Hata ikiundwa tume kuchunguza hiyo kitu, unafikilia nini kitatokea??? Uchunguzi unaweza kufanyiwa na kukuta Kuna ubadhirifu mkubwa na Chama dola kikashindwa kuitoa ripoti hadharani kwa kuhofia itawaghalimu sana ktk uchaguzi.Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Mbunge wa jimbo LA Mtama Mh Nape Moses Nnauye,ameibua mjadala mitandaoni kwa hoja yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni ya kutaka kuwepo kwa uchunguzi wa kina kuhusu hoja iliyoibuka ya kuwepo kwa deni kubwa LA taifa.
Mh Nape anasema "kufanyike uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa matumizi ya fedha za mikopo hiyo iliyokopwa na Nchi na kulinganisha na kiasi cha gharama ya miradi ya maendeleo iliyofanyika."
Anasema "kipindi cha awamu ya tano kumekuwepo na usiri mkubwa katika ukopaji wa fedha hizo na ndicho kipindi kilichokopa pesa nyingi ukilinganisha na awamu zote japo ni awamu iliyokaa muda mfupi madarakani kuliko awamu zote."
Akaenda mbali zaidi kwa kutolea mfano awamu ya sita chini Rais Mama Samia, kama mfano bora wa uongozi wa uwazi kwa kuweka bayana matumizi ya mkopo wa fedha za IMF 1.3Trilions namna zilivyoainishwa upatikanaji wake na matumizi yake.
Mm binafsi kama Chakwale naona Nape ana hoja ya msingi ya kutaka kuwepo uwazi na ukweli wa matumizi ya fedha zote za serikali,kwa sababu matumizi yoyote ya hovyo mzigo wote anaubeba or tunaubeba sisi Wananchi wa kipato cha chini.
Unaweza kuona serikali ya awamu ya sita inavyopambana katika kuongeza vyanzo vya vipya vya mapato ikiwemo Kuanzisha tozo Mpya za Miamala ili walau kuongeza wigo wa mapato jambo ambalo limepigiwa kelele na wananchi kuwa linawaongezea mzigo maisha.
Sasa kama Wananchi tumejaribu kupaza sauti zetu kuhusu tozo sababu zimetugusa moja kwa moja nilitarajia hata hili LA Mh Nape lingeungwa mkono kama LA tozo sababu adhari zake ni zilezile kwa mwananchi wa hali ya chini.
Badala yake imekuwa kinyume kwa Mh Nape kuonekana kama ni MTU mwenye Chuki,kisasi or hasira na utawala uliopita wa awamu ya tano,kwa kuwa tu eti alienguliwa Uwaziri wa Habari Sanaa na Michezo kwa kile alichokuwa akikiamini juu ya sakata zima LA aliekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar.
Ninachokiona watu hawaangalii hoja iliyotolewa na kuijadili Bali wanachoangalia ni mtoa hoja ni nani,so inaonekana watu hawana shida na hoja ila wana shida na mtoa hoja kitu ambacho katika karne hii ni matumizi mabovu ya rasilimali kichwa.
Kumchukia MTU kwa sababu zako binafsi hakuondoi Uimara,umaana,hekima,busara wala mantiki ya kile alichokisema.kwanza unatakiwa utafakari uchuje then uunge mkono or kukosoa kwa hoja si kwa kutumia chuki zako binafsi.
Kama taifa lililo serious na Maendeleo endelevu ya Nchi yetu tulipaswa kumuunga mkono Nape kwa hoja yake aliyotoa ili kujiridhisha.Sababu haiwezekani watu wengine wabebeshwe mzigo kwa ujinga,tamaa na chuki za watu wengine tutakuwa tunacheza "Mark time" tu bila kusonga mbele.
Kwa Nchi za wenzetu bei tu mkate ikipanda bei pasipokuwapo sababu zinazoeleweka hapakaliki lazima watu wawajibike kwa hilo sembuse sisi ambao Trillions of money hazieleweki zinatumikaje halafu tupotupo tu.
Nilitarajia vyama vyetu vya upinzani vingekuwa vimepata agenda ya kuvifanya vitengeneze uwepo wao,navyo vimelala usingizi wa pono vina ajenda moja tu ya katiba Mpya ambayo imefinyiwa kwapani hawana mbadala tena.Kama huwezi kuwasemea Wananchi katika haya yanayowahusu kama ya Tozo,kupanda kwa bei ya mbolea na bidhaa zingine,mazingira bora ya machinga,ukosefu wa ajira kwa vijana nk nk ni mwananchi gani atakusapoti suala lako LA katiba ambalo anajua ni LA tamaa zako tu za kutaka kukuingiza madarakani ila sio kumtetea yeye??
Alamsiki
Sisi wtz ni watu wa ajabu sana. Kazi Yetu kulalamika tu hatuwezi kuiwajibisha Serikali wakati sisi ndio wenye nchi
Kitu kibubwa na cha mingi ili kukomesha haya mambo ya kijinga ni kupata katiba Mya itakayo wawajibisha viongozi na kutupilia mbali Sheria ya kijinga ya kutokushitakiwa kwamakosa watakayofanya wakati wakiwa madalakani kwani hiyo Sheria ndio inayotufanya tuingizwe chaka