Nape aivua nguo CCM,audanganya umma...

Nape hawezi kunitoa nyumbani kwenda kumsikiliza hata kama yuko hatua 10 kutoka nyumbani kwangu hafai kazi kulopoka maongezi yake hayana mshiko.
 
yupo umu JF anasoma ujumbe , but habadiliki , hajifunzi, anyway yeye na waliompa nafasi, na chama chake kwa ujumla sio watu makini, naamini kila anachofanya anakuwa ametumwa na anasema kama kilivyo , they are on the way to their grave

Nape ni kijana anayeweza kubadilika na kufuel mabadiliko, tatizo kazungukwa na madingi maconservative hadi basi, pale hapumui, ataongea mpaka atajichanganya awaudhi wazee wake, mwisho si mzuri, magamba hayo ni kama ya kobe hayavuliki kirahisi labda umuue kobe mwenyewe

my take; take care Nape, watakuponza wanamtandao, hawata dumu milele. watakupa kichwa sasa hivi kesho hawapo madarakani si kwenye chama wala serikalini.
 
Hivi Nape ndivyo alivyo? Au anatekeleza maagizo na ndivyo asivyo? Hivi huyu kijana vipi huyu? Akizeeka je? Atakuwaje? Mbona anaropoka sana? Akiipenda siasa, basi aachane na ccm, vinginevyo anajichimbia kaburi refu la kujizika mwenyewe.
 
Nape anaipenda CCM ila hapendi yanayofanyika ndani yake na hana ubavu wa kubadilisha chochote. Tumuombee tu ili wasije waka -MKOLIMBA
 
Hayo yote yanatokana na vuguvugu la M4C,.maji yameshawafika shingoni na bado huo ni mwanzo tu watatueleza mengine mengi tu hata ambayo hatujawahi kusikia wala kuyafikiria,.they are on the death row...
 
Yuko sawa. ccm wanabeba watu kwenye malori. Sasa jambo la kujiuliza mbumbumbu ni wanaobwebwa au wanobeba? Hivi wananchi wakikataa kuingia kwenye hayo malori watakamatwa kwa nguvu? Nape na wenzake wameshapima kuwa watanzania hamnazo siku moja wakiona malori yao yanapata hasara watabeba watu kwenye majeneza na kwa kuwa yatakuwa majeneza ya chama dume, chama tawala watu watapanda tena kwa kugombania.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye amekivua nguo chama tawala.Amedai kuwa wakati wa kampeni,vyama hubeba watu kutoka sehemu mbalimbali ili kujaza wahudhuriaji.Watu hao,ingawa si wapiga kura,hubebwa ili kuuhadaa umma kuwa mkutano wa chama husika umehudhuriwa na umati wa watu.Hakutaja ni chama gani hasa.Nani asiyejua kuwa mtindo huu hutumiwa na CCM tu? Kwanini Nape ameamua kuiumbua nyumba yake?

Kama hiyo haitoshi,Nape amedai kuwa CCM ina utaratibu wa kuwalazimisha wanachama wake kujiandikisha na kupiga kura. Akitoa mfano,Nape amedai kuwa hata kwenye kura za maoni CCM ilanzisha utaratibu wa kila mwanachama kuwa na kadi mbili:ya kupiga kura na ya uanachama.Nani hajui kuwa huu haukuwa utaratibu rasmi wa CCM? Utaratibu huu ulileta sintofahamu kubwa ndani ya CCM kwa kuletwa kwa kukurupuka.Uliwalenga wachache ili washindwe.Nape ameudanganya umma.Amefanya kusudi?


Source: Mahojiano yake na Issac Gamba wa Radio One Stereo katika kipindi cha Hoja ya Leo jana.

Nape ameteuliwa na Kikwete na kikwete ndiyo muongo Mkuu unategemea nini?
 
Yuko sawa. ccm wanabeba watu kwenye malori. Sasa jambo la kujiuliza mbumbumbu ni wanaobwebwa au wanobeba? Hivi wananchi wakikataa kuingia kwenye hayo malori watakamatwa kwa nguvu? Nape na wenzake wameshapima kuwa watanzania hamnazo siku moja wakiona malori yao yanapata hasara watabeba watu kwenye majeneza na kwa kuwa yatakuwa majeneza ya chama dume, chama tawala watu watapanda tena kwa kugombania.
Ukatae kuingia kwenye roli wakati wanagawa na posho, pilau ya bure na ze comedy ya bila kiingilio.Lakini cha kufurahisha pilau wanakula na kura kwa CDM hayo ndio malipo ya kufikiri watu wote ni wajinga.
 
Mwache Nape aitwe Nape msomi mzuri lakini .......!!!!,iwache CCM iitwe CCM lakini majibu yake 2015,kama mtoto wa mwanasiasa anakuwa mwanasiasa na anataka chama kilekile cha baba yake unategemea kuna mabadiliko? ni siasa zile za mwaka 47!kwa msemo mwingine bado ana mawazo ya baba yake ya kupigania uhuru kusini mwa jangwa la sahara,au kulinda maslahi ya watangulizi wao na hawa wako wengi kina Mwinyi,Kawawa,Nchimbi,Ridh.....,Msuya na wengineo lukuki, Ila kama chama kinarithiwa kihivyo ina maana siye hatuna chetu bali ni kuelezwa maneno mazuri ili usishituke kujua kinachoendelea(kuvua magamba),wenye akili timamu(vijana)wameamua kuchagua kingine,ikiwa propaganda zitaendelea kihivyo basi 2015 mhnnnn...........malizia mwenyewe.watangulizi hawatakuwepo
 
Miongoni mwa vijana ambao nilikuwa nawaheshimu kwa kuwa walionyesha kuleta mabadiliko ni pamoja na huyu bwana kabla ya kupewa Cheo,Baada ya kupewa cheo amebadilika sana na kutoa kauli ambazo hazina utafiti wa kutosha na mwisho wake huishia kuwa kauli dhaifu.kwa maoni yangu pengine bwana huyu hutoa matamko kwa kufurahisha kundi fulani na kushambulia kundi ambalo halipendi yeye na ndio maana kauli zake huangukia patupu.Namwomba abadilike ili aweze kushirikiana na vijana wenzake kuleta mabadiliko katika nchi yetu.

Mwisho naomba niwashirikishe kituko ambacho ni cha kweli na nimekishuhudia mwenyewe.
Kuna jamaa yangu alikuwa anaangalia TV na mara akatokeza bwana Nape na matamko yake,Jamaa alikwazika na kushindwa hata kula chakula na kumpelekea kutapika sana kwa kukwazwa na Nape tena kwenye TV.kila mara nikimwona Nape huwa namkumbuka huyo Jamaa yangu.
 
mh nape? baade atasema wamemsingizia ila kama mambo hayaendi si aamie cdm?

ccm ni wezi tunajua hila zao zote dawa yao imeshapikwa ni kuwapa tu na safari hii jino kwa jino wakiiba kichapo hapo hapo kituo cha kupiga kura.
 
Back
Top Bottom