Akiongea na MakutanoShow sasa hivi ameongelea kuhusu mgombea urais kupitia CCM baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mbio za urais.
Amesema hata kama mtu akijaza wapambe wake CC na NEC siyo kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa urahisi.
Alitoa mfano mara tatu kuhusu Lowassa kwamba siyo msafi na hata Nyerere alisema hivyo. Alisema kwamba siyo lazima kuwepo ushahidi bali kama watu wanaongea tu na kukuhisi inatosha kuthibitisha kwamba wewe siyo msafi.
Katibu wa itikadi na Uenezi anayeeneza uchafu wa chama chake na wanachama bila kushurutisha hatua za kinidhamu kuchukuliwa.ningekuwa yeye ningejiuzulu nafasi hiyo kwa kuwa inaonekana chama hakiko tayari kujisafisha ili aeneze mambo masafi ya chama!
Akiongea na MakutanoShow sasa hivi ameongelea kuhusu mgombea urais kupitia CCM baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusishwa na mbio za urais.
Amesema hata kama mtu akijaza wapambe wake CC na NEC siyo kigezo cha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa urahisi.
Alitoa mfano mara tatu kuhusu Lowassa kwamba siyo msafi na hata Nyerere alisema hivyo. Alisema kwamba siyo lazima kuwepo ushahidi bali kama watu wanaongea tu na kukuhisi inatosha kuthibitisha kwamba wewe siyo msafi.
Nape amekosa uhalali kwenda kwenye vyombo vya habari na kuongelea rushwa na matumizi mengine mabaya ya fedha ndani ya ccm. Anazidi kuanika uozo ndani ya chama chake kuwa hakiko makini kuwashughulikia mafisadi kuendelea kujenga mitandao ya urais ndani ya chama.
Cha kujiuliza, kama Nape aligundua kuwa kuna hako ka mchezo ka kupanga wajumbe wa cc na halmashauri kuu yeye kwa nafasi yake na wengine wachukia maovu ndani ya ccm walifanya nini kabla ya yeye kuyasema hayo kupitia makutano show?!
Kama alikaa kimya na hakuweza kusema kitu bora angeendelea kukaa kimya kuliko kuanika udhaifu na upumbavu wao. Mtoto wa baba wa taifa kang'olewa kwa milioni 300 za rushwa, chama kimefanya nini baada ya kugundua kuwa Makongoro kachezewa rafu?! Usanii mtupu.
Hadithi za vilinge vya kahawa; iweje Nape akose uhalali wa kuongelea rushwa? Nape akiwa kama mmoja wa watendaji wa chama ana haki zote za kuongelea maovu; si kweli kama wajumbe wa CC ni wala rushwa; wapo wachache ambao wanajulikana wazi kwa matendo yao ya rushwa; hebu tupe uthibitisho wa hizo mil.300 zilivyotumika kuomng`oa Makongoro.
Chama
Gongo la mboto DSM
Hahahaha yaani chama unathubutu kuziba shimo la panya kwa mkate? ccm na rushwa ni sawa na samaki na maji, bila rushwa ccm inakufa sekunde mbili tu.
Nape anakiri kwamba lowasa amejitahidi kuweka watu wake cc na nec halafu wewe unajaribu kukanusha kauli yake? umepima uzito wa kauli ya nape kwamba hata kama lowasa amejaza watu wake cc na nec hiyo haimpi tiketi ya kuwa mgombea!? hahahaha,,, twende dodoma basi tukampongeze mama nonino ameshinda uenyekiti uwt sijui katoa milioni ngapi raundi hii nakumbuka last time alimwaga mpunga hadi mama kahama akalia.
Dr. AshaRose MingiruNani ni msafi huko NyiNyiEMu anyway? Wote mmejaa matope matupu!