Nape ailipua CHADEMA

Nape ailipua CHADEMA

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
NAPE AILIPUA CHADEMA!!
Posted on 23:40

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, amewataka wananchi wasikubali kuandamana kwa shinikizo la viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili kushinikiza Bunge Maalumu la Katiba lisitishe vikao vyake kabla ya Oktoba 4,2014.

Bw. Nnauye aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani na kusisitiza kuwa, maandamano hayo aachiwe Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bw. Freeman Mbowe, familia yake na viongozi wengine.

Alisema chama hicho kina utamaduni wa kutumia damu za Watanzania kama mtaji wake kisiasa kwani vyombo vya dola vinapochukua hatua ya kuzuia maandamano, wanaoathirika si viongozi wa chama hicho au familia zao ndio maana wanaona fahari watu wanapokufa.

"Upinzani katika nchi hii umegeuka kuwa laana, kazi kubwa ambayo wanaifanya ni kuchonganisha watu na Watanzania ni mashahidi, maeneo ambayo CHADEMA wamefanya maandamano, watu maskini wamepoteza maisha.

"Viongozi wa CHADEMA wanabaki salama na familia zao hivyo kama Mbowe anataka kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe, aanze kutangulia yeye, mkewe na watoto zake, Watanzania wamechoka kushuhudia damu za watu maskini zikimwagika," alisema Nape.

Aliwataka wananchi kufahamu kuwa, Katiba haimpeleki mwanasiasa au mtu yoyote Ikulu badala yake kura ndizo zinazoweza kumpeleka Ikulu ambapo CHADEMA, Chama cha Wananchi (CUF) pamoja na NCCR-Mageuzi, wanaamini Katiba ikipatikana ndio inayoweza kuwapa ushindi katika Uchaguzi Mkuu 2015.

"Vyama hivi vinataka kuligawa Taifa kwa kutumia mchakato wa Katiba, umefika wakati wa Watanzania kuachana na upinzani wenye kujenga chuki...CCM na viongozi wake wamekuwa wakihubiri amani, mshikamano na umoja lakini wapinzani wanatumia muda mwingi kuhubiri chuki," alisema.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Abdulrahman Kinana, amepongeza juhudi za Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, kwa juhudi zake za kuwasaidia wanawake na watoto wa kike kupitia taasisi hiyo.

Bw. Kinana alitoa pongezi hizo juzi baada ya kutembelea Shule ya Wanawake ya Wama Nakayama, inayomilikiwa na taasisi hiyo iliyopo kwenye Kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.

Alis ema Mama Kikwete amekuwa na mchango mkubwa nchini kutokana na jitihada zake za kusaidia makundi mbalimbali wakiwemo watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.

Aliwataka wanafunzi shuleni hapo, kusoma kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Mama Kikwete kwani wao ndio viongozi wa baadaye ambao watashika nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Suma Mensah, alisema shule hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Rufiji na nje ya Wilaya hiyo kwani inatoa elimu kwa wanafunzi wasio na uwezo pamoja na yatima.

"Juhudi za Mama Kikwete kwa watoto wa kike zimefanikiwa kwani watoto waliokuwa hawana mwelekeo wa maisha, hivi sasa wanafurahia kupata elimu bora," alisema Mensah.
 
-Super sana Bro Nape. Hawa wahuni wanavuruga nchi yetu. Wakapigane na kiandamani huko hai kwa mbowe. Mamburula kama Ben saa nane wamechoka ku baby sit Jr. Apelekwe hai akalime

-CCM ni chama dume chama cha uhakika. Super sana.

Lebig Show. King of all social network. Sauti ya umeme@NY
 
Mbowe ana familia? Si nilisikia ana kaugomvi cha kudumu na mtoto wa Mzee mtei na sasa kaamuwa kufanya zinaa na mbunge wake wa upendeleo.

Kwi kwi kwi.

Nape, Mbowe hata siku moja hawezi kuleta wanawe kwenye maandamano, saa hizi wanakula pizza Dubai au UK. Cheza na Mbowe wewe? Hata bilicanas hawakanyagi, pale wanaenda wajinga waliwao tu. Itakuwa kwenye maandamano ya kumwaga damu?
 
Mbowe ana familia? Si nilisikia ana kaugomvi cha kudumuna mtoto wa Mzee mtei na sasa kaamuwa kufanya zinaa na mbunge wake wa ependeleo.

-Sista foxy, salute sana. Karibu kijiweni. Jawa chagadema mburilas bin mburals hawana adamu kabisa

Lebig Show. King of all social networking. Sauti ya umeme@NY
 
mbowe ana familia? Si nilisikia ana kaugomvi cha kudumuna mtoto wa mzee mtei na sasa kaamuwa kufanya zinaa na mbunge wake wa ependeleo.

Kwi kwi kwi.

Nape, mbowe hata siku moja hawezi kuleta wanawe kwenye maandamano, saa hizi wanakula pizza dubai au uk. Cheza na mbowe wewe? Hata bilicanas hawakanyagi, pale wanaenda wajinga waliwao tu. Itakuwa kwenye maandamano ya kumwaga damu?

mbona inaonyesha una dalili ya umbeaumbea? Unasikia????!!1
 
It's time now to ignore every kind of being blinded. ENOUGH. these people on power have no future with us. Only oneness can take us to the right way. UKAWA paves the way to YES. If we real feel and have passion for our nation, we can't let the few to play behind our "back".
 
Mbowe ana familia? Si nilisikia ana kaugomvi cha kudumuna mtoto wa Mzee mtei na sasa kaamuwa kufanya zinaa na mbunge wake wa ependeleo.

Kwi kwi kwi.

Nape, Mbowe hata siku moja hawezi kuleta wanawe kwenye maandamano, saa hizi wanakula pizza Dubai au UK. Cheza na Mbowe wewe? Hata bilicanas hawakanyagi, pale wanaenda wajinga waliwao tu. Itakuwa kwenye maandamano ya kumwaga damu?

Tunavyoongea sasa, Mbowe yuko Afrika ya kusini anafanya yake!
 
Nape alishajichokea zake.Akaoe kwanza labda atapata akili yake yake mwenyewe.
 
ndugu yangu faiza chama chako kinawafiramisha masheikh wetu jela na ww ukijinasib ni muislam sina mengi ila mwenyezi akuhidi na akuoneshe dhulma inayofanywa juu ya masheikh wetu
 
  • Thanks
Reactions: prs
ndugu yangu faiza chama chako kinawafiramisha masheikh wetu jela na ww ukijinasib ni muislam sina mengi ila mwenyezi akuhidi na akuoneshe dhulma inayofanywa juu ya masheikh wetu
Acha ukinga wa kuleta udini kwenye mambo ya kijamii koma kutumia maneno haya wala kutumia dini kwa manufaa yako.
 
Mbowe ana familia? Si nilisikia ana kaugomvi cha kudumuna mtoto wa Mzee mtei na sasa kaamuwa kufanya zinaa na mbunge wake wa ependeleo.

Kwi kwi kwi.

Nape, Mbowe hata siku moja hawezi kuleta wanawe kwenye maandamano, saa hizi wanakula pizza Dubai au UK. Cheza na Mbowe wewe? Hata bilicanas hawakanyagi, pale wanaenda wajinga waliwao tu. Itakuwa kwenye maandamano ya kumwaga damu?
Amani kwako,habari ya kitambo.
Mbowe siyo mtu wa maana anao hao wengi sana kaharibu mpaka yule mtoto wa wasira aliyehemia chadema kwa sasa anamtoto chadema chaka la michepuko.
 
kama nape anafahamu watanzania wanaoshiriki maandamano ni masikin akiwa kama katibu itikad ccm ,afanye mpango bunge maalum la katiba lisitishe vikao vvisivyo na tija ya kuleta katiba bora kwa watz na hizo posho wanazolipana zitumike kuondoa umasikin kwa watz ,nasema maandamano yapo palepale ,watanzania tuungane tuandamane nchi nzima ,mim saa 11 alfajiri nipo arusha kupanga vijana barabaran had kieleweke ,kama vip tutaingia msituni .
 
It's time now to ignore every kind of being blinded. ENOUGH. these people on power have no future with us. Only oneness can take us to the right way. UKAWA paves the way to YES. If we real feel and have passion for our nation, we can't let the few to play behind our "back".
But you can let the few to play behind ur life
 
Nape nae ana uwezo wa kuilipua cdm? aka mtafute kwanza baba yake ndio aje hapa kuja.mba jam.ba.
 
Mbowe ana familia? Si nilisikia ana kaugomvi cha kudumuna mtoto wa Mzee mtei na sasa kaamuwa kufanya zinaa na mbunge wake wa ependeleo.

Kwi kwi kwi.

Nape, Mbowe hata siku moja hawezi kuleta wanawe kwenye maandamano, saa hizi wanakula pizza Dubai au UK. Cheza na Mbowe wewe? Hata bilicanas hawakanyagi, pale wanaenda wajinga waliwao tu. Itakuwa kwenye maandamano ya kumwaga damu?

Na siku Waislamu wakiamua kuandamana kudai mahakama ya kadhi wakipigwa na polisi usije kulalamika, kwani wakati mwingine wewe uko kama popo
 
Back
Top Bottom