Nape atoa msimamo wa CCM dhidi ya posho za wabunge

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Sema tu niko na aleji na TBC sijui hata alikuwa anaongea nini. Karibuni niko natupia Kili Bariiiid. Mdogomdogo mwendo wa kobe na bendi moja ya Bakulutu. Karibuni sana.
 
Naöna leo kaongea maneno yamenivutia!amepinga ongezeko la posho kuwa linaongeza gap ya wenye nazo na ambao hawana.
 
Naöna leo kaongea maneno yamenivutia!amepinga ongezeko la posho kuwa linaongeza gap ya wenye nazo na ambao hawana.

labda anaendeleza siasa zake za ''mjadala wa posho si wa chadema peke yake''
 
Sema tu niko na aleji na TBC sijui hata alikuwa anaongea nini. Karibuni niko natupia Kili Bariiiid. Mdogomdogo mwendo wa kobe na bendi moja ya Bakulutu. Karibuni sana.

mmemnukuu vibaya kuhusu posho au mpaka akanushe?? alisema posho ni muhimu maana gest ni bei gali 100.000.00 kwa usiku mmoja naungana na waheshimiwa wabunge by jr....,
 
Hii ni nitoke vipi baada ya sherehe za miaka 50 ya Tan... (sorry, nimesahau hiyo nchi iliyotimiza miaka 50 inaitwaje?
 
Nakupongeza Nape kwa kauli yako ya kupinga posho za wabunge. Huo ndio uzalendo bila kujali itikadi za chama chako pampja na kuwa wana ccm wenzako hawatafurahia msimamo wako. Mi siipendi CCM kwa maovu yake, ila wanapofanya jambo jema kama ulilolifanya (nadhani ni msimamo wa chama??????, maana ulikuwa ofisini Lumumba) ni vyema kupongeza mema aliyoyafanya mtu. Nakupongeza kwa hili, hili ni jema kabisa
 
Nakupongeza Nape kwa kauli yako ya kupinga posho za wabunge. Huo ndio uzalendo bila kujali itikadi za chama chako pampja na kuwa wana ccm wenzako hawatafurahia msimamo wako. Mi siipendi CCM kwa maovu yake, ila wanapofanya jambo jema kama ulilolifanya (nadhani ni msimamo wa chama??????, maana ulikuwa ofisini Lumumba) ni vyema kupongeza mema aliyoyafanya mtu. Nakupongeza kwa hili, hili ni jema kabisa

ndg yangu Nape anatabia ya kujikana. Subiri auliswe na wakubwa kasema nini, utasikia atakavyojibu. Nape si lolote si chochote
 
Kila kauli ya viongozi wa CCM na serikali kulitolea kauli swala hili la posho linaendelea kutuchanganya na kudhihirisha usanii wa CCM na serikali yake.Je Makinda sio sehemu ya CCM?Iko wapi Ikulu kulitolea tamko swala hili?Niwazi kua swala hili lilikua limekubariwa katika ngazi zote CCM ,Serikali na Rais mwenyewe JK.Na swala hili lilitaka kupitishwa kimya kimya baada ya baada ya kuibuliwa na wabunge wa CHADEMA na reaction ya jamii na wanaharakati CCM na Serikali wanatafuta mlango wa kutokea soon tutasikia kauli ya JK.AIBU MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
NAPE_PC[1].jpg


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hivi karibuni kumeibuka mjadala juu ya ongezeko la posho za wabunge kwa karibu ya asilimia 200, kutoka sh. 70,000 hadi sh. 200,000.

Malipo hayo yaliyoibua mjadala baina ya wadau mbalimbali, ni yale yanayohusisha posho ya kikao cha bunge kwa siku.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefuatilia kwa makini suala hilo la nyongeza ya posho hiyo ya wabunge kama lilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na baadae kutolewa maelezo na Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilila na Spika wa Bunge Anne Makinda.

Kwa namna suala lenyewe linavyopewa msukumo, CCM imeona si vema kukaa kulikalia kimya na hivyo imetoa msimamo wake kama ifuatavyo:-


i. Linapotekelezwa jambo lolote kwa kigezo cha ugumu wa maisha au kupanda kwa gharama za maisha, ni lazima jambo husika lilenge kutatua ugumu huo wa maisha kwa makundi yote katika jamii na si kwa makundi machache ndani ya jamii.


ii. Kwa kuongeza kiwango hicho cha posho kwa wabunge ni kuongeza pengo/tofauti ya mapato kati ya wenye nacho na wasionacho katika jamii yetu hasa kwa kuegemea baadhi ya makundi.

iii. Bunge ni chombo muhimu cha kutunga sheria, kinapoibuka na madai kwamba sababu za kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma kama alivyoainisha Spika wa Bunge, ndiyo inasababishahofu na mashaka miongoni mwa Watanzania. Na kwa kweli swali kubwa kwa Watanzania hao ni je, maisha yanapanda Dodoma pekeake na kwa wabunge tu?


Hivyo basi CCM inashauri kwa kuzingatia masilahi mapana ya nchi na jamii yetu kwa ujumla, waheshimiwa wabunge wetu na mamlaka zingine zinazohusika na swala hili, kulitafakari upya jambo hili. Tunaamini busara itatumika kuachana na jambo hili, kwani kuendelea nalo kunaweza kutafisiriwa ni kuwasaliti watendaji katika sekta nyingine wakiwemo Walimu, askari, Madaktari na wengineo.

Ni muhimu ifahamike kuwa kuongoza ni kuonesha njia, hivyo si sahihi kwa wabunge kuonesha njia kwa kujiongezea posho peke yao kwa kisingizio cha ugumu wa maisha huku wakiwaacha wananchi ambao ndiyo wanaowawakilisha bungeni wakikosa nafasi ya kupunguza ugumu wa maisha unaowakabili, jambo ambalo ni hatari.


Katika hatua nyingine, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawapongeza sana Watanzania kwa ujumnla wao, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kwa kushiriki kwa amani na utulivu katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Ushiriki wao kwa pamoja, umeyafanya maadhimisho hayo yafane sana. CCM inaamini kuwa maadhimisho haya ya miaka 50 yatatumika kuendelea kujenga uzalendo, umoja na mshikamano wan chi yetu katika kufikia maendeleo.

Imetolewa na:-



Nape M. Nnauye,


KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA ITIKADI NA UENEZI.
 
Nape amezungumza vizuri sana na ameonyesha msimamo wa chama kuhusu hili suala la posho. Kwa undani zaidi wa aliyoyaongea leo Chanel ten unaweza ukafuatilia hii link hapa chini
MICHUZI
 
Basi kuna mtu anatakiwa ajiuzuru lakini ctoshangaa akitokea na kudai eti alikuwa anatikisa kiberiti tu.Siasa nyepesi kwenye mambo mazito zinatukost sana
 
Back
Top Bottom