Nape ana hoja ya msingi ila shida ni yeye

Chakwale

JF-Expert Member
May 17, 2015
1,068
1,542
Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Mbunge wa jimbo LA Mtama Mh Nape Moses Nnauye,ameibua mjadala mitandaoni kwa hoja yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni ya kutaka kuwepo kwa uchunguzi wa kina kuhusu hoja iliyoibuka ya kuwepo kwa deni kubwa LA taifa.

Mh Nape anasema "kufanyike uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa matumizi ya fedha za mikopo hiyo iliyokopwa na Nchi na kulinganisha na kiasi cha gharama ya miradi ya maendeleo iliyofanyika."

Anasema "kipindi cha awamu ya tano kumekuwepo na usiri mkubwa katika ukopaji wa fedha hizo na ndicho kipindi kilichokopa pesa nyingi ukilinganisha na awamu zote japo ni awamu iliyokaa muda mfupi madarakani kuliko awamu zote."

Akaenda mbali zaidi kwa kutolea mfano awamu ya sita chini Rais Mama Samia, kama mfano bora wa uongozi wa uwazi kwa kuweka bayana matumizi ya mkopo wa fedha za IMF 1.3Trilions namna zilivyoainishwa upatikanaji wake na matumizi yake.

Mm binafsi kama Chakwale naona Nape ana hoja ya msingi ya kutaka kuwepo uwazi na ukweli wa matumizi ya fedha zote za serikali,kwa sababu matumizi yoyote ya hovyo mzigo wote anaubeba or tunaubeba sisi Wananchi wa kipato cha chini.

Unaweza kuona serikali ya awamu ya sita inavyopambana katika kuongeza vyanzo vya vipya vya mapato ikiwemo Kuanzisha tozo Mpya za Miamala ili walau kuongeza wigo wa mapato jambo ambalo limepigiwa kelele na wananchi kuwa linawaongezea mzigo maisha.

Sasa kama Wananchi tumejaribu kupaza sauti zetu kuhusu tozo sababu zimetugusa moja kwa moja nilitarajia hata hili LA Mh Nape lingeungwa mkono kama LA tozo sababu adhari zake ni zilezile kwa mwananchi wa hali ya chini.

Badala yake imekuwa kinyume kwa Mh Nape kuonekana kama ni MTU mwenye Chuki,kisasi or hasira na utawala uliopita wa awamu ya tano,kwa kuwa tu eti alienguliwa Uwaziri wa Habari Sanaa na Michezo kwa kile alichokuwa akikiamini juu ya sakata zima LA aliekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar.

Ninachokiona watu hawaangalii hoja iliyotolewa na kuijadili Bali wanachoangalia ni mtoa hoja ni nani,so inaonekana watu hawana shida na hoja ila wana shida na mtoa hoja kitu ambacho katika karne hii ni matumizi mabovu ya rasilimali kichwa.

Kumchukia MTU kwa sababu zako binafsi hakuondoi Uimara,umaana,hekima,busara wala mantiki ya kile alichokisema.kwanza unatakiwa utafakari uchuje then uunge mkono or kukosoa kwa hoja si kwa kutumia chuki zako binafsi.

Kama taifa lililo serious na Maendeleo endelevu ya Nchi yetu tulipaswa kumuunga mkono Nape kwa hoja yake aliyotoa ili kujiridhisha.Sababu haiwezekani watu wengine wabebeshwe mzigo kwa ujinga,tamaa na chuki za watu wengine tutakuwa tunacheza "Mark time" tu bila kusonga mbele.

Kwa Nchi za wenzetu bei tu mkate ikipanda bei pasipokuwapo sababu zinazoeleweka hapakaliki lazima watu wawajibike kwa hilo sembuse sisi ambao Trillions of money hazieleweki zinatumikaje halafu tupotupo tu.

Nilitarajia vyama vyetu vya upinzani vingekuwa vimepata agenda ya kuvifanya vitengeneze uwepo wao,navyo vimelala usingizi wa pono vina ajenda moja tu ya katiba Mpya ambayo imefinyiwa kwapani hawana mbadala tena.Kama huwezi kuwasemea Wananchi katika haya yanayowahusu kama ya Tozo,kupanda kwa bei ya mbolea na bidhaa zingine,mazingira bora ya machinga,ukosefu wa ajira kwa vijana nk nk ni mwananchi gani atakusapoti suala lako LA katiba ambalo anajua ni LA tamaa zako tu za kutaka kukuingiza madarakani ila sio kumtetea yeye??

Alamsiki
 
Kwanza ikumbukwe kuwa, Nape na Genge lake waliwahi kumtukana sana Mzalendo wetu JPM, yeye(Nape) alipoona mambo yote yapo hadharani, aliamua kwenda kwa JPM kuomba msamaha.

Hata kipindi cha Bunge kilichopita, Nape huyu huyu alionesha dalili za moja kwa moja za kupinga kabisa Legacy ya JPM, alipopigwa mashambulizi makali mitandaoni, aliamua kuchuchumaa.

Kwa hiyo, leo hii Nape atatuambia nini ili tumwamini?
Zaidi sana hapo yeye anachokitafuta ni kupata uteuzi tu na wala si vinginevyo.

Ili ujue kichwa chake ni kibovu kabisa ni pale anaposhindwa hata kujua kuwa, Serikali ya awamu ya tano ya JPM ndiyo iluyofanya maajabu ya kufanya mambo makubwa kabisa ambayo wengine wote waliopita walishindwa kabisa ingawa walikaa madarakani kwa miaka 10.

Nape asicheze na akili za Watanzania wa leo. Kuna siku atakuja kuumbuka mchana kweupe.
 
Siasa zetu zimekuwa za hovyo sana!

Siasa imekuwa ndo uwanja pekee ambao kila mtu anaweza kuingia na kutoboa kwa sasa!

Wameingia kwenye siasa matapeli,waganga wa kienyeji ,machangudoa na vi.laza wengi sana! Hivyo siasa za hoja hazina nafasi tena.

Na pia wananchi wengi wa Nchi yetu kutokana na elimu duni na maarifa madogo hawajui mantiki ni nini na pumba ni nini?!

Angalia hata kwenye Bunge letu akina Musukuma, Lusinde ( Kibajaji) wana nguvu na ushawishi na wanaeleweka kwa Wananchi kuliko hata Maprofesa walioko Bungeni!
 
Mkuu naona na ww unapita mulemule kwenye kumuattack MTU personally badala ya kuattack hoja yake.

Niambie hoja yake ina shida gani?wapi pana shida kwenye hoja yake?wapi amepatia pia?kusema sijui alionyesha kupinga Legacy ya JPM hiyo mbona haihusiani na hoja aliyoitoa?hata kama ni kweli alionyesha kupinga shida iko wapi si alitumia Uhuru wake binafsi wa kikatiba kutoa maoni yake?

So unataka kuniaminisha kuwa MTU akiwa kinyume na mawazo or mtazamo aliokuwa nao JPM ni kosa ambalo hastahili kusikilizwa hata anasema nini?

Kama ni hivyo ni akina nani basi wenye haki na hati miliki ya kusema na kusikilizwa bila hata ya kuchuja kuwa wamesema nini?
 
Mleta uzi umekuja na hoja ya Nape, lakini unarushia mpira wapinzani. Kwa taarifa yako hoja za hivyo wapinzani wanazo muda wote, ni lini umemuona huyo Nape akiwaunga mkono? Au kazi ya wapinzani wao ni kusubiri hoja ya mwanaccm na kuiunga mkono? Sio mara moja au mbili wapinzani walihoji mtindo wa Magufuli kufanya mambo bila uwazi, na watu kama akina Nape ndio walikuwa mstari wa mbele kusema wapinzani wanapinga kila kitu.

Mwambie Nape apambane na hoja yake, maana alikuwa anachekelea wapinzani kuporwa haki yao ya kufanya siasa na kuhoji. Hao wananchi unaotaka wawaunge mkono wapinzani, unataka wawaunge mkono mara 2? Lakini kwenye chaguzi si ndio huko akina Nape kwa kushirikiana na vyombo vya dola na tume ya uchaguzi hupita bila kupingwa, au kuingiza mabox ya kura?
 
Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Mbunge wa jimbo LA Mtama Mh Nape Moses Nnauye,ameibua mjadala mitandaoni kwa hoja yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni ya kutaka kuwepo kwa uchunguzi wa kina kuhusu hoja iliyoibuka ya kuwepo kwa deni kubwa LA taifa.
Ukweli ni kwamba labda tunasahau tu Ila huyu Nape wakati akiwa Waziri alituletea Sheria za kishenzi sana kwenye sekta ya Habari na ndio alikuwa kinara wa kuhakikisha bunge live inaondolewa.

Nape aliona kama ndio wameirithi Tanzania na siwezi kumtofautisha Nape na Polepole au Bashite, sema era yao ipo tofauti Ila alimtukana San mzee Lowassa akiwa na marehemu Samwel Sitta. Huyu nae ni mwehu mwingine akisaidiana na Makamba Jr.
 
kuna msemo wa wazungu unasema "Marehemu hawezi kujitetea" kila la kusemwa litasemwa ila kamwe hatutaweza kusikia upande wa mlalamikiwa ukitoa ushaidi
Ni kweli Mkuu kabisa usemacho kuwa Marehemu hawezi kujitetea,ila Mahakamani wana msemo wao unasema "ili iwe fundisho kwa wengine"..

Yaani Mahakama inakuadhibu ww kwa kukukuta na hatia Fulani,na inakuadhibu ww " ili iwe fundisho kwa wengine"..maana yake ni kwamba kwa kosa ulilolifanya unapewa adhabu ili wengine wajifunze kuwa wakifanya kosa kama lako na wao pia wataadhibiwa kama ambavyo ww umeadhibiwa.

Hii inajenga nidhamu,ustaarabu,heshima,na watu kuishi katika maadili yanayotakikana.So kwa hili LA uchunguzi hata kama Marehem hawezi jitetea ila uchunguzi ukibaini kuna hila na udanganyifu wa aina yeyote itasaidia kwa viongozi wengine wajao kujifunza makosa yaliyofanyika hivyo kujenga taifa bora LA baadae.

Kukalia kimya hili maana yake ni kwamba tumeamua kuwa shamba LA bibi kila MTU anaamua kujifanyia anachotaka pasipo kufanywa chochote.kule China sheria za kunyonga zimesaidia kuibadili China na kufika hapo ilipo.
 
Kwanza ikumbukwe kuwa, Nape na Genge lake waliwahi kumtukana sana Mzalendo wetu JPM, yeye(Nape) alipoona mambo yote yapo hadharani, aliamua kwenda kwa JPM kuomba msamaha.
Tatizo la Nape ni njaa na alijianimisha kuwa yeye ndie mwenye CCM kisa baba yake alikuwa nae mwenye CCM, Nape huyu huyu ndie alijifanya ana uchungu na mali za Umoja wa Vijana baada ya yalipokuwa makao makuu ya Umoja wa Vijana kukwapuliwa na akina mamvi na wahindi wenzake na akasahau kuwa mamvi hakuwa peke yake, matokeo yake akawa anabweka tu na hakuna lolote alilofanya nae ndio akaanza tabia za wizi wa mali za CCM na bwana Ndovu na yule babu wa Lushoto, huyu Nape ni genge la wahuni na wezi na hana uchungu wowote kelele zote za sasa ni kutaka cheo serikalini, ukiangalia timu yake ya mwanzoni wenzake wote ni mawaziri,Bashe,January ni yeye na mtoto wa remote ndio hawamo kwenye baraza ingawa bado mtoto wa remote ameanza kuwa na nguvu hivi sasa kutokana na nguvu za remote alizonazo hivi .
 
Ukweli ni kwamba labda tunasahau tu Ila huyu Nape wakati akiwa Waziri alituletea Sheria za kishenzi sana kwenye sekta ya Habari na ndio alikuwa kinara wa kuhakikisha bunge live inaondolewa.

Nape aliona kama ndio wameirithi Tanzania na siwezi kumtofautisha Nape na Polepole au Bashite, sema era yao ipo tofauti Ila alimtukana San mzee Lowassa akiwa na marehemu Samwel Sitta. Huyu nae ni mwehu mwingine akisaidiana na Makamba Jr.
Mkuu mtoto akinyea kiganja cha mkono hatukati tunachofanya ni kusafisha tu..Unajuaje kama hizo Sheria kandamizi kwenye sekta ya Habari na usimamizi wa kuzimwa bunge Live yeye alishurutishwa tu na Mamlaka za juu yake??

Kwani sote si mashahidi humu kuwa kuna yeyote ambae angeweza kufurukuta kusema chochote kwenye utawala uliopita wa awamu ya tano?

Pia sote ni mashahidi namna Nape alipambana kuhakikisha haki inapatikana na kutenda dhidi ya Uvamizi uliofanyika katika kituo cha kurushia matangazo cha Clouds,kilichomkuta sote si tunakifahamu?
Waswahili husema Nia njema ni tiba,na nia ovu ni sumu,huwezi kumuhukumu Nape kwa yaliyo nje ya uwezo wake.
 
Heheh, anyway wacha ninyamaze tu.
 
Basi aliyekuwa makamu wa rais ajihuzulu kupisha uchunguzi kwa wizara zilizokuwa chini ya ofisi ya makamu wa rais ili kuwa na uchunguzi ulio huru. Vile vile mawaziri wote waliokuwepo wapishe uchunguzi huru ufanyike kwenye wizara zao
 
Ni kweli Mkuu kabisa usemacho kuwa Marehemu hawezi kujitetea,ila Mahakamani wana msemo wao unasema "ili iwe fundisho kwa wengine"..

Yaani Mahakama inakuadhibu ww kwa kukukuta na hatia Fulani,na inakuadhibu ww " ili iwe fundisho kwa wengine"..maana yake ni kwamba kwa kosa
Mahakama inatoa nafasi kwa mtu kujitetea, sasa marehemu atajiteteaje ?
 
Kwanza ikumbukwe kuwa, Nape na Genge lake waliwahi kumtukana sana Mzalendo wetu JPM, yeye(Nape) alipoona mambo yote yapo hadharani, aliamua kwenda kwa JPM kuomba msamaha.

Hata kipindi cha Bunge kilichopita, Nape huyu huyu alionesha dalili za moja kwa moja za kupinga kabisa Legacy ya JPM, alipopigwa mashambulizi makali mitandaoni, aliamua kuchuchumaa.

Kwa hiyo, leo hii Nape atatuambia nini ili tumwamini?
Zaidi sana hapo yeye anachokitafuta ni kupata uteuzi tu na wala si vinginevyo.
Ili ujue kichwa chake ni kibovu kabisa ni pale anaposhindwa hata kujua kuwa, Serikali ya awamu ya tano ya JPM ndiyo iluyofanya maajabu ya kufanya mambo makubwa kabisa ambayo wengine wote waliopita walishindwa kabisa ingawa walikaa madarakani kwa miaka 10.
Nape asicheze na akili za Watanzania wa leo. Kuna siku atakuja kuumbuka mchana kweupe.
Haya usemayo yazingatiwe baada ya uchunguzi kufanyika kwanza.
 
Tatizo la Nape ni njaa na alijianimisha kuwa yeye ndie mwenye CCM kisa baba yake alikuwa nae mwenye CCM, Nape huyu huyu ndie alijifanya ana uchungu na mali za Umoja wa Vijana baada ya yalipokuwa makao makuu ya Umoja wa Vijana kukwapuliwa na akina mamvi na wahindi wenzake na akasahau kuwa mamvi hakuwa peke yake, matokeo yake akawa anabweka tu na hakuna lolote alilofanya nae ndio akaanza tabia za wizi wa mali za CCM na bwana Ndovu na yule babu wa Lushoto, huyu Nape ni genge la wahuni na wezi na hana uchungu wowote kelele zote za sasa ni kutaka cheo serikalini, ukiangalia timu yake ya mwanzoni wenzake wote ni mawaziri,Bashe,January ni yeye na mtoto wa remote ndio hawamo kwenye baraza ingawa bado mtoto wa remote ameanza kuwa na nguvu hivi sasa kutokana na nguvu za remote alizonazo hivi .

Mtoto wa Remote anapigiwa campaign ya nguvu sana ili akubalike kuingizwa serikalini. Mke anaweza kupewa madaraka makubwa tu.

Sekta muhimu zote,Madini, nishati, kilimo, biashara vyote waweke watu wao. Wapiga dili.
 
Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Mbunge wa jimbo LA Mtama Mh Nape Moses Nnauye,ameibua mjadala mitandaoni kwa hoja yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni ya kutaka kuwepo kwa uchunguzi wa kina kuhusu hoja iliyoibuka ya kuwepo kwa deni kubwa LA taifa.
Hoja yake ni muhimu,ya msingi ijadiliwe.

Uweke msisitizo huo huo kwa matumizi ya yote ya sasa, mikopo, kodi, tozo zote na wale wote waliohusika kupitisha hayo matumizi, wote hadi viongozi wa sasa.Wawajibike.
 
Huo uchunguzi utafanyikaje wakati viongozi wako madarakani
 
Huo uchunguzi utafanyikaje kati viongizi wako madarakani

Kabisa hadi uteuzi,utenguzi awamu hii unazingatia vigezo gani?

Mtu alichukua mikopo mabilioni ya pesa za walipa kodi NSSF kifisadi anapewa wizara, haijalipa. Anashangiliwa.

Anatenguliwa aliyefanya umeme usikatike, kusimamia kwa usahihi kujenga bwawa jipya kupunguza tozo za umeme.

Mantiki, vigezo vyote vya maamuzi, CV zao, kazi zao zote tuwekewe wazi.
 
kuna msemo wa wazungu unasema "Marehemu hawezi kujitetea" kila la kusemwa litasemwa ila kamwe hatutaweza kusikia upande wa mlalamikiwa ukitoa ushaidi
Kama mnaamini nadharia za aina hiyo msigombee nafasi za uongozi wa uma.
Uma una haki kukukosoa bila kujali uko hai au laa.

Dunia nzima inaongelea matendo ya viongozi wao, walio hai hata waliofariki, sisi ni nani hasa tusihoji ubadhirifu wa viongozi wetu?
 
Back
Top Bottom