Napatwa na kichefuchefu kila wakati ila sina mimba wala Malaria! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napatwa na kichefuchefu kila wakati ila sina mimba wala Malaria!

Discussion in 'JF Doctor' started by SWEET GIRL, Jan 3, 2012.

 1. S

  SWEET GIRL JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Heshima mbele,
  jamani toka jana nasikia kichefu chefu cha ajabu sana.najua wapo watakao sema ni mimba lakini sina mimba nina uhakika na pia malaria sina.sasa sijajua hichi kichefu chefu kinatokana na nini tafadhali naomba mnisaidie nile nini kipotee??? jana nilitumia ndimu lakini bado nakisikia.kinanipa shida kweli.naombeni msaada.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ulikula nini kabla hujaanza kusikia kichefuchefu?
   
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Una uhakika gani huna kama hujapima?
  Nenda kapime yawezekana ni mimba changa
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kama huna mimba basi yawezekani una minyoo jaribu kucheck
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  kichefuchefu siku mbili? nenda ukamuone doctor aisee. mkesha wa sikukuu ya christmas ulifanyanini?. kwa kukusaidia huduma ya kwanza fanya hivi; Nusa kikwapa chako kama mala 5 hivi.yaani weka mkono kwapani halafu uwe unaunusa. ukivuta kama mala 5 hiyo hali itaisha. hii dawa nilipewa na bibi. huwa natumia kila nisikiapo kichefuchefu na kinaisha. Mia
   
 6. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mmh! MIA!!!
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Inabidi ufungue huduma aisee! Akitoka MziziMkavu unakamata #2,lol
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Hajapata exposure kwa visababishi vya mimba. Haitoshi?
   
 9. S

  SWEET GIRL JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  JF kuna watu wa ajabu!!!wanalazimisha kama nina mimba wakati mimi mwenyewe najijua sina.me nilihitaji daktari aliyepo humu JF aniambie ni kitu gani hasa kinanisibu kwa dalili hizi
   
 10. S

  SWEET GIRL JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  jana nakumbuka asubuhi nilikula chapati,kitumbua na chai.mchana nilipata chipsi na kakuku kidogo plus mboga ya kunde.baada ya hapo ndo nilianza kusikia kichefu chefu.
   
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Je kuna dawa unazotumia regular kama dawa za moyo, arvs na nyinginezo?
   
 12. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Inategemea umri wako na kama unakunywa vileo au la. Ila kuna watu hupata kichefuchefu ama baada tu ya kula (hasa vyakula vyenye maji maji kama supu) au akikaa muda mrefu bila kula.

  Fanya yafuatayo huenda ikakusaidia:

  1. [*=1]Usiwe unakula chakula cha moto na cha baridi wakati mmoja (kwa mfano pilau ya moto na kachumbari/soda baridi).
   [*=1]Kunywa green tea na kula ndizi mbivu asubuhi.
   [*=1]Kama unakunywa pombe, well punguza matumizi yake.
   
 13. S

  SWEET GIRL JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  currently situmii dawa yoyote ile
   
 14. S

  SWEET GIRL JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  pombe situmii na kula yangu ni asubuhi na mchana tu usiku mara nyingi nakunywa plain tea,au matunda na sometimes soda tu
   
 15. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nunua dawa inayoitwa nosic tablet huwasaidia wakina mama wajawazito wanapokuwa wanasikia kichefuchefu na kutapika ni combination ya doxylamine succinate 10mg na pyridoxine hcl 10mg.

  Ukiendelea kutapika mwone daktari.
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280

  Sweet mbona mgumu kuelewa? Unasema huna mimba ulipima? Na kama ulipima kitu gani kilichokufanya ukapime mimba? Njia za kupata mimba unazijua zote?,je unaviamini hvyo vifaa ulivyotumia? Usiwe mbishi kapime mimba wewe
   
 17. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Punguza kula vitu vyenye mafuta mengi, sukari nyingi kwa ufupi vitu vitamu kwako siyo vizuri. Fanya mazoezi hiyo hali itaisha. Dawa ya haraka haraka kupunguza hiyo hali nusa kikwapa chako kama mdau (MIA) alivyosema hapo.
   
 18. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Minyoo hiyo!
   
 19. n

  ngwana ongwa doi Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kanunue phenergan vidonge au metoclopromide vidonge mojawapo ya hizi dawa itakusaidia,vinginevyo sababu za kusababisha kutapika ziko nyingi mfano infection kwenye tumbo nk.yafaa kwenda hosp.ukienda watapima na kubaini chanzo.
   
 20. n

  ngwana ongwa doi Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pia vi vema ukapima na vipimo vingine kama wadau wanavyoshauri.
   
Loading...