Nape amefuata nini udom?

JACADUOGO2.

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
930
217
Jamani ndugu zangu wanajf naombeni tuwe makini na tuache unafiki. Nape Nnauye amefika chuo kikuu cha Dodoma (Udom) majira ya saa 5 asubuhi. Hivi Nape alikuja kufanya nini Udom na alitumwa na nani kwani amekuja na kuingia bwenini na ndani ya baadhi ya vyumba na kudai kuwa anakagua nyufa ndani vyumba na kukagua maeneo machafu ndani ya chuo. Hivi Nape ni injinia wa Udom? Au Nape ni bwana afya wa Udom? Au Nape ndiye msemaji wa wanachuo kwa rais wa nchi? Tunaomba Nape atueleze vizuri alichoijia Udom kwani hatujajua alichokuja kufanya. Mimi ni mwanafunzi wa Udom na ninavyokijua Udom na viongozi wa Udom siyo rahisi kumruhusu mwanasiasa kuingia ndani ya chuo bila wanafunzi kujulishwa juu ya ujio wake na lengo lake. Mbaya zaidi Nape ameruhusiwa kuingia hadi ndani ya vyumba vya wanafunzi. Hata Lema hakuwahutubia wanafunzi ndani eneo la chuo. Tunaomba ufafanuzi!
 
amekuja kusalimia ndugu yake labda.....kumbuka nape si katibu mwenezi tu wa ccm pia ni KAKA,WIFI,SHEMEJI,MKWE,KAKABINAMU, MJOMBA AU HATA MSHENGA WA WATU.....

mix with yours
 
We Arafat unaweza kujilinganisha na Nape? ni Ukweli usiopingika kijana ni mchapa kazi na uchungu na nchi hii. Usisahau yeye kama Katibu Mwenezi wa Chama Tawala ndiye mwenye Ilani na ndiye msimamizi wa yale aliyowaahidi kwa wananchi. Wewe ulitaka ukuta udondoke ndo aende kutoa pole kwa walioangukiwa na ukuta? Kumbuka vijana wa Chuo ndio waliomsimamisha Nape na kumuomba aende kuona hali yao ilivyo kule mabwenini. Jambo usilolijua usilisemee si lazima kila kitu uandike, andika vile unavyovijua.
 
Nape gani tena jamani, huyu huyu mkuu wa wilaya ya Masasi?

Sijui kama analipwa mshahara, wajuzi wajaribu kuangalia hii isije ikawa anakula kodi zetu kwa kukitumikia chama badala ya wananchi.
 
We Arafat unaweza kujilinganisha na Nape? ni Ukweli usiopingika kijana ni mchapa kazi na uchungu na nchi hii. Usisahau yeye kama Katibu Mwenezi wa Chama Tawala ndiye mwenye Ilani na ndiye msimamizi wa yale aliyowaahidi kwa wananchi. Wewe ulitaka ukuta udondoke ndo aende kutoa pole kwa walioangukiwa na ukuta? Kumbuka vijana wa Chuo ndio waliomsimamisha Nape na kumuomba aende kuona hali yao ilivyo kule mabwenini. Jambo usilolijua usilisemee si lazima kila kitu uandike, andika vile unavyovijua.

Usisahau yeye kama Katibu Mwenezi wa Chama Tawala ndiye mwenye Ilani na ndiye msimamizi wa yale aliyowaahidi kwa wananch
Kuna kitu kinaitwa mgawanyo wa madaraka, Nape kuwa na Ilani haina maana kuwa na madaraka ya kuingilia kila kitu. Kanuni za Vyuo zinzkataza shughuli zozote za kisiasa vyuoni.Kumbuka vijana wa Chuo ndio waliomsimamisha Nape na kumuomba aende kuona hali yao ilivyo kule mabweniniHta hao vijana waliomsimamisha ni vihiyo hawajui chochote na inaelekea wapo hapo chuoni kwa kugushi mitihani tu, walipaswa kujua kuwa vyuponi shughuli za siasa haziruhusiwi. Kwani Nape ni Waziri wa Elimu ya Juu?
 
Man sijaona kwanini unalalamika!? kwani UDOM kuna watu flani flani hawatakiwi kukanyaga.. na swali kenda fanya nini kwanini usimuulize wewe uliyemuona..?!!! ukaja ukatujuza huku.. "kumuona umuone wewe swali utuulize ambao hatujamuona"

wasted

Jamani ndugu zangu wanajf naombeni tuwe makini na tuache unafiki. Nape Nnauye amefika chuo kikuu cha Dodoma (Udom) majira ya saa 5 asubuhi. Hivi Nape alikuja kufanya nini Udom na alitumwa na nani kwani amekuja na kuingia bwenini na ndani ya baadhi ya vyumba na kudai kuwa anakagua nyufa ndani vyumba na kukagua maeneo machafu ndani ya chuo. Hivi Nape ni injinia wa Udom? Au Nape ni bwana afya wa Udom? Au Nape ndiye msemaji wa wanachuo kwa rais wa nchi? Tunaomba Nape atueleze vizuri alichoijia Udom kwani hatujajua alichokuja kufanya. Mimi ni mwanafunzi wa Udom na ninavyokijua Udom na viongozi wa Udom siyo rahisi kumruhusu mwanasiasa kuingia ndani ya chuo bila wanafunzi kujulishwa juu ya ujio wake na lengo lake. Mbaya zaidi Nape ameruhusiwa kuingia hadi ndani ya vyumba vya wanafunzi. Hata Lema hakuwahutubia wanafunzi ndani eneo la chuo. Tunaomba ufafanuzi!
Lazima atakuwa anatafuta vijana ili wajiunge na JF tayari kwa kupambana na wapenda nchi yao............... KUMBUKENI JF ILITAJWA KAMA ADUI WA CHAMA CHA MAGAMBA.............. HIVYO KWAO JF NI GAMBA LA CCM KAMA ILIVYO CDM............. ANAHAMSISHA WANACHUO WENGI WAJIUNGE NA JF ILI TUSHAMBULIANE...........Lakini anasahau kuwa ukweli utabaki kuwa ukweli bila kujali idfadi ya waongo. HATA AKIKUSANYA WANAFUNZI WA VYUO VYOTE WAJIUNGE NA JF ....haitabadili ukweli kuwa
1. Wana CCM wanahusika na wizi wa EPA
2. Wana CCM wanahusika na wizi wa MANUNUZI YA RADA
3 Wana CCM wanahusika na wizi wa MEREMETA
4. Wana CCM wanahusika na wizi wa WANYAMA PORI WA PALE KIA
5 Wana CCM wanahusika na wizi wa UUZWAJI WA LORIONDO
6. Wana CCM wanahusika UOTAJI WA MAGAMBA
7. Wana CCM wanahusika na wizi wa .................. YOU NAME IT.............
 
sasa mnataka aende wapi jamani? first lady kaende bunda kaonyeshwa alama ya V sasa unafikiri Nape anayataka haya mambo? bora aende Udom
 
Albano huna lolote nawe! Bado unaishi katika tabaka lisilotaka kubadilika.Ujima! hoja yako haina mashiko.kwani yeye ni mtendaji wa serikali?Acha kukumbatia magamba kwa kutaka misifa isiyo na dira!
 
mwache aende hata Dilema college akiongea upuuzi atabaki nao mwenyewe akiongea hekima tutachukua for future use
 
Nape ni nani? zaidi ya katibu mwenezi wa ccm au pia kisa anapokeya mishahara miwili kwa mpigo je anamadaraka gani kiserikali ya kuhakikisha huo ukuta unazuiwa kuanguka? kama umefuatilia vizuri semina ya professa issa shivji mwamfupe alisema namnukuu ninakushuru prof.kwa lecture yako nzuri na naomba niwahakikishie nyie wanafunzi kuwa tutaendeleya kuwaalika watu mbali2 ila sio wote ni wale tu tunaowaona wanafaa these means itakuwa kwa wale tu wa chama cha majambazi lakini waupinzani hamna ni kwa sababu ya tu ccm wao wakija wanakunya lakini upinzani ukija wataharisha ila naomba uondoe idea yako ya kipumbavu na wenye mtazamo vinyu eti wanafunzi wa udom ndio waliomwomba nape aje aangalie huo ukuta kwa barua ipi? wakati nape amekuja bila hata viongozi wa udoso kujua na management . kubali usikubali kuja kwa Nape ni kujitafutia umaarufu lakini labda kwa wajinga chache tu kama wewe Albano na wanafunzi wengi tumemeshtukia upumbavu wake apeleke siasa za makabila huko na sio hapa udom. hapa ameula ya chuya ambulii kitu
 
hebu weka wazi,alikuwa college gani? maana huku education hajafika kwani huku mtu kama yule kuja lazima kungelipuka na angetolewa kwa kasi,maana amekuja kisiasa.Kama alikuwa social science huko nasikia ccm hamuitaki ila kusema mnaogopa!shauri yenu sie huku coed tayari ccm wanaishi kama wapo exile,maana madudu ya chama chao yanawasuta.
 
Back
Top Bottom