Nape na ombi lake kwa vijana........... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape na ombi lake kwa vijana...........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Sep 15, 2011.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamvi hili mara kwa mara limekuwa likitoa ushari wa dhati kabisa kwa Nape pamoja na kuwa yeye pia ni mdau humu nimeshindwa kuelewa ni kwamba haelewi au amekuwa sikio la kufa......... Nimechukua baadhi ya maneno au majibu ya Wilson Mukama (Katibu Mkuu wa CCM) dhidi ya Nape ili hoja hii ikae sawa (Source Mwanahalisi)


  1. Taarifa zinamnukuu Mukama akimueleza Nape " ............nimeambiwa umekwenda Igunga, wakati Kamati Kuu ya Chama imekuzuia kwenda huko. Unataka nini? Mbona unataka kutuharibia uchaguzi? alifoka Mukama


  2. Mukama kwa hasira alihoji, "Nape kwa nini umekwenda Igunga? Alipojaribu kujitetea kwamba alikwenda huko kuhani, Mukama alisema, "Nani amekutuma? Nani amekuruhusu? Kijana tafadhali usituharibie uchaguzi"


  3. Mukama akamuuliza Nape, "Nimeambiwa unajiandaa kwenda Igunga, mbona wewe kijana husikii?


  Nyongeza ya Hayo; Baada ya ufunguzi wa Kampeni Mukama akiwa mwenye furaha, aliwaambia baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho, "Tumefanikiwa sana katika mkutano wetu huu, kuna watu wengine bwana hawana Discipline (nidhamu), hawana adabu wanajiona wanaweza kuvuta watu kwenye mkutano. Mwiguru Nchemba anafanya kazi nzuri sana. Ameratibu mkutano huu vizuri Kampeni zimekwenda vema. Ni kijana mwenye busara sana yule"

  Kwa kauli hii ya Mukama kuna maswali ya kujiuliza; Mosi ni watu gani hao wasio na nidhamu na adabu? Pili ni nani anayefanya kazi mbaya? Tatu ni kijana yupi asiye na busara kama za Nchemba?

  Mwandishi (Alfred Lucas) anasema, alipowasiliana na Nape ili kuthibitsha haya au kukanusha majibu ya Nape yakawa haya "Alfred, mimi sina la kusema juu ya hilo, Nape akauliza, Jamani mimi kijana mwenzenu nimewakosea nini? Niambieni basi"

  Binafsi sina shaka hata kidogo juu ya maneno ya Wilson Mukama kwa Nape hayo yanathibitika si tu kwa Alfred Lucas bali wenye uwezo wa kufahamu tunafahamu haya kuwa ni ya kweli labda mazungumzo ya Nape na Alfred ndiyo ninayoweza kusema kuwa siwezi kuyanenea ila vile vile Alfred hana sababu yeyote ya kudanganya juu ya majibu aliyoyatoa Nape.

  Swali langu wanajamvi; is this not embarassement? Hivi ni mpaka Malaika ashuke ndo Nape atapata uelewa au? What else do he want........ Ni kweli kwamba anahitaji vijana wamwambie alichowakosea au? (Mtu kama Mwita si lazma ajibu hili)
   
 2. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Siasa za chuki na ubaguzi zinawamaliza wenyewe ccm,adui muombee njaa
   
 3. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Niliisoma hiyo habari na mimi nimeshangaa! Nape kujidai kote JF kuwa yuko Igunga. Kumbe ni kujipendekeza na wala hakutumwa, bora yule baunsa angempiga pale baa, akome majitambo yake.
   
 4. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Bahati nzuri nimetokea kuwafahamu Mukama na Nape kwa muda mrefu. Mukama kupitia sehemu ambazo amefanya kazi hadi kufikia kustaafu, na Nape kupitia family connections toka Mzee Nnauye akiwa hai.


  Wote wawili ni vichwa ngumu.


  Nisiishie hapo lakini. Kwa upande wa Mukama, siwezi kujua ni nini kinachomsukuma, kwani inaaminika kuwa ni Mukama ndiye aliyepenyeza hilo wazo la Nape - Katibu Mwenezi na Itikadi (CCM - Taifa), kuzuiwa kwenda Igunga kufanya sehemu za kazi zake (Uenezi na Itikadi).

  Lakini pia ni Mukama huyo huyo ndiye anayeidhinisha masurufu ya safari, mikutano na gharama zingine za uendeshaji wa shughuli za Makao Mkuu, ambapo Nape ni mmojawapo pia. Ni vigumu kujua nini kinaendelea kwa mgongo wa Mukama.

  Tukirudi kwa Nape, naye ana yake lukuki. Kutumia ujana kama kigezo cha 'kulindwa' kwa uozo wa utendaji wake, ndiyo hayo yaliyotufanya tukapewa JK, Kijana mwenzetu, Chaguo la Mungu. Kama ubovu ni ubovu tu. Nilisema hapa JF kuwa Nape kwenda Igunga si bure, aidha atakuwa amekaidi maagizo ya Kamati Kuu au atakuwa ametumwa.

  Hata hivyo, kwa utetezi wa Nape, ninasimama naye kuwa kujiuzulu au kuachia ngazi hilo lisiwepo kabisa. Komaa nao hapo hapo Nape.

  Nape hakuomba hiyo kazi, hakuwa na ndoto ya kupewa hiyo kazi, na wala hakupigiwa ndogondogo kuipata hiyo kazi. Walimtoa UVCCM, kwa kejeli na mateke wakamtupa Masasi kumtuliza. Wao wenyewe kwa kujua wanachotaka kufanya na jinsi gani wanaweza kumtumia, wakamfuata Masasi na kumpa kuwa Katibu Mwenezi na Itikadi (CCM-T). Hakuulizwa kama anataka au la. Alipewa. Ndivyo hivyo alivyopewa Mukama pia.

  Sasa kama wanaona 'kazi' waliyompa Nape kamaliza, basi ni wao wamtoe. Kama hawa wawili wana mgongano wa utekelezaji, basi Mwenyekiti wao na mshauri wake mkuu kichama Msekwa, ndiyo waamue zipi pumba na zipi mchele. Na wote tunafahamu 'maamuzi' ya Mwenyekiti, ni kama yale ya Ngeleja, Luhanjo na Jairo. Pima upepo, mtakesha mkisubiri.
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Duh Nape kama ni kweli atakuwa anajisikia Baja akiendelea na magamba watamvua hadi nguo aone aibu kutembea barabarani kama madiwani wale wa Arusha CCM sio uijuavyo si wale wa ndani au nje
   
 6. NEW TANZANIA

  NEW TANZANIA Senior Member

  #6
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  me i like is brainstorm in chama cha majuha wacha wamalizane nguvu
   
 7. m

  mtoto wa mama Senior Member

  #7
  Sep 15, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kumbe gazeti lenyewe la chadema mwanahalisi..
   
 8. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Duuuuuuuuu! sikujua kumbe ndio hv?
  sasa anangoja nini kukamilisha usajili wa ccj asepe tuuuuuuuu
   
 9. String Theorist

  String Theorist JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  INAONEKA NAPE AMESAINISHWA MIKATABA NA CCM AMBAYO HUENDA NDIO INAYOMFANYA ASIJIUZURU. Sii ujua tena "we are not afraid of death, but no one is hurry to die"
   
 10. H

  Honey K JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu salaam,

  Nilikuwa kwenye kampeni ndo naingia Singida sasa.. Nimekuwa nikisoma maneno mengi sana juu ya Nape humu jf mengi kwakweli ni ya kunitukana na kunikejeli kiasi kwamba nadhani karibu ntaacha kuingia humu maana mwanzoni nilizoea ukiingia humu unakuta watu wanaongea vitu seriuos tena kwa ushahidi mkubwa sio kuokoteleza vijigazeti vya barabarani na kudai ndio ushahidi!

  Kinachonipa tabu mara nyingi kujadili hoja flani humu jf kwasasa licha ya matusi tena yasiyo hata na tija, lakini pia baada ya hoja kufafanuliwa pengine kinyume na mods wanavyotaka utaona hiyo thread inaondolewa....

  Haya ya Mwanahalisi ni uongo wa ,chana peupe, hata watu wanaosoma hiyo stori na kujua nilikuwa wapi siku inayotajwa ya tarehe tisa ni aibu kubwa... Kama nasi humu tunaweza kuamini,basi tunaipeleka pabaya jf yetu
   
 11. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #11
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape kwanza nakupongeza na kukutia moyo kuwa kazi unaiweza. Songa mbele.
  Nakushauri wala usiache kupita humu, we pita tu ila mengi ni ya kupuuza puuza

  Najua matusi ya jf kweli kama mwanadamu yanavunja moyo. Lakini jipe moyo wako watu makini wanakuunga mkono.
  Watu makini hutowaona wakijibu kila thread au wakitukana.

  Hapa jf sura za cdm ni zilezile, hata Zitto mwenyewe naona kapunguza kuingia jf.

  Mods nao wameifanya jf si huru tena. Lakini pambana so long as uko kwenye haki.
  Watu makini ndo wapiga kura na si wapiga porojo/matusi hapa jf
   
 12. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nape, Nape, Nape, wewe ni mwiba mbaya kwa upinzani ndio wanakusema sana, songa mbele kaka wewe ni lulu na mataji wa ccm, waliokuchagua wanajua hilo, wazee wanajua, vijana wanajua, akina mama wanajua ,watanzania wanajua.

  Kama wasivyokusema sasa watasema nini, wapinzani kwa sasa kwa kweli hali yao mbaya. Endelea na kazi zako, mwanahalisi ni mali ya cdm na pia kunamkataba na wafisadi wale 3. nakutakia kazi njema kaka.

  Mimi binafsi nakuamini sana.
   
 13. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mmmmm kweli unayoyasema NAPE? Kama ni kweli hongera zako lakini kama ni Uongo kazi unayo na naomba ufaham ukweli siku zote huwa haufichiki siku zijazo tutaja pata ukweli na itakuwa aibu
   
 14. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  <br />


  Ndugu,

  Kwanza hongera kwa kujitokeza kujibu angalau maswali yaliyokuwa yamejadiliwa hapa.

  Pili, unatambua hii forum is for the GT.

  Unapokuja na majibu mepesi namna hiyo, unazidi kutuchanganya. Mwandishi wa gazeti amesema amekuhoji, hilo nalo ni uongo wa mchana? Kuna hoja ya kukatazwa kwenda Igunga, hiyo unasemaje?

  Unaweza kusema kauli tajwa za Mukama ni uongo. Lakini hoja za msingi za wewe kukaidi tamko lililokuzuia kwenda Igunga na mahojiano na mwandishi ulitakiwa kuziweka wazi ili tuutenganishe uongo na ukweli.
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Nape nikupongeze kwa roho ngumu, ila nikutahadharishe tena si kila kitu kinataktaka roho ngumu. Kwanza umejibu hoja kiujumla sana pili kwa wanaoijua ccm wanajua ilivyokufanyia kwenye jengo la uvccm,wewe ni itikadi na uenezi kwa nini uende igunga kwenye msiba?

  Na si kwenye kampeni? Nani anaeneza itikadi ya chama kwa wana igunga?au kuna kaimu wako?kumbuka ccm wanataka panga lenye makali tu,wakishalipiga kwenye mawe wanalitupa. Sasa hivi nchemba wanamwamini kuliko wewe,ila tunaowafaham tunajua. Huyu Mwigulu na kuropoka kwake tunamhesabia siku.

  Na wewe kama utasimama kwenye ukwel mungu atakaa upande wako ila kama unasema uongo ili uonewe huruma nakuambia muda si mrefu utaumbuka.
   
 16. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  ccm wanamalizana wenyewe kwa wenyewe.
   
 17. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ndugu nape jibu hizo hoja na acha hasira, anza na gazeti je hukufanya mahojiano? Kwa nini siku ya ufunguzi hukuwepo? Na kwanini sasa hauko Igunga?
   
 18. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape binafsi sina sababu yeyote ya kutokukupongeza kwa kujitokeza na kujaribu kujibu thread hii japo naamini kama cheo chako kilivyo unafahamu hoja hujibiwa kwa hoja na kujibu hoja kwa ujumla hakumaanishi kitu kingine zaidi ya kukwepa kujibu hoja hiyo.

  Hivyo niungane na baadhi ya waJF kwamba umejibu hoja kwa ujumla na kwa kweli hujaeleweka vyema. Lakini vile vile kama kuna wanaokutusi humu nikupe pole na kama alivyosema Mbunge mmoja mwanasiasa shurti uwe na ngozi ngumu kama ya Mamba na vile vile kutokuingia humu hakutasaidia lolote manake "running from the problem isnt the way of solving it."

  Unasema habati ni za uongo ila unakiri kuwa umetokea Singida na mwandishi alisema kuwa baada ya songombingo kati yako na yule baunsa uliondoka na kuelekea Singida hivyo zimwi la Afred bado linakuandama.

  Lakini mwisho unaonekana kutumia defence of Alibi kwamba tarehe tajwa hukuwepo eeo husika na vile vile kwa kumwamini Alfred Lucas tutakuwa tunalipeleka Taifa bapaya. Tatizo linabaki pale pale tutaache kumwamini Alfred tumwamini nani huku majibu yako hayaridhishi. Tafakari kwa kina. Nikutakie heri
   
 19. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  NAPE NAUYE, First you are not a great thinker. Why?. Huwezi kujibu hoja ngumu kwa majibu mepesi namna hii. Acha kulaumu, jibu hoja, kwa nini ulienda igunga wakati ulipigwa ban? Kwa gharama ya nani ulienda igunga? Nani alikutuma huko?

  Huu ni unafiki, kama kweli wewe huna hila ndani yako nakushauri hama ccm haraka sana. Usianze kusema gazeti wala kuwa wote tuliomo humu ni chadema. When you present a substance in your argument we will agree with you despite you are magamba or not.

  Najua kwa uwezo unamzidi mchembe, lakini kama alivyosema member mmoja hapa kuwa ccm wakisha kukutumia kama panga kali na makali yakaisha, the hide or throw you in the dust bin.

  Achana na mambo ya ccm ya kukanusha hata kama kitu ni kweli. KWAO KITU CHEUPE KINAWEZA KUITWA CHEUSI NA KUKUBALIKA.
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nape, kwani kauli zako kwa wapinzani wako zinatia moyo. Nani kakuambia unahitajika humu? Madudu yako yanatosha tu kujadiliwa humu na huna ulazima wa kuingia humu, Fb panatosha. Ukitaka uheshimiwe uwe unaongea kwa busara na sio kupakana kauli chafu.

  Ni kweli kuwa CCM wamekuchoka kiaina. Na wanakujua kuwa wewe na kundi lako ni wasaliti. Wanachofanya ni kukutumia kama nguo ya ndani na itafika siku watakumwaga. Tofauti yako wewe na uwt ni kuwa wewe unatumika hadharani na hadharani utatupwa. Kwa misingi hiyo usitake tukuonee huruma ilhali huna huruma
   
Loading...