Nape ailipua CHADEMA

Nape ailipua CHADEMA

kama nape anafahamu watanzania wanaoshiriki maandamano ni masikin akiwa kama katibu itikad ccm ,afanye mpango bunge maalum la katiba lisitishe vikao vvisivyo na tija ya kuleta katiba bora kwa watz na hizo posho wanazolipana zitumike kuondoa umasikin kwa watz ,nasema maandamano yapo palepale ,watanzania tuungane tuandamane nchi nzima ,mim saa 11 alfajiri nipo arusha kupanga vijana barabaran had kieleweke ,kama vip tutaingia msituni .


hivi umaskini unaondolewaje??
 
NAPE AILIPUA CHADEMA!!
Posted on 23:40

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, amewataka wananchi wasikubali kuandamana kwa shinikizo la viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili kushinikiza Bunge Maalumu la Katiba lisitishe vikao vyake kabla ya Oktoba 4,2014.

Bw. Nnauye aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani na kusisitiza kuwa, maandamano hayo aachiwe Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bw. Freeman Mbowe, familia yake na viongozi wengine.

Alisema chama hicho kina utamaduni wa kutumia damu za Watanzania kama mtaji wake kisiasa kwani vyombo vya dola vinapochukua hatua ya kuzuia maandamano, wanaoathirika si viongozi wa chama hicho au familia zao ndio maana wanaona fahari watu wanapokufa.

"Upinzani katika nchi hii umegeuka kuwa laana, kazi kubwa ambayo wanaifanya ni kuchonganisha watu na Watanzania ni mashahidi, maeneo ambayo CHADEMA wamefanya maandamano, watu maskini wamepoteza maisha.

"Viongozi wa CHADEMA wanabaki salama na familia zao hivyo kama Mbowe anataka kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe, aanze kutangulia yeye, mkewe na watoto zake, Watanzania wamechoka kushuhudia damu za watu maskini zikimwagika," alisema Nape.

Aliwataka wananchi kufahamu kuwa, Katiba haimpeleki mwanasiasa au mtu yoyote Ikulu badala yake kura ndizo zinazoweza kumpeleka Ikulu ambapo CHADEMA, Chama cha Wananchi (CUF) pamoja na NCCR-Mageuzi, wanaamini Katiba ikipatikana ndio inayoweza kuwapa ushindi katika Uchaguzi Mkuu 2015.

"Vyama hivi vinataka kuligawa Taifa kwa kutumia mchakato wa Katiba, umefika wakati wa Watanzania kuachana na upinzani wenye kujenga chuki...CCM na viongozi wake wamekuwa wakihubiri amani, mshikamano na umoja lakini wapinzani wanatumia muda mwingi kuhubiri chuki," alisema.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Abdulrahman Kinana, amepongeza juhudi za Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, kwa juhudi zake za kuwasaidia wanawake na watoto wa kike kupitia taasisi hiyo.

Bw. Kinana alitoa pongezi hizo juzi baada ya kutembelea Shule ya Wanawake ya Wama Nakayama, inayomilikiwa na taasisi hiyo iliyopo kwenye Kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.

Alis ema Mama Kikwete amekuwa na mchango mkubwa nchini kutokana na jitihada zake za kusaidia makundi mbalimbali wakiwemo watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.

Aliwataka wanafunzi shuleni hapo, kusoma kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Mama Kikwete kwani wao ndio viongozi wa baadaye ambao watashika nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Suma Mensah, alisema shule hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Rufiji na nje ya Wilaya hiyo kwani inatoa elimu kwa wanafunzi wasio na uwezo pamoja na yatima.

"Juhudi za Mama Kikwete kwa watoto wa kike zimefanikiwa kwani watoto waliokuwa hawana mwelekeo wa maisha, hivi sasa wanafurahia kupata elimu bora," alisema Mensah.

Amekiri kuwa kwa miaka hamsini hawajafanya ki2
 
Na siku Waislamu wakiamua kuandamana kudai mahakama ya kadhi wakipigwa na polisi usije kulalamika, kwani wakati mwingine wewe uko kama popo

Kama kuna mtu anaweza kumsikiliza Nape na kuona anachoongea ni point basi taifa hili bado linasafari ndefu! Kama unajua kuangalia mambo utagundua kua kinana hapendezewi na hotuba za Nape hata kidogo ndiyo maana yeye ameongea tofauti kabisa kwenye huo mkutano maana anajua watu si wajinga wanaelewa kinachoendelea tofauti na Nape anayedhani kuwa anahutubia ng'ombe wasiojitambua! Mtanzania gani asiyejua kinachoendelea bungeni sasa! Ujinga ni mzigo!
 
Back
Top Bottom