364333_n.jpg
 
Ha ha ha ha Nape.. Hayo sio maneno ya kujenga.. Mnategemea ccm itashinda kwa kumwaga hela upinzani ufarakane, wakati huko kwenu mko vipande.. Ni vizuri muanze kujiandaa kisaikolojia.. Kama mwenyekiti wenu JK alivyowashauri..
 
Back
Top Bottom