VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,006
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye amekivua nguo chama tawala.Amedai kuwa wakati wa kampeni,vyama hubeba watu kutoka sehemu mbalimbali ili kujaza wahudhuriaji.Watu hao,ingawa si wapiga kura,hubebwa ili kuuhadaa umma kuwa mkutano wa chama husika umehudhuriwa na umati wa watu.Hakutaja ni chama gani hasa.Nani asiyejua kuwa mtindo huu hutumiwa na CCM tu? Kwanini Nape ameamua kuiumbua nyumba yake?
Kama hiyo haitoshi,Nape amedai kuwa CCM ina utaratibu wa kuwalazimisha wanachama wake kujiandikisha na kupiga kura. Akitoa mfano,Nape amedai kuwa hata kwenye kura za maoni CCM ilanzisha utaratibu wa kila mwanachama kuwa na kadi mbili:ya kupiga kura na ya uanachama.Nani hajui kuwa huu haukuwa utaratibu rasmi wa CCM? Utaratibu huu ulileta sintofahamu kubwa ndani ya CCM kwa kuletwa kwa kukurupuka.Uliwalenga wachache ili washindwe.Nape ameudanganya umma.Amefanya kusudi?
Source: Mahojiano yake na Issac Gamba wa Radio One Stereo katika kipindi cha Hoja ya Leo jana.