Nape atahadharisha watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape atahadharisha watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by the horse, Jun 20, 2012.

 1. t

  the horse JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Leo ni siku ya wakimbizi duniani. Tanzania inaungana na Mataifa mengine duniani katika kuadhimisha siku hii. Tangu kupata Uhuru Tanzania imekuwa Taifa lililo mstari wa mbele katika kusaidia wakimbizi kutoka katika Nchi mbalimbali hasa zile ilizopakana nazo.

  Tanzania ni nchi ambayo imezungukwa na kupakana na Nchi zenye machafuko, aidha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kama ilivyokuwa kwa Burundi na Rwanda, pia imepakana na nchi zenye makundi ya waasi wanaopinga serikali zao na kusababisha machafuko kama vile Uganda, Somalia, Sudan na Kongo, lakini pia imepakana na nchi zenye machafuko ya kisiasa kama vile Kenya.

  Siku za hapo nyuma kidogo, kutokana na Athari mbalimbali zilizotokana na Idadi kubwa ya wakimbizi hapa nchini, ambapo ilikadiriwa kufikia 1,000,000 Serikali ililazimika kubadili sera ya wakimbizi ambayo ilitoa fursa ya kila familia kupatiwa hekta mbili na nusu za ardhi na kuanzisha makazi na badala yake kuwatengea maeneo maalum ya makambi, pamoja na hilo Serikali iliendelea kutafuta namna ya kuondokana na Athari hizo na hivyo kufikiria njia mbadala katika kutafuta namna nzuri ya kuondokana na Athari zilizoletwa na wakimbizi kama uharibifu wa mazingira, ujambazi, wizi lakini pia wakimbizi walikuwa ni mzigo mkubwa kwa serikali kwani walitakiwa kupata stahili zote za maisha ikiwemo, chakula, malazi, mavazi pamoja na Ulinzi. Gharama za huduma hizi zote zilikuwa chini ya Serikali ingawa baadhi ya Serikali za Mataifa makubwa zilisaidia pamoja na Mashirika kama UNICEF, OAU na UNHCR.

  Katika kufikiri juu ya kuondokana na tatizo hili, Serikali ya Awamu yaTatu na Nne chini ya Rais Jakaya M. Kikwete waliamua kuwa ni vema kwenda katika nchi husika na kushauri njia sahihi za mazungumzo na kumaliza tofauti zao ili kuweza kupata Amani ambayo itawezesha wakimbizi kurudi katika Nchi zao. Juhudi hizi zilizaa matunda kwa Baadhi ya Nchi ikiwemo Burundi, Rwanda na Kenya hivi karibuni.

  Aidha, katika kuadhimisha siku hii ya wakimbizi, lipo jambo la msingi ambalo kama Taifa lazima tujifunze na tulielewe kutoka katika mafunzo hayo. Jambo lenyewe ni Umuhimu wa kutunza Amani yetu. Sehemu zote ambazo zimezalisha wakimbizi hazikuwa na sababu nyingine kama njaa ama majanga ya asili bali ni kutokana na sababu kuu moja ya kuvunjika kwa Amani. Lakini tukienda mbele zaidi na kujiuliza ni nini chanzo cha uvunjifu huo wa Amani, tunapata jibu kuwa ni kutokana na Uroho wa Madaraka na Ukabila.

  Katika mambo ya msingi ambayo kama Taifa tulifundwa na kuaminishwa ni pamoja na kupinga namna yoyote ya kubaguana kikabila, kidini ama kikanda. Lakini pia tukafundwa katika misingi ya Uzalendo na Utaifa pamoja na Kuheshimu Utawala wa Sheria na Mamlaka ya Nchi. Lakini hivi sasa hali imekuwa Tofauti, tayari wapo watu ambao wameanza kutia doa na kuchokonoa yale yanayotujenga kama Taifa lenye Amani, tayari wapo wanaonadi Ubaguzi na Utengano, wapo wanaodharau na hata kubeza mamlaka husika na hawaheshimu tena Utawala wa Sheria. Mambo haya yanafanywa kwa jina la siasa, tumekuwa tukishuhudia kauli pamoja na matendo yanayodhihirisha muelekeo huu mbaya.

  Hali hii haitoi picha nzuri katika mustakabali wa kujenga , kuendeleza na kuimarisha Taifa letu. Tanzania tunao utamaduni wa kuheshimu Mamlaka na Utii wa Sheria. Lazima wote tangu sasa tuamue kuchukua hatua thabiti kulinda umoja na amani yetu, kwani hata sisi twaweza kuwa wakimbizi pia. Hatuna kinga ya kuzuia hilo isipokuwa kurudi katika misingi yetu iliyowekwa na waasisi wa Taifa hili. Jukumu la kustawisha na kulinda umoja na amani yetu ni letu wote. Tuilinde Tanzania yetu, tujivunie Utaifa wetu.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  ignorance ye' carasa!!
   
 3. t

  the horse JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  i have reasons why i support this gentlemen..,he prorate his prose....!
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nape anautangazia umma wa Tanzania kuwa hali ya nchi ni tete? Ningetaka kusikia kauli ya serikali na hasa waziri wa mambo ya ndani au/na jeshi la polisi.

  Haiwezekani hii kauli imetoka hivi hivi, penging ama Nape anajua mpango unaosukwa na hivyo anaandaa umma kwa mgogoro! Uchaguzi wa 2010 tulisikia kelele za udini na watu wakahoji udini uko wapi mbona huku mtaani watu wanaishi vizuri licha ya kuwa na dini tofauti? baadae ikaonekana ni mtaji wa kisiasa. Sasa Nape anakuja na statement ya aina nyingine! Kuna nini?
   
 5. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,180
  Likes Received: 1,904
  Trophy Points: 280
  Ni nani wa kuchukua hatua ikiwa hadi viongozi wanalalamika, na kuchoche hali hiyo kwa kukumbatia UJINGA, UMASKINI, MARADHI NA UFISADI? Ada ya mja hunena Muungwana ni vitendo!
   
 6. R

  Rapkatuni Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  this is very true..,kama watanzania wataliangalia hili kwa umakini wanaweza kukubaliana na Nape katika hili.
   
Loading...