Napatwa na kichefuchefu kila wakati ila sina mimba wala Malaria!

Pole Mpenzi Sweet Girl kwa hayo maradhi ya kichefuchefu jaribu dawa yangu hii

Asali
safi mbichi ya nyuki wakubwa, imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondowa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu, kwa hiyo tengeneza chai kisha tia kwenye kikombe asali vijiko vinne na unga wa mdalasini vijiko viwili koroga tumia, kesho yake vile vile fanya hivyo utapata nafuu kubwa sana Inshaallah.

Dozi nyingine ya ugonjwa huo, twanga kamun aswad unga wake uwe ujazo wa kikombe cha kahawa, kisha kamua machungwa makubwa 6, juice yake weka kwenye chupa. mgonjwa atatumia kikombe cha kahawa 1x2 wiki moja.

Dozi nyingine ni Dawa inayoitwa (Algama) mpingadume-muubuzi na tangawizi mbichi twanga sawa sawa kisha chemsha dawa hizo ujazo wa maji nusu lita.Mgonjwa atatumia nusu kikombe 1x1 siku 6. tahadhari mama mjamzito asitumie dozi hiyo ni hatari.

Chanzo: P.h.D. Mzizimkavu. Tumia kisha unipe mimi FeedBack Tafadhali.
 
Mgonjwa vipi? unaendeleaje? kama hujapata nafuu nenda kapime mimba baada ya wiki mbili halafu unipm. Pole sana. ndo ukubwa huo. Mia
 
Mgonjwa vipi? unaendeleaje? kama hujapata nafuu nenda kapime mimba baada ya wiki mbili halafu unipm. Pole sana. ndo ukubwa huo. Mia

naendelea vizuri kabisa yaani leo sina kichefu chefu kabisa na nimewza kula vizuri tu.naona wewe mwenzangu ndo unaumwa ugonjwa mbaya wa kung'ang'ania.manake umekazania kweli,oh mimba hiyo!!jamni watu wengine!
 
iko akilini tu , acha kufikiria kuhusu kichefu chefu usjali kawaida tu, itapita.
 
naendelea vizuri kabisa yaani leo sina kichefu chefu kabisa na nimewza kula vizuri tu.naona wewe mwenzangu ndo unaumwa ugonjwa mbaya wa kung'ang'ania.manake umekazania kweli,oh mimba hiyo!!jamni watu wengine!

Mkuu sina nia mbaya. wewe nmekupa dawa badala ya kunishukuru unaniletea jeuri. kwani kupata ujauzito ni kosa? kama kuzaa utazaa tu labda kama wewe tasa. una mawazo finyu kama maisha ya funza. pumbavu zako. Mia
 
naombeni msaada,, mara kwa mara siku za karibuni nimekuwa napatwa na hali ya kichefuchefu kikali sana natamani kutapika ila najizuia...sijawahi kuwa na shida kama hii hapo nyuma, mimba sina malaria sina ila nilimeza mseto hivyohivyo,, lakini kuna mida kile kichefuchefu kinakuja ghafla naweza kaa nacho kama dk 10 au 20
nafanyaje???
 
kapime minyoo. meza mebendazole
 
ok asante ntaenda kupima minyoo...

samtime unaweza kula au kunywa maji ndio kinakuja na mate kujaa mdomoni izo ndo dalil za minyoo ,safura punguza kula bila kunawa mikono ,makachumbri jumla punguza kula ovyo ovyo kama kuku bana
 
Back
Top Bottom