Napataje kazi ya Afisa Utendaji Dar es Salaam?

Napataje kazi ya Afisa Utendaji Dar es Salaam?

Jusikafiri

Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
12
Reaction score
67
Salaam,

Mimi ni mtanzania msaka tonge kama wasaka tonge wengine nakumbuka mwaka 2016 nilihitimu diploma yangu katika chuo kinachotambuliwa na serikali ya Tanzania, nina vyeti vitatu apa nilipo cha NTA Level 4,5,6 ila najua kwa kazi niliyoikusudia apo ntatumia cheti cha Level 5.

Jambo langu kubwa nahitaji msaada wa connection yakupata utendaji ndani ya jiji la Dar es salaam, najua ni changamoto ndo maana nimeandika huu uzi ila isingekua changamoto nisingemwaga wino hapa.

Ndugu zangu nisaidieni ntapata vipi hii connection yakupata hata matangazo ya kazi za utendaji ndani ya hili jiji kwasababu ni mji ambao matangazo ya kazi yakitoka kazi kama hizi ni ngumu sana kupata.

Apa najua wengi mtanishangaa kwanini usi apply sehem nyingine, ukweli ni kwamba tangu nimemaliza chuo nipo town na familia inanitegemea nipo nayo na nina vimishe mishe vyangu vya kuniingizia tonge mdomoni ambavyo nikiondoka tu kwenye hili city ntaharibu kila kitu.

Ukizingatia mshahara wa utendaji sio mkubwa sana kuna kipindi nilijaribu kuhama mji kubadili mazingira nikaharibu kila kitu nikaanza upya tena ikumbukwe nna watu nyuma yangu.

Kwaiyo natamani niingie kwenye system nikiwa hapa hapa Dar na kitu kikubwa nimegundua ni mtu ambaye naweza kufanya kazi iyo kwa experience ya mtaa, ni mtu ambaye nafuatwa sana na watu kuwasaidia mambo mbali mbali ukiwa pamoja na ushauri.

Kwa kifupi ndugu zangu nisaidieni connection niingie kwenye system hapa hapa town.

Uzi tayari.
 
Na hili tangazo lako huogopi afisa vipenyo humu ndani [emoji2]

Wanapenda kutumia id mpya id Ina post mbili tayari mtu ashakuja pm anakuuliza habari ya kazi [emoji2]
 
Na Mimi BabaMorgan Naomba connection ya kazi Dar es salaam japo nipo kwetu Namtumbo ila My dreams siku zote nikuishi Dar sema ndio hivyo sijui pakuanzia kabisa.
 
Salaam..

Mimi ni mtanzania msaka tonge kama wasaka tonge wengine nakumbuka mwaka 2016 nilihitimu diploma yangu katika chuo kinachotambuliwa na serikali ya Tanzania, nina vyeti vitatu apa nilipo cha NTA Level 4,5,6 ila najua kwa kazi niliyoikusudia apo ntatumia cheti cha Level 5
Fuatlia matangazo ya ajira za utendaji Ndani ya Halmashauri, omba popote pale.

Ukishaajiriwa popote pale hata iwe Hai milimani. Ukishapata "Check Number" na kuthibitishwa kazini.

Nitafute nikusaidie kuhamia DAR au Karibu na Dar
 
Salaam..

Mimi ni mtanzania msaka tonge kama wasaka tonge wengine nakumbuka mwaka 2016 nilihitimu diploma yangu katika chuo kinachotambuliwa na serikali ya Tanzania, nina vyeti vitatu apa nilipo cha NTA Level 4,5,6 ila najua kwa kazi niliyoikusudia apo ntatumia cheti cha Level 5
Usilazimishie tu kwenye utendaji, tafuta kazi yoyote ya utawala au mfuate mtendaji direct atakupa mbinu
 
Mwezi wa 6 zilitoka nafasi halmashauri karibu zote na wengine wamemaliza usahili wiki iliyopita,
 
Dar zenyewe zilikuwepo na usahili walishafanya
 
mwezi wa 6 zilitoka natafasi halmashauri karibu zote na wengine wamemaliza usahili wiki iliyopita,
Nahitaji madini kama ayo kwasasa ngoja niingie kweny ajira tu nadhani sikuwa mfatiliaji kiundani ila kwa sasa nahitaji acha nifatilie ukipata update usisite kunitag fursa
 
Nahitaji madini kama ayo kwasasa ngoja niingie kweny ajira tu nadhani sikuwa mfatiliaji kiundani ila kwa sasa nahitaji acha nifatilie ukipata update usisite kunitag fursa
Unaonekana ni mzembe sana,, Why miezi Ile yote watu wanaangaikia maombi ya Ajira Kila Halmashauri Ila we ulikuwa upoupo tu.. huna smartphone au.

Acha Tabia za kizee, wewe ni kijna kuwa updated... Ajira zote zinapatikana mitandaoni
 
Okey nashukuru kwa msaada.. ila sijawah hangaikia kiundani ajira ndo naanza rasmi.. sihusiani na uzembe kwenye maisha yangu
 
Back
Top Bottom