KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, juzi alikumbana na msukosuko wa kuzomewa na wananchi wakati akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mkoma, wilayani Rorya, mkoa wa Mara.
Nape alizomewa na wananchi hao waliokuwa wakimsikiliza mara tu baada ya kutoa kauli za kukikejeli Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambazo zilitafsiriwa kama matusi na kashfa kwa chama hicho.
Katika uchaguzi huo mdogo kwenye kata hiyo, CHADEMA pia imemsimamisha mgombea wa udiwani. Na hivyo kauli ya Nape kuwa chama hicho ni cha wahuni, kinachotumia salamu ya kunyoosha vidole viwili juu kama alama ya kutukana, ilionekana kuwakera wananchi.
"Hata salamu yao ni ya kihuni, ni ishara ya matusi. Na ninyi vijana mnashabikia hiyo bila kujua. Hivyo salamu haiwafai kuonyesha vidole viwili; ni salamu inayowafaa vijana wahuni," alisema mwanasiasa huyo huku akinyoosha salamu hiyo kwa vidole vyake.
Huku akitamka maneno mengine ambayo kimaadili hayaandikiki kwenye chombo cha habari makini kama Tanzaima Diama, Nape aliendelea kuikejeli CHADEMA hatua iliyowakera wananchi na wengi wakaanza kuguna.
Hata hivyo, wakati akiendelea na tafsiri zake kuhusu salamu za CHADEMA ikiwemo ile ya kukunja ngumi na kusema ‘people's power', ghafla baadhi ya wananchi walianza kumzomea, huku sauti nyingine zikisema, ‘Ongea sera…huo uwongo..unatudanganya.'
Hali hiyo iliendelea kuzusha zogo kutoka kwa wananchi wengi kila upande mkutanoni hapo na zomeazomea ya ‘ooh…oooh' ikakolea na kusababisha wananchi kuanza kuondoka.
Nape alionyesha kupuuza hali hiyo na hivyo kuendelea kusisitiza kuwa wakichagua diwani kutoka CHADEMA hawatapata maendeleo yoyote kwa sababu chama hicho hakina serikali.
Uzuri Nape yupo hapa JF atatuambia nini kilimsibu huko Rorya.
Hivi na ww kwa akili yako unategemea tanzania daima liandike mema ya ccm. Hili lajulikana ni gazeti la mbowe, unataka wenzako wanyimwe mshahara km wasipo andika mabaya ya ccm. TANZANIA DAIMA = MBOWE = CDM , unategemea nn sasa hapo !
Hapo kwenye red panadhihirisha kuwa Nape Nnauye ni mlemavu wa kufikiri. Ishara ya vidole viwili ni sign of victory na hii sign inajulikana universally yani mtoto wangu wa baby class ukimuonyesha alama ya vidole viwili anakuambia ni sign of victory. Alama hii inatumika kama ishara ya ushindi.Katika uchaguzi huo mdogo kwenye kata hiyo, CHADEMA pia imemsimamisha mgombea wa udiwani. Na hivyo kauli ya Nape kuwa chama hicho ni cha wahuni, kinachotumia salamu ya kunyoosha vidole viwili juu kama alama ya kutukana, ilionekana kuwakera wananchi.
"Hata salamu yao ni ya kihuni, ni ishara ya matusi. Na ninyi vijana mnashabikia hiyo bila kujua. Hivyo salamu haiwafai kuonyesha vidole viwili; ni salamu inayowafaa vijana wahuni," alisema mwanasiasa huyo huku akinyoosha salamu hiyo kwa vidole vyake.
Huku akitamka maneno mengine ambayo kimaadili hayaandikiki kwenye chombo cha habari makini kama Tanzaima Diama, Nape aliendelea kuikejeli CHADEMA hatua iliyowakera wananchi na wengi wakaanza kuguna.
Hata hivyo, wakati akiendelea na tafsiri zake kuhusu salamu za CHADEMA ikiwemo ile ya kukunja ngumi na kusema ‘people's power', ghafla baadhi ya wananchi walianza kumzomea, huku sauti nyingine zikisema, ‘Ongea sera…huo uwongo..unatudanganya.'
Hapo kwenye red panadhihirisha kuwa Nape Nnauye ni mlemavu wa kufikiri. Ishara ya vidole viwili ni sign of victory na hii sign inajulikana universally yani mtoto wangu wa baby class ukimuonyesha alama ya vidole viwili anakuambia ni sign of victory. Alama hii inatumika kama ishara ya ushindi.
Sikutegemea kijana msomi kama Nape Nnauye unaweza kuchemka kutafsri ya alama hii ya kimataifa na umeamua kufanya siasa za maji ya chooni kama layman, Inshort nimegundua Nape Nnauye umepanic, hali ni tete juu yako na CCM, kazi uliyopewa ni ngumu na sio nyepesi kama ulivyodhani awali.
hand showing victory sign
View attachment 38157 Nape Nnauye nakushauri uwe na tabia ya kujisomea ile uende sawa na kizazi hichi, tenga mda na tengeneza ratiba ya kujisomea vitu mbalimbali kwa manufaa yako.
rudi kule kwenye jukwaa la watotohata mumseme nape hawezi kata tamaa lile ni greda anakatua go nape go on!
Hivi na ww kwa akili yako unategemea tanzania daima liandike mema ya ccm. Hili lajulikana ni gazeti la mbowe, unataka wenzako wanyimwe mshahara km wasipo andika mabaya ya ccm. TANZANIA DAIMA = MBOWE = CDM , unategemea nn sasa hapo !
Tingatinga lenyewe limeshasalimu amri na kujituliza huko Mvumi ije iwe hako kagreda kanako piga kelele za kujivua gamba? Kwanza hata huko CCM wamekachoka ndio maana kamepigwa red card Igungahata mumseme nape hawezi kata tamaa lile ni greda anakatua go nape go on!