Nape amfyatua Mwigulu kuhusu BMK

Nape amfyatua Mwigulu kuhusu BMK

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,073
Reaction score
134,453
SIKU moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba kunukuliwa na gazeti la serikali la Habari Leo akitamba kupinga nyongeza ya siku 60 za Bunge la Katiba, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, amempinga akisema hawezi.

Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alitoa tambo hizo juzi mjini Iringa wakati akihutubia mkutano wa hadhara, akisema kuwa atapinga kwa nguvu zake zote Bunge hilo kukutana kwa siku nyingine 60.

Hata hivyo, msimamo wake unakinzana na chama chake ambacho kimeapa kwamba hata kama wajumbe wenzao wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wasiporudi bungeni, wao wataendelea na Bunge hadi katiba mpya ipatikane.

Katika kikao chake cha Kamati Kuu cha hivi karibuni, CCM iliazimia kupambana na UKAWA popote, nje na ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, huku ikisisitiza kwamba haiwezi kuwabembeleza warudi bungeni kwa sababu chama hicho kinao wajumbe wa kutosha kutimiza theluthi mbili ya kura zinazotakiwa kikanuni.

Kufuatia mkorogano huo, Tanzania Daima Jumatano lilimtafuta Nape jana kwa simu akiwa ziarani mkoani Manyara ili kupata msimamo wa chama kuhusu katiba mpya.

Katika majibu yake kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu, Nape alisema: "Gazeti la Habari Leo limemnukuu vibaya Mwigulu. Hawezi kupinga jambo ambalo rais amelipitisha.

"Chama kupitia vikao halali kimeishatoa tamko na msimamo unajulikana. Vinginevyo ili ampinge rais, yeye kama naibu waziri alipaswa ajiuzulu kwanza. Hata hivyo, naibu waziri haruhusiwi kuwasilisha hoja binafsi."

Kwa mkanganyiko huo, ni dhahiri CCM wanakinzana katika suala zima la upatikanaji wa katiba mpya inayotokana na matakwa ya wananchi.

Itakumbukwa kuwa katika siku za hivi karibuni kwenye mikutano yao ya hadhara iliyofanyika visiwani Zanzibar na mkoani Tabora, CCM kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana na Nape walisema kuwa hawahitaji katiba mpya kwa sababu sio muarobaini wa matatizo waliyonayo wananchi.

Viongozi hao walisisitiza kuwa hata katiba mpya ikipatikana itawekwa kabatini, huku Nape akizidi kuwashambulia wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, akisema wamekengeuka kwa mapendekezo yao ya muundo wa serikali tatu.

Licha ya rasimu ya katiba kupendekeza muundo wa serikali tatu, CCM imekuwa ikiendesha harakati za kuipindua, ikitetea muundo wa sasa wa serikali mbili uendelee, jambo linalopingwa na UKAWA hadi kufikia hatua ya kutoka nje ya Bunge hilo.

Katika mkutano wake wa mjini Iringa, Mwigulu alipinga Bunge hilo lisiongezewe muda kwa madai kwamba likiendelea kwa mtindo kama wa awamu ya kwanza, itakuwa sawa na kutumia vibaya fedha ya walipa kodi.

Aliahidi kumshauri Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta, amuandikie barua Rais Jakaya Kikwete, ili avunje Bunge hilo endapo wajumbe wake watashindwa kutumia wiki mbili za mwanzo kujadili mambo ya msingi katika rasimu hiyo.

Source: Tanzania Daima

My Take: UKAWA warudi bungeni only and only if itaamuliwa kujadili rasimu ya wananchi na sio ya Kikwete
 
Katibu wa itkadi na uenezi wa CCM,NAPE NNAUYE amemwambia Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho MWIGULU NCHEMBA kuwa hana uwezo wakuzuia kuendelea kwa Bunge la katiba kwa kuwa yeye pia ni Mjumbe wa Bunge hilo,Hvyo akitaka mpaka kwanza Ajiuzulu nafasi hyo,
CHANZO TANZANIA DAIMA TOLEO LA LEO.
 
Katibu wa itkadi na uenezi wa CCM,NAPE NNAUYE amemwambia Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho MWIGULU NCHEMBA kuwa hana uwezo wakuzuia kuendelea kwa Bunge la katiba kwa kuwa yeye pia ni Mjumbe wa Bunge hilo,Hvyo akitaka mpaka kwanza Ajiuzulu nafasi hyo,
CHANZO TANZANIA DAIMA TOLEDO LA LEO.

sijawahi kuimini habari yoyote ya tanzania daima ni gazeti la udaku
 
Laana na iwatafune kama wale wa Babeli
 
Sijaona, kama kinachoendelea kati ya akina-Kinana na serikali yake. Ni sawa na kumnanga mkeo hadharani.
 
Na hapo ndio wameanza laana zao zitawatafuna sio mchezo,na vile mchawi wao alishakufa hakuna tiba ni kufa tu ccm sasa.
 
Wanapima upepo wote ni wale wale tu.wanafanya tafiti kisiasa ili kuway out the best option ili kikinusuru chama
 
tanzania daima sijui wanapata faida gani kuandika uongo kama huu.
 
Katibu wa propaganda wa CCM amemshukia Dikteta Mwigulu Nchemba kutokana na kauli ya yake ya kuongeza siku za kujadili rasimu ya katiba mpya. Nape amesisitiza kuwa kama anataka kufanya hayo basi hana budi kujiuzuru mara moja

Source: Tanzania Daima

My Take: UKAWA warudi bungeni only and only if itaamuliwa kujadili rasimu ya wananchi na sio ya Kikwete

Tatizo lenu kazi ya mwigulu na nape humuijui pia hamjui wanafanya nini kwa akili yako unadhani wanapiga siasa tu ngoja wakuache njia panda.
 
tanzania daima sijui wanapata faida gani kuandika uongo kama huu.

Hivi wewe ni kiziwi au kipofu funguka for your family future.wewe mama kweli yaani kitu kimetokea na msomari kamuambia savimbi hivyo.maintarahamwe kidonda sugu.
 
Atakuja hapa MwanaDiwani kutoa ufafanuzi...Tumsubiri,au atasema amenukuliwa vibaya??
 
Tatizo lenu kazi ya mwigulu na nape humuijui pia hamjui wanafanya nini kwa akili yako unadhani wanapiga siasa tu ngoja wakuache njia panda.

kazi zao unazifahamu wewe kigoli!
 
Sijaona, kama kinachoendelea kati ya akina-Kinana na serikali yake. Ni sawa na kumnanga mkeo hadharani.

kwa hiyo kikwete ndiyo mke au mme maana kinana juzi alisema serikali ya ccm ni dhaifu...
 
Magazeti yakufungia vitumbua bavicha na ukawa kwao ndiyo gazeti la habari.
 
Back
Top Bottom