Napata kigugumizi kumsamehe huyu binti

Napata kigugumizi kumsamehe huyu binti

bongompya

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2015
Posts
224
Reaction score
43
Yalishanikuta ila Mungu ndo aliye nisaidia kushinda msala huo,Demu alikua anakuja geto namgegeda analala mpaka anapika na kufanya majukumu yote yanayo muhusu mwanamke wa kiafrica,mwanzoni tulikua tunatumia ndom,baadae akanishawishi kwamba tuache kutumia kwa sababu yeye ni muaminifu na Mimi pekee ndie mpenzi wake wa dhati,basi nikashawishika kutotumia ndom baada ya kujizihilisha kwamba tupo safi,baada ya mwaka mmoja akaniambia ana ujauzito wangu hivi anataka nipeleke barua kwao kabla haijaonekana kwao na kujulikana rasmi kwao kwamba mjamzito.Kama ujuavyo sisi wanaume ni wabishi kukubali mizigo kirahisi kirahisi.Basi tukaendelea kugombana mpaka ikafika miezi 3.

Alivyoona kuwa ishu sasa imekua ngumu na mwanaume bado anaendelea kukomaa kwamba ujauzito sio wa kwake,akaamua kwenda ustawi wa jamii kushitaki kwamba nimempa mimba na nimeikataa kwamba hiyo mimba so ya kwangu wakati tulikua tunagegedana kwa muda upatao kama mwaka sasa,Baada ya siku mbili nikaona napigiwa simu na afisa ustawi wa jamii na kunutaka niende ofisini kwao nikajibu mashitaka hayo.kwasababu nilibanwa sana kazini nikaomba niende siku ya pili maana sikuwa na nafasi siku hiyo.Mungu sio Athumami kabla haijafika siku ya pili Nikapigiwa simu na mtu ambaye simjui na ninamba ngeni kwangu.

Kwanza kanipa pole kwa hiki kilicho nisibu,pia akaniambia kwamba huyu Binti in jeuli kwa sababu ananipakazia hiyo mimba kuwa ni ya kwangu wakati ni ya kwake,na kunihakikishia kuwa kesho yake atakwenda ustawi wa jamii ili kuona kesi iliyofunguliwa dhidi yangu.Kesho yake asubuh Binti wakahi ustawi wa jamii kama mshitaki tayari kwa kunisubili Mimi kama mshitakiwa.Baada ya nusu saa kabla ya mimi kutinga ustawi,nikapigiwa simu na yule afisa ustawi kwamba pale ofisini kwao pametokea tafrani baada ya Binti kumuona yuke mwenye mzigo wa halari anaingia pale baada ya Mimi mshitakiwa kukawa na vurugu kubwa mpaka binti ilitakiwa anywee kwa kile kwa kuto kuamini kile alichokiona pale ofisini,kumbe kilichofanyika Binti alikua na wanaume zaidi ya watatu na Mimi nikiwa wa nne ,na hao wote walikua wamemzidi umri tena kama babazake,kisa cha kunizingizia in kwamba alikua hana namna kwa sababu wale wanaume walikua wameoa na wanafamilia zao,hivi binti alikua hana namna zaidi ya kunizingizia mimi.

Basi Binti toka siku hiyo karidhika mpaka pale alipo jifungua na kumlea mtoto wake na sasa kashafikisha miaka 2 sasa.Kwakipindi hicho nilikua sina maisha mazuri sana kwasababu ndo kwanza nilikua nimeajiliwa kwenye taasisi mojahivi na maslahi yalikua madogo sana.Baada ya mwaka nikawa nimeondoka baada ya kupata kazi sehemu nyingine,nikiwa ofisini nikaona mtu anagonga mlango nikawa nimeitikia kwamba aingie, alipoingia nikaona Huyo Binti amekuja kuomba kazi kwa sababu tulikua tumetangaza kazi hapo ofisini kwetu.Alipoingia na kuniona Mimi yaani nusu azimie kwa hofu,lakini nilimsisitiza aongee nilichomleta pale ofisini,baada alinieleza kwamba maisha take ni magumu na anaomba kazi ili aweze kuendelea kumlea mwanae maana wale wore waliokua wanamgegeda kipindi akiwepo yule mzee aliyempa mimba wote wamekimbia.

Sasa je mdau unashauri nini ,na kama ungekua wewe kama bosi ungefanyaje?
 
Mpe kazi bhana..sisi ni binadamu tena ushamtumia ni vzr ukamwonea huruma!huwezi kujua kwa nn mwenyezi mungu kamlengesha kwako!
 
Ningemsaidia kupata kazi kama mtu mwingine yeyote ambaye angekuja ofisini.Yale yalipita na hakuna haja ya kuweka kinyongo.Ukimsaidia yeye utakuwa umemsaidia mwanae anayeteseka.Usimuangalie yeye muonee huruma huyo mtoto anayeteseka kutokana na maisha magumu ya mamayake
 
Kazi na mapenzi ya zamani hayagongani, kwani unataka aendeleee kugegedwa ndio ufurahi? Kama anasifa za kupata Kazi mpatie okoa maisha yake na ya mtoto.
 
kama huna kinyongo naye bora umsaidie aweze kupata kazi hapo
 
Cha ajabu wakati tungali tupo wapenzi,aliniaga kwamba anakwenda kwao kuwaona wazazi wake ,toka siku alipoanza safari hakupatikana kwenye simu ,baada ya wiki moja alilejea tena,na nilipomuuliza kulikoni mbona toka aondoke alikua hapatikani kwenye simu akanieleza simu yake ilikua mbovu,nilipomuomba anipe ili niipeleke kwa fundi akaniambia atanipa tukagombana sana na hakuweza kuleta ile simu,baadae niliamua kupuuzia na kumsamehe,nikamnunulia simu nyingine maisha yakaendelea,Kumbe inaonekana baada ya yeye kuondoka hakwenda kwao,akawa ameondoka na yule jibaba kisafari baada ya kuanza safari wakaanza kugombana na yule mzee akaamua kumnyang'anya simu kwa sababu wakati wakiwa njiani kuna mwanaume alimpigia na demu kashindwa kuongea kwavile yupo na mzee.
 
Is a True story aisee sio masiala mkuu.

Sijakataa kuhusu ukweli wa hadithi yako, nikichokataa ni ww kuhusika na recruitment kwny taasisi yenu, labda organization yenu iwe ni non-professional
 
Sasa unachojishauri ni nini? Mwanaume ni kusahau bro...
 
Inategemea aina ya kaz mkuu kuna baadhi huwa zinatangazwa
 
Kazi mpe tu mkuu. Uhasama wa nini bhana. Furaha yako ipo kwa watu. Ili uishi kwa furaha wafurahishe watu kwanza.


Somo; hiki ndicho kinafanya wanaume wengi kukataa ujauzito. Lakini wanawake huchukulia kama ni roho za unyama.
 
Back
Top Bottom