Napata Mkanganyiko hapa kuhusu hii simu. Sijalala toka jana

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,514
Shemeji baada ya kuona namtengenezea mazingira mazuri ya ndoa yake na Sister akaona simu yangu imechoka sana..hapa naandika nikiwa nmei connect kwenye charge moja kwa moja.

Mtu akinitingisha tu ikachomoka inazima. Basi shem ameonekana kutambua Juhudi zangu na kunipa offer ya kuninulia simu. Anyway haya mengine ni mambo ya kifamilia. Ngoja ni nyooke kwenye point.

Mnaionaje Hii NOKIA G21 kwa sifa na bei yake haizidi 500,000. Kwa wale wanaozifahamu Nokia. Hii ni ya mwaka 2022 February. Je inastahili badala ya xiomi, one plus,redmi na vivo za the same price?

Yaani ingetokea unaambiwa uchague hii Nokia G 21 na Vivo, Xiomi, Redmi,One Plus au Huawei yenye thamani hiyo hiyo ungechagua ipi? Isizidi tsh 500,000.

Wazoefu na Wataalamu please.

Screenshot_20220718-110555~3.png
Screenshot_20220718-110555~3.png
 
Si simu mbaya mkuu ila haina Amoled display

A22 na Redmi note 11 overall ni simu nzuri zaidi,

Mwisho wa siku angalia mwenyewe unataka Stock android ama android yenye features nyingi
So unashari Redmi Note 11? Hiyo A22 ni brand gani? Napokea ushauri Mkuu. Ndo maana nimeleta kwenu. Simu ambayo ukinishauri nikanunue wewe naenda straight dukani kununua.
 
So unashari Redmi Note 11? Hiyo A22 ni brand gani? Napokea ushauri Mkuu. Ndo maana nimeleta kwenu. Simu ambayo ukinishauri nikanunue wewe naenda straight dukani kununua.
Ni Samsung mkuu, hio A22, na redmi note 11 ni ya Xiaomi zote ni simu nzuri kwa budget ya around 400,000
 
Mkuu ipi ni the best. Hasa kwa camera,storage na ubora mwingineo...
All around redmi note 11 ni nzuri zaidi
-Display ni nzuri kwa bei
-Storage yake ni UFS ni nzuri (A22 inatumia emmc)
-speaker, ukaaji chaji, na mambo mengine ya kawaida ipo vizuri pia.

A22 yenyewe ina support kubwa zaidi mambo ya software, sina uhakika ila camera inaweza kuwa pia nzuri zaidi
 
Mkuu. Kesho tu Nachukua Redmi Note 11. Hii nitaiita Chief Mkwawa 1. Nikija nunua ya bei kubwa zaidi itakuwa 2 na kuendelea mbele. Nashukuru sana.
 
Dada hii style ya kudandia wanaume wa watu utafanywa kitu kibaya.
Nimekupa tu ukweli, mtu kakuambia angalau hizo we unakazana the best one... seriously unaweza pata simu the best kwa laki 5?

Afterall mimi nawewe nani atafanywa kitu kibaya? Yaani mtoto wa kiume unajisifu kununuliwa simu na mwanaume anaempanda dadako? Hapo upo chumbani hapo kwa shemeji yako unasikilizia mikito ya dadako huku unangojea simu? One man down!!!
 
Nyie wadada wa hivi huwa hamuolewi na baadaye mnasema sisi wanaume wabaya. Kumbe tabia zenu kama hizi ndo zinatukatisha tamaa.
 
Kwa hio simu ya Laki 5 ndio hujalala unashangaa au mim sijaelewa mada vizuri ?
 
Kweli ndoa inatafutwa sana na Ke kwa udi na uvumba hadi kukutoa 500,000/= ilimradi umuowe fasta kabla ya mambo kuwa mengi na mengi yasiwe mambo
 
Kwa hio simu ya Laki 5 ndio hujalala unashangaa au mim sijaelewa mada vizuri ?
🤣🤣🤣 Hiyo 500,000 ni nyingi sana hasa kwa sisi watu wa kipato cha chini. Yaani sielewi nitawakoga namna gani washkaji kitaa. Mimi kabla ya hii nilikuwa na simu moja kali sana nlipewa na Boss wangu Mhindi baada ya kuwa imeanza msumbua. Hii ndo ninayotumia mpaka leo ina miaka 8.

Sasa imajini napata simu ya tsh 500,000 mpya kabisa . Kuna kulala hapo? Acha kabisa. Hivi siwezi kupata na cover ya chuma au bati ili hata ikitokea bahati mbaya imeanguka isithurike?
 
Shemeji baada ya kuona namtengenezea mazingira mazuri ya ndoa yake na Sister akaona simu yangu imechoka sana..hapa naandika nikiwa nmei connect kwenye charge moja kwa moja.

Mtu akinitingisha tu ikachomoka inazima. Basi shem ameonekana kutambua Juhudi zangu na kunipa offer ya kuninulia simu. Anyway haya mengine ni mambo ya kifamilia. Ngoja ni nyooke kwenye point.

Mnaionaje Hii NOKIA G21 kwa sifa na bei yake haizidi 500,000. Kwa wale wanaozifahamu Nokia. Hii ni ya mwaka 2022 February. Je inastahili badala ya xiomi, one plus,redmi na vivo za the same price?

Yaani ingetokea unaambiwa uchague hii Nokia G 21 na Vivo, Xiomi,Redmi,One Plus au Huawei yenye thamani hiyo hiyo ungechagua ipi? Isizidi tsh 500,000.

Wazoefu na Wataalamu please.

View attachment 2295034View attachment 2295034
Cha msingi tafuta simu yenye storage kubwa, ram kubwa na muhimu zaidi yenye battery kubwa basi simu za sikuizi za budget hua ni nzuri sana hata usihofu
 
Back
Top Bottom