Kuna kiongozi mmoja wa ccm niliwahi kumwambia anachojaribu kufanya Nape hakiwezekani! Mwisho zigo atabaki nalo! Nape alianza kumgusa lowasa wazi wazi toka uvccm! Na recently amekuwa akijaribu kujenga taswira ya kutenganisha chama na mafisadi lakini hili hata wanajf walimuonya maana CCM ilipofikia ni kama yule mdudu ambaye ili maisha yaendelee lazima afe kwa kupasuka tumbo na watoto kutoka ccm imefika mwisho na wamegawanyika sana! Nape amethubutu mfupa mgumu sana!Mkuu with all due respect hakuna anayepinga kwamba Nape alichofanya ni kitendo cha kishujaa- nadahini wengi wetu tunamkubali ameweza kusema kile ambacho wengi ndani ya chama chao wameogopa kusema- tatitzo ni kwamba alishindwa kusoma mazingira kwani alitakiwa kujua waliomtuma ni watu wa aina gani, kiongozi wa juu aliyepo ni mnafiki kupindukia hilo alitakiwa kulijua na kuwa makini kwenye utendaji wake. Katibu mkuu aliwahi kumpinga hadharani kuhusiana na suala la kutaja majina, hakupata sapoti yoyote toka kwa mwenyekiti-kwangu mimi hiyo ilikuwa ni dalili tosha ya kuwa makini, EL alipozungumza na mzee Msekwa aliweka wazi kwamba hayo anyoambiwa siyo anayoambiwa na mwenyekiti pale wanapozungumza, mwenyekiti hakubisha na wala hakutolea ufafanuzi kauli hiyo! Sasa kwa akili ya kawaida usingeona kuna shida hapo?
This is rather sad; hivi kweli tatizo la CCM ni NAPE. As a matter of fact Nape angepewa pongezi na kuungwa mkono na wana CCM wanaotaka mabadiliko ya kweli. Alichokifanya Nape hadharani hakijawahi kufanywa na kionogozi yeyote wa CCM. Wengi wa wale wanaojiita viongozi au wanajionesha kuwa niviongozi hawajawa na ujasiri wa kusimama na kuiita limau limau na chenza chenza! Tangu mwanzo wa sakata hili sikuwahi kusema lolote juu ya Nape lakini ukweli ni kuwa Nape amefanya kilichowashinda wengi na kama aliamua kuondoka kwenye vikao vyao pia ni uamuzi wa akili kwa sababu kwanini watu wakae mahali ambapo hawawezi kusimamia walichokisea. Kama watu wote wenye nguvu Tanzania wanakutanika kwenye chumba kimoja halafu wanashindwa kuchukua uamuzi ambao wanajua walipaswa kuukua bado wanaonekana wamefanya la maana?
Hivi kweli mnataka kusema ndani ya kundi zima la watu wa Kamati Kuu na NEC hakuna mtu aliyekuwa na uwezo wakujibu hoja zinazodaiwa kutolewa na Lowassa, really? Nape hata akijiuzulu kesho, atakuwa amejionesha kuwa amethubutu kufanya kilichomshinda fisi.
Kwa wenye negativity dhidi ya Nape pasipo kujali UKWELI [REALITY] ya mwenendo mzima wa Matendo ya CCM dhidi ya TAIFA hakika subilieni TUTAWATAFUTA KUWAKUMBUSHA MANENO YENU HUMU NDANI, ILI MKANE MLICHOONGEA MSISAHAU MANENO YA MTOTO WA BABA WA TAIFA KUWA RACHEL NINI?
Mheshimiwa Mwenyekiti sina tatizo na kaka Yangu Lowasa lakini ulipomuinua Mkono Uko Monduli site [Wananchi] wakasema HIKI NI NINI?
Mheshmiwa Mwenyekiti nampenda Ndugu yangu Chenge wanamuita Mzee wa Vijisenti hilo Mimi Sina Hakika Nalo ulipomuinua Mkono huko Maswa site [Wananchi] wakasema HIKI NDIO NINI?
Mheshimiwa Mwenyekiti anakotembele Rostam Mimi Nisifiki na Naye afiki Mimi nilipo, ulipomuinua Mkono uko IGUNGA site [Wananchi ] wakauliza HIKi NINI?
Sasa nyie mnaoshabikia PUMBA [Kisa Wanachadema] mnatupa shaka sie tusio wananchama wa chama chochote kweli nyie ni wapenzi wa Nchi.
Tunawasubilia manake kwa wanaojua michezo ya CCM tegemeeni Chochote Kipya wakati wowote.Time will tell.
Kuna kiongozi mmoja wa ccm niliwahi kumwambia anachojaribu kufanya Nape hakiwezekani! Mwisho zigo atabaki nalo! Nape alianza kumgusa lowasa wazi wazi toka uvccm! Na recently amekuwa akijaribu kujenga taswira ya kutenganisha chama na mafisadi lakini hili hata wanajf walimuonya maana CCM ilipofikia ni kama yule mdudu ambaye ili maisha yaendelee lazima afe kwa kupasuka tumbo na watoto kutoka ccm imefika mwisho na wamegawanyika sana! Nape amethubutu mfupa mgumu sana!
Mwanakijiji, kutokana na hoja yako, kuwa Nape kafanya kile ambacho wengi ndani ya CCM kimewasinda, na matokeo yake ndiyo hayo yanayomfika, ili aweze kuthibitisha utofauti wake na wengine ndani ya CCM, anatakiwa afanye nini sasa?...what is his way forward, ambayo itazidi kumpambanua na wengine ndani ya CCM?
Nasubiri mchango wako.
Nape alikuwa anapigana vita asiyoijua.
Nani kawaambia Nape anaondolewa? Muwe makini na mijadala yenu, msirukie katikati bila kupima na kudadavua uhalisia wake. Kila mtu amekomalia habari ambayo siyo!
kwani wamesha maliza kumtumia...
kaka upo huru sana, tunahitaji watu wazima kama weweMimi sioni tatizo lolote la CCM kama chama cha siasa. CCM inajua fika inachokitaka na inajua kucheza karata zake vizuri inafanya siasa. Napa nae kama mwanasiasa alicheza karata zake vizuri akafika hapo alipo leo na kuwaacha mbali wapinzani wake waliomfanyia mtima nyongo kule UVCCM. Hakuna ubaya katika siasa unapopata nafasi ya kumuangusha au kujaribu kumuangusha mtu ili wewe upande ngazi na upate madaraka na hakuna kujipendekeza kwa mtu mwenye nguvu au madaraka ili nawe upate madaraka au uendelee kuwa kwenye madaraka. CCM kama chama kilichokomaa kimeona na kutambua hatari ya ya kile walichotaka kukifanya. Angalau kwa kusema tu walikuwa mameyakaribia matamanio na watanzania wengi wenye imani kuwa CCM na uongozi uliopo utawaletea maendeleo na pia kilikuwa kimegusa matamanio ya wengi wasioipenda CCM kuwa iko siku CCM hii kubwa itasambaratika angalau safari ya kushika madaraka ingekuwa imefanywa nyepesi kidogo. Katika hili utatambua kumbe asilimia kubwa ya watanzania wapo wakisubiri wengine watende wao washabikie matokeo yake. Ukweli hakukuwa na haja kwa wale mashabiki wa CCM kuisubiri NEC au CC iwafukuze hao wanaowaharibia chama. Kilichohitajika ni wao kusema hapana, watuwataki watu wa namna hii ambao sio tu wamekipotezea nuru na umaarufu chama bali pia wametuwekeza katika lindi kubwa la ujinga na umasikini. Wale wasiokuwa wana CCM lakini wenye mapenzi na nchi yao iliwapasa kusema tu tumjue kwa hakika aliyetuletea madudu ya RICHMOND na DOWANS kisha wamuulize rais iweje Bunge letu lipitishe muswada wa katiba wewe ukubali na jioni yake uhutubie na kulisifia kwelikweli lakini likifanya uchunguzi na kusema fulani ana harufu ya wizi na matumizi mabaya ya madaraka wewe ubaki kuendelea kusema unatafuta ushahidi? Watanzania wangeingia barabarani kwa ujumla wao na kusema huyu rais Muongo ajiuzulu, kwani kuna siku alituambia hata hitaji ushahidi wa kimahakama kumuwajibisha mtu, tuhuma tu pekee zitatosha sasa leo iweje ageuke?
Usichanganye habari hapa wewe mtetee Nape kama Nape usisingizie wapenzi wa Chadema, nyie na kina Rejao, FF & co. ndio mliomponza Nape kwa kumdanganya mfalme kavaa nguo kumbe yuko uchi, you didn't tell him the truth and still yet mnasema eti tutegemee chochote kipya, for your information huo ndio mwisho wake kwenye chama kama ulikuwa na mawazo kuwa he will come back sahau. Tatizo lenu mnajifanya mnaijua CCM kuliko wengine kuna watu tupo CCM tangu enzi ya TANU tunapoisema CCM negatively si kwamba hatuipendi tunataka ijirekebishe.Kwa wenye negativity dhidi ya Nape pasipo kujali UKWELI [REALITY] ya mwenendo mzima wa Matendo ya CCM dhidi ya TAIFA hakika subilieni TUTAWATAFUTA KUWAKUMBUSHA MANENO YENU HUMU NDANI, ILI MKANE MLICHOONGEA MSISAHAU MANENO YA MTOTO WA BABA WA TAIFA KUWA RACHEL NINI?
Mheshimiwa Mwenyekiti sina tatizo na kaka Yangu Lowasa lakini ulipomuinua Mkono Uko Monduli site [Wananchi] wakasema HIKI NI NINI?
Mheshmiwa Mwenyekiti nampenda Ndugu yangu Chenge wanamuita Mzee wa Vijisenti hilo Mimi Sina Hakika Nalo ulipomuinua Mkono huko Maswa site [Wananchi] wakasema HIKI NDIO NINI?
Mheshimiwa Mwenyekiti anakotembele Rostam Mimi Nisifiki na Naye afiki Mimi nilipo, ulipomuinua Mkono uko IGUNGA site [Wananchi ] wakauliza HIKi NINI?
Sasa nyie mnaoshabikia PUMBA [Kisa Wanachadema] mnatupa shaka sie tusio wananchama wa chama chochote kweli nyie ni wapenzi wa Nchi.
Tunawasubilia manake kwa wanaojua michezo ya CCM tegemeeni Chochote Kipya wakati wowote.Time will tell.
Nape, kwani kauli zako kwa wapinzani wako zinatia moyo. Nani kakuambia unahitajika humu? Madudu yako yanatosha tu kujadiliwa humu na huna ulazima wa kuingia humu, Fb panatosha. Ukitaka uheshimiwe uwe unaongea kwa busara na sio kupakana kauli chafu.
Ni kweli kuwa CCM wamekuchoka kiaina. Na wanakujua kuwa wewe na kundi lako ni wasaliti. Wanachofanya ni kukutumia kama nguo ya ndani na itafika siku watakumwaga. Tofauti yako wewe na uwt ni kuwa wewe unatumika hadharani na hadharani utatupwa. Kwa misingi hiyo usitake tukuonee huruma ilhali huna huruma
ndugu Nape alitaka kufanya press conference na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC lakini alizuiwa na wakubwa wa CHAMA kuwa hakuna haja hali iliyopelekea Nape kususia kikao cha viongozi wa Chama na habari zaidi nilizopata ni kwamba amerejea Dar mapema zaidi hata kabla ya wenzie kutawanyika.
Umenikumbusha, kuna rafiki yangu alivamiwa na kibaka maeneo ya Gongo la Mboto wakati akitoka bar usiku, kibaka wenyewe ni hawa wanaoshindia mihogo kwa maji, alichokifanya ni kumpa kabari la nguvu kibaka hadi kibaka akaanza kupiga kelele kuomba msaada kwa wapitanjia.The hunter has become the hunted!!!!!