Nape Aikubali CHADEMA,Ntagazwa apokelewa rasmi

Next Level, mimi wasi wasi wangu kama mpiga kura ni mmoja tu, kuwa confused na nani nimpigie kura.....................ccm ikimuweka Nape Ubungo, na Chadema ikimuweka Mnyika, tumpigie kura nani wakati tushaambiwa Nape ana dhamira moja na ya chadema na ni kijana machachari?!

sina nia ya kuwa wapinzani wapigwe mawe, lakini pia hakuna haja ya kwenda 'out of our way' na kuwasifu watu walioko kwenye ccm.
 
ulitaka apelekwe mtu mwenye nguvu kutoka CCM kwani umeambiwa kulikuwa na mieleka huko kwenye mkutano wa Chadema? Acha fikira mgando hizo, Nape anatosha sana kuhudhuria mkutano huo,akili na busara za mtu hazipimwi kwa wingi wa mvi, ukubwa wa kichwa na upana wa mdomo.
 
Next Level, mimi wasi wasi wangu kama mpiga kura ni mmoja tu, kuwa confused na nani nimpigie kura.....................ccm ikimuweka Nape Ubungo, na Chadema ikimuweka Mnyika, tumpigie kura nani wakati tushaambiwa Nape ana dhamira moja na ya chadema na ni kijana machachari?!

Naamini hata vitu viwili vikiwa bora, kutakuwa na kuzidiana ubora au kutakuwa na sababu ya kukitofautisha na kingine.......! kwa mfano: tuchukulie Mwalimu Nyerere angekuwa anagombea uongozi fulani Africa pamoja na Madiba.....at the end tungekuja kumpata aliye bora zaidi kati ya hao wawili though wote wawili ni wazuri.....! vivyo hivyo kwa Nape ukimweka na Mnyika kwa mfano....aliye bora zaidi kati ya hawa wawili ndio anapaswa kuchaguliwa no matter anatokea CCM or CHADEMA!

sina nia ya kuwa wapinzani wapigwe mawe, lakini pia hakuna haja ya kwenda 'out of our way' na kuwasifu watu walioko kwenye ccm.
Agreed......lakini kuwasifu wapinzania wetu si kuwa ''out of our way'' utakuwa out of your way kama tu utakubaliana na kila kitu ambacho mpinzania wako anakihubiri na ikifikia hivyo hutaitwa mpinzani utakuwa swahiba na itabidi ujiunge nao......!
 
Ccm wamejawa na dharau, na kuamua kupeleka mtu asijekuwa na jina kwenye ngazi ya uongozi katika mkutano mkuu wa wenzao, lakini hili halishangazi sana, ccm wanajuulikana kwa dharau yao.

Kinachonishangaza ni chadema kufurahia hali hiyo na kumwagia sifa kem kem Nape wakati huu tukielekea kwenye uchaguzi mkuu.

Ikiwa chama cha upinzani kinafikia hatua ya kukiri kwa kujifaharisha kuwa ndani ya ccm kuna watu machachari ambao opinions zao zina matter ndani ya chama hicho, kwanini tukichague chama pinzani?

wanaccm wanaojifanya kuwa ni wanachadema hapa JF utawajua tu kwa maandishi yao. Ona huyu mnafiki naye. Hata level ya kuropoka ya Makamba hajaifikia
 
ulitaka apelekwe mtu mwenye nguvu kutoka CCM kwani umeambiwa kulikuwa na mieleka huko kwenye mkutano wa Chadema? Acha fikira mgando hizo, Nape anatosha sana kuhudhuria mkutano huo,akili na busara za mtu hazipimwi kwa wingi wa mvi, ukubwa wa kichwa na upana wa mdomo.

eh he he heh heeeeeeeeeeee,

kwa jinsi walivyofungwa macho na ufisadi, sidhani kama hawa watetezi wa ufisadi Kiranga na wenzake watakuelewa

natumaini wana ccm h
 
Kwa sisi tunaoangalia beyond personality cult kuna suala moja muhimu tunaliona hapa...! Ondoa "Nape" weka Mwakilishi wa CCM na hivyo kufanya alichokisema kuwa ni kauli ya CCM.

Sasa utamu una kuja hapa ....."akitoa salamu toka chama chake amekiri kwamba CHADEMA ni chama kilichojijenga kitaasis kuliko alivyokuwa akidhani.Nape alikuwa akimwakilisha Katibu wao Mkuu Yusuph Makamba." kauli hii ina nullify propaganda za CCM kuwa CHADEMA ni kama NGO hivi nani chama cha kikabila/kifamilia.....nzuri zaidi ni hii inatoka kwa CCM yenyewe...safi sana..!
 
Kamati kuu ya CCM na watendaji wakuu wote wako Dodoma. Kama alivyosema Iza, hawawezi kuacha (Majenerali) kikao chao kikuu cha kuandaa majeshi ya Oktoba waje kwenye mkutano wa Chadema-wapinzani wo wakuu, ndo maana wakawakilishwa na Mwakilishi ambaye -hata wao wanajua anatosha.
Lakini najiuliza pia , hasa kwa wenzetu hapa wanaosema Chadema wamedharauliwa na CCM, sasa kama ni hivyo si imekwishatokea? Ingekuwa vyema basi wale mnao ona hivyo mtoe ushauri Chadema wafanye nini sasa !-kama kuna tija lakini.
 
kwakweli nimejiridhisha na ile kauli ya ''MEDIA NA UPOTOSHAJI WA HABARI''
 
I think you've had a long day ma man...maana mimi nimeongelea kudharauliwa huko huko unakokuongelea wewe....unless labda macho yangu yananidanganya hapa...

NN,

The guy needs a lil nap or something ... recently, anamwaga pumba kaa hana akili vile. Anajichanganya kweli. Anaauliza maswali na kujijibu mwenyewe na kisha anapinga majibu yake kabla ya kuuliza maswali kwenye majibu ya maswali ya majibu ya mapingo ya majibu ya maswali .... so mixed up
 
Siasa sio uadui mkuu na sijaeleza hayo uliyoyataja popote.

Kwa mfumo wa uchaguzi tulio nao, mbunge kwanza ni wa chama kisha ni wa wananchi wa jimbo, uchaguzi huu ni juu ya sifa za wagombea wenyewe lakini pia vyama na sera zao.

Kumbuka ubunge utakoma pale mbunge akapovuliwa uanachama wa chama chake kwa kwenda kinyume na maagizo ya chama, kutokuliona hili kutapoteza nafasi ya wapinzani kushindana na kuwashinda wagombea wa CCM, ambao katika majimbo mengi nchini wana sifa kuliko wagombea wa vyama vya upinzani.

Ha ha ha,

Ona huyu naye, utadhani anaandika insha ya mtihani wa darasa la nne. Gooosh, ccm imeishiwa kweli
 
Uzuri wa 'huyu jamaa' ni kwamba hana haja na sifa, wala haogopi lawama.Na baada ya hapo hafungamani na upande wowote kumshinda Sukarno pale Bandung. Halafu hana dogo, down to the Oxford comma. Kwa nini numskulls wasiendeshe matumbo?

numskulls have nothing to lose .... katika hili unaonekana kama the guy anayependa sifa kutoka kwa upande ambao anadai kuwa hafungamani nao. Unajionesha kabisa kuwa una team katika hili, so far that team aint chadema!
 
In context, in context my dude.Sijasema CHADEMA wamedharau, nimesema wamedharauliwa.

Ingekuwa hivyo tu ningechill, kwani mangapi fyongo nayaona lakini sina muda? Lakini huyu dada wa CHADEMA kaja na propaganda mbuzi anakenua mpaka jino la mwisho kwamba kapata kumuona Nape ananukia kweli, mimi nikamwambia careful sis, that Nape is a slick attack dog usijione eti 'tuna nia moja' above all kuletewa ki Nape ni diss.CCM wana vi subliminal messages babu kama huko sawa sawa unaweza kutukanwa hivi hivi ukawa unashangilia, usiku unaenda kulala ndiyo unashtuka, alaa, kumbe pale nilitukanwa eenh ?

See, this is what I am talking. It is beyond obsession.
 
Na pia napenda kuwatahadharisha kuhusu Mabere Marando, bingwa wa kuvuruga vyama. Mkijisahau mkamweka jikoni atamwaga sumu kwenye mboga mtatafutana hamtaonana! Si vyote vyafaa kuzoa ati! Muwe makini na hii 'zoa zoa'.

Mkuu huyu jamaa anajulikana kwa uvurugaji wa vyama vinavyochipua vizuri. Yuko kazini huyu.
Tunajua hii toka mwanzo wa vyama vya siasa, the guy is destroyer. Tamwaga upupu mpaka mshangae!!!:becky:
 
Kila ajiungae CHADEMA, akimbilia kugombea Ubunge. Mm hivi ni idiolojia au ni kula kunakowafanya wakimbie CCM na kujiunga CHADEMA.

Kwa maoni yangu, hao wakimbiao CCM na kujiunga CHADEMA na kugombea Ubunge, wanafanya hivyo kwasababu ushindani ndani ya CCM hasa katika kugombea ubunge ni mkubwa sana. Na halai ni mbaya zaidi kwa wazee au wale waliokaa katika uongozi ndani ya chama kwa muda mrefu.

jAMANI KATANGAZA NIA NA HUKO KAMA KUNA WENGINE WATAKAOGOMBEA BASI KUNAMCHAKATO WA KICHAMA UTAPITA ATAKAYECHAGULIWA NDIO ATAKAYEGOMBEA
 
Back
Top Bottom