Nilichokurupuka ni kipi? au kwasababu nimepingana na hoja ya kuwaita vijana bomu kila siku? Na kisa kasema flani? Lazima umtukane nape na kumwita mbumbumbu ndio siku yako iende?... Serikali imetoa takwimu za hali halisi ya ajira nchini, nikatakiwa kutoa maoni, nilichojibu kuwa serikali iko sahihi, hali ya ajira nchini kwa takwimu sio maneno ya barabarani, na hasa ukilinganisha na nchi hata za Afrika mashariki tu Tanzania ni bora kuliko zingine, umbumbumbu wa Nape uko wapi?
Nadhani ni vizuri pamoja na kutakiwa kutukana kila unapokuta jina la Nape, akili za kuambiwa changanya na zako....
Kwanza nimefurahishwa na utayari wako wa kutetea kile unachoamini. Kuhusu suala la ajira kwa vijana nadhani utakuwa ama kujamwelewa vyema waziri mkuu mjiuzulu Lowassa au kwa makusudi unabadili kile alichosema ili upate hoja za kumpinga. Hakuwaita vijana mabomu bali alisema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ndio bomu. Sio kweli pia kuwa Mh. Lowassa amekuwa akiwaita vijana mabomu kila siku kama unavyodai kwenye hoja yako.
Tukirudi kwenye ukweli wa mambo suala la ukosefu wa ajira kwa vijana lipo na kama alivyosema Mh. Lowassa ni bomu linalosubiri kulipuka. Ni kweli serikali na sekta mbalimbali wamekuwa wakiajiri vijana wanaomaliza masomo kwenye ngazi mbalimbali lakini kiwango cha ongezeko la vijana wanaohitaji ajira baada ya kumaliza masomo yao ni kikubwa kuliko kiwango cha ajira zinazotolewa nchini. Hii imesababisha ziada ya vijana wasiokuwa na ajira ambao idadi yao inaongezeka kila mwaka. Kwa lugha ya kimahesabu wakati ambapo ajira zinaongezeka "arithmetically" idadi ya vijana wanaohitaji ajira imekuwa ikiongezeka "geometrically" na kusababisha ongezeko la vijana wasioajiriwa.