Nape akimbia nguvu ya Mnyika Ubungo

Nape akimbia nguvu ya Mnyika Ubungo

Nape, kamwe haiwezi Ubungo, na sio Nape tu, bali asilimia 80 ya wabunge wa CCM hawayawezi majimbo yaliyo chini ya UKAWA, ikiwemo Ubungo! Ndio maana CCM inabanana na Tume ya Uchaguzi ili kuongeza Majimbo mapya ili ipate ahueni, maana mwaka huu UKAWA inakula majimbo ya CCM kwa zaidi ya nusu!

Kuna point hapo mkuu.Ubungo kwa uchaguzi wa 2010 ndio ilikuwa inaongoza kwa idadi ya wapiga kura takribani 350000 ila kwa fitna za tume hawakuligawa jimbo hilo,ila kwa vyovyote vile CCM ijiandae kisaikolojia maana siku zao zinahesabika kutoka Magogoni
 
Tupa kule fisadi nape hilo.....mtz gani atampigia kura ya kuwa mbunge.
 
Nape namhurumia sana nafuu angekimbilia mbinguni ambako UKAWA hawawezi kufika angekuwa amefanikiwa kukimbia mafuriko ya UKAWA. Ili mradi kakimbilia mtama ambako UKAWA wanaweza kufika,Nape ajiandae kusombwa na mafuriko ya UKAWA.

Mwaka huu haponi mtu, hata kama watatafuta urafiki na panya wakajificha kwenye mahandaki ya panya watachomolewa tu.
 
Maoni ya Mtatiro kuhusu Jimbo la Mtama

"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014 ni ushahidi muhimu kuwa CCM bado imeweka mizizi Mtama na kwamba upinzani lazima upinde migongo. Kati ya vijiji takribani 100 vilivyofanya uchaguzi, CUF imepata vijiji 15 tu, CHADEMA 1 na CCM zaidi ya vijiji 80 na kwa upande wa vitongoji zaidi ya 300 vilivyofanya uchaguzi – CCM imepata 223 huku CUF ikipata 89. Kwa vyovyote vile iwavyo, bado hakuna miujiza ya upinzani kuchukua jimbo la Mtama, juhudi zozote kwa sasa zitakuwa na maana ya kupunguza ushindi wa CCM tu.

Wana Mtama wanaichagua CCM si kwa sababu kuna jambo la maana imewafanyia katika kipindi cha miaka 15 ya Benard Membe, la hasha! CCM inatamba Mtama kwa sababu Upinzani haujafanya kazi kubwa, ya muda mrefu na inayosimamiwa na makada waliojitoa kufa na kupona kuhakikisha kuwa sauti za wananchi zinajibiwa kwa kupewa matumaini kabla ya kutoa kura zao kwa mtu makini. CCM wakimsimamisha mgombea yeyote anaweza kushinda bila tabu hapa Mtama".
 
rallphryder
mimi ni mwana kusini ni kweli wengi huku kusini tumelala mno kila anayetaka ubunge wa bure anakimbilia kusini.
 
Last edited by a moderator:
IWE MVUA AU JUA, NAPE hawezi pita Jimbo la mtama,CCM lazima ilijue hili,ikijafanya Kichwa ngumu na kumpitisha NAPE JIMBO LINAENDA UKAWA, alishatia nuksi Ubungo 2010, jimbo likaenda CDM.

Nape hatakiwi na wana mtama na alishaambiwa,hajawai kua na nasaba wala urafiki na jimbo la Mtama, Nape aliulizwa ulipokua mkuu wa wilaya masasi mbona ukuwai tembelea watu wa mtama, alikosa jibu.

Watu wa MTAMA HAWATAKI KUWA DARAJA, kamwe kizazi cha kina NNAUYE hakina HISTORIA NJEMA na mikoa ya kusini, sio Nape,wala anaesemwa kuwa ni babayake,waliitupa kusini,maneno haya nitakuja yakumbusha mwezi November 201.

NAPE ni Mgombea wa Membe sio CCM,Membe mwenyewe hatakiwi kwa alichowafanyia watu Lindi,ameua kiwanda cha Cement, alidanganya atamleta Dinosaur Lindi kutoka German, hajafanya ilo.
 
mkuu kule mtama nape anajua wana mtama watapewa kanga na kapelo na kisha jamaa atapewa ubunge kiulaini kabisa.

NAPE hawezi pita,na ikitokea bahati mbaya emepitishwa,wananchi na wazee wa Mtama jimbo zima kwa ujumla,wamesema kura zinaenda UKAWA
 
nape amekimbilia kwa ndugu zangu wa lindi ili akagombee ubunge. wana mtama kuweni makini sana.kumbukeni masuala ya gesi yetu.

Hawezi pita mkuu,ata aonge kiasi gani,Nape ni Mgombea wa Membe sio CCM,kamwe na Abadani hawezi pita...ikilazimishwa jimbo linaenda Ukawa,ukawa wajipange tu,kunamgombea wa TLP alipata kura 4000 nk,tena alirudishwa bado wiki mbili na Tume ya uchaguzi
 
mkuu kule mtama nape anajua wana mtama watapewa kanga na kapelo na kisha jamaa atapewa ubunge kiulaini kabisa.

Watz wa sasa sio kiazi km zamani.....SASA WANAJUA maccm YOTE NI MAJIZI TU HAKUNA MTETEZI WA WATZ.
nape amalize kwanza sinema yake ya kuwavua gamba mafisadi wa ccm km alivyoahidi vinginevyo anapoteza tu muda
 
Hahahaha ubungo amemwachia bondia wa wazee mwenye uzoefu wa kupigwa mawe ubungo aka makonde
 
Habari wana jamvi,

Wakati joto la uchaguzi mkuu likiendelea kupamba moto imefahamika kuwa jimbo la ubungo wagombea wengi wameanza kuogopa nguvu ya JJ Mnyika ambapo sasa wameamua kutafuta majimbo mengine.

Mmoja wa wanasiasa ambae amekimbia moto wa Mnyika ni bwana Nape Nnauye ambae ameenda kujiandikisha kupiga kura Jimbo la Mtama Mkoani lindi,itakumbukwa kuwa mwaka 2010 kwenye kura za maoni za CCM Nape alishiriki kuomba ridhaa ya chama chake kupitia Ubungo na kushindwa na Shamsa Mwangunga.

Heko Mnyika juhudi zako kwa jimbo la Ubungo zimeoneka na chama tawala kimejianda kuwa chama pinzani.Naaomba UKAWA wazidishe kutoa elimu ya uraia hasa umuhimu wa kupiga kura hasa maeneo ya vijijini kama Mtama ili hata kile walichobakiwa nacho kipotee kabisa.

Nape na kadi yake Mtama

8.jpg

ni hawa ng'humbi na sio shamsa
 
Kweli mnyika juhudi zako ubungo zimeonekana kina masawe wanatuuzia maji kwa sh. 1000 kwa dumu la lita 20 wapishi wa gongo wameongezeka makoka na kirungule nakumbuka 2010 ulikuwa unatembea mpaka saa sita usiku kuomba kura ktk vibanda vya gongo leo gongo yote ya dsm inatoka makoka.

Wizi wameongezeka ubungo ktk kipindi chako daladala za ubungo makoka nauli 600 badala ya 400 ni umbali ea km moja na nusu kwa sababu barabara haipitiki hata wenye magari hawafiki na magari yao makoka wanalaza river side.

Vyoo vya shule nyingi za ubungo ni taabu UTI zimetawala kwa watoto wetu . Madawati hamna . Sitoacha kusema kweli najutia kura yangu kwa Mnyika.
 
Kiukweli Jimbo la Ubungo ni jimbo gumu, 2010 CCM ilifanya kosa kusimamisha debe tupu!, kosa hili CCM imeligundua kosa hilo na kuamua kufuata ushauri wa Mwalimu Nyerere, kuwa "kufanya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa!", hivyo 2015 CCM hawatafanya kosa tena, na uamuzi wa Vuvuzela kuliepuka jimbo hilo linalohitaji watu makini kama JJM, ni uamuzi wa busara, hivyo kuamua kugombea majimbo ya vibonde!.

Pasikali
 
Acha kudharau na kukashifu binaadamu wenzako. Nyie wa kaskazini mna ubaguzi sana na dharau kwa watu wa kusini.
Mbona huu ulioufanya pia ni ubaguzi...lakini ni kweli watu wa kusini wamelala...hawajitambui
 
Back
Top Bottom