Naota mazingira haya mara kwa mara

Naota mazingira haya mara kwa mara

WABALLA Inc

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2014
Posts
2,711
Reaction score
1,018
Habari wakuu?

Naomba wanaojua tafsiri ya ndoto hii wanisaidie, maana nasikia ukiota ndoto inajirudiarudia inakuwa na maana fulani. Nimekuwa naota nipo shuleni mara nyingi shule ya msingi au sekondari.

Mara zote ndoto ninazoota (nikiwa mazingira ya shule) nakuwa mazingira /sehemu mbaya mfano ninaota sina viatu nipo na wenzangu sehemu kama chooni, wakati mwingine nimevaa mavazi yaliyochakaa.

Mara nyingine nipo sehemu za misitu, muda mwingine nipo kwenye mtihani maswali yananishinda kujibu. Sijui hii inaashiria na ni miaka zaidi ya kumi nimesoma sasa ni mtu mzima mwenye familia.
 
Habari Wakuu? Naomba wanaojua tafsiri ya ndoto hii wanisaidie, maana nasikia ukiota ndoto inajirudiarudia inakuwa na maana fulani.
Nimekuwa naota nipo shuleni mara nyingi shule ya msingi au sekondari. Mara zote ndoto ninazoota (nikiwa mazingira ya shule) nakuwa mazingira /sehemu mbaya mfano ninaota sina viatu nipo na wenzangu sehemu kama chooni, wakati mwingine nimevaa mavazi yaliyochakaa, mara nyingine nipo sehemu Za misitu, muda mwingine nipo kwenye mtihani maswali yananishinda kujibu.
Sijui hii inaashiria na ni miaka zaidi ya kumi nimesoma sasa ni mtu mzima mwenye familia.
Hiyo ndoto yakuota unafanya mtihan maswali yanakushinda pia ni ndoto ambayo huwa inajirudia sana kwangu..
Nasikia huwa ni roho za mizimu bt ngoja wajuzi waje
hizo ndoto zinaashiria kurudi nyuma kimaisha ,majanga manuksi ya hatare yaani wahini kama ni waumini safi pigeni maombi sana kama upo legelege wahini tu kwa wazee maana mtakuja kulia na kusaga meno sitanii
 
mkuu hizo ndoto zako zinaashiria bado kwenye maisha yako kuna sehemu unapitia magumu sana na pia unahitaji ukae chini uangalie wapi unakosea,pia kuna marafik zako ambayo umesoma nao wana maisha mazuri kupita wewe ingawa uliwazidi kwa vitu vingi kipindi hicho
usiogope hizo ndoto maana mungu bado anakukumbusha kuwa kuna sehemu unakosea namna ya utafutaji wa maisha yako
hizo ndoto zilinisumbua sana mkuu hadi pale mhubiri mw.christopha mwakasege alipoanza kuelezea maana ya ndoto za kusoma shule,hiyo hata kama umeshamaliza chuo hautaota mazingira ya chuo bali zitakupeleka shule ya msingi.
kwa kifupi unafeli sana kwenye ishu za kimaendeleo
 
Ndugu ningekuwa na mengi yakuongea nawe ila kwa ufupi, ndoto ni picha halisi ya maisha ya mtu yajayo, yaliyopo au past life . Kuna mambo uneyashindwa ambayo Ulitakiwa uyafanye but still you have a chance, Jambo la pili la kuota uko uchi kuna Jambo la aibu limejificha,either dhambi au laana
 
hizo ndoto zinaashiria kurudi nyuma kimaisha ,majanga manuksi ya hatare yaani wahini kama ni waumini safi pigeni maombi sana kama upo legelege wahini tu kwa wazee maana mtakuja kulia na kusaga meno sitanii
Una imani haba
 
mkuu hizo ndoto zako zinaashiria bado kwenye maisha yako kuna sehemu unapitia magumu sana na pia unahitaji ukae chini uangalie wapi unakosea,pia kuna marafik zako ambayo umesoma nao wana maisha mazuri kupita wewe ingawa uliwazidi kwa vitu vingi kipindi hicho
usiogope hizo ndoto maana mungu bado anakukumbusha kuwa kuna sehemu unakosea namna ya utafutaji wa maisha yako
hizo ndoto zilinisumbua sana mkuu hadi pale mhubiri mw.christopha mwakasege alipoanza kuelezea maana ya ndoto za kusoma shule,hiyo hata kama umeshamaliza chuo hautaota mazingira ya chuo bali zitakupeleka shule ya msingi.
kwa kifupi unafeli sana kwenye ishu za kimaendeleo
Yani shule ya msingi kila siku lazima niote niko class
 
Habari Wakuu? Naomba wanaojua tafsiri ya ndoto hii wanisaidie, maana nasikia ukiota ndoto inajirudiarudia inakuwa na maana fulani.
Nimekuwa naota nipo shuleni mara nyingi shule ya msingi au sekondari. Mara zote ndoto ninazoota (nikiwa mazingira ya shule) nakuwa mazingira /sehemu mbaya mfano ninaota sina viatu nipo na wenzangu sehemu kama chooni, wakati mwingine nimevaa mavazi yaliyochakaa, mara nyingine nipo sehemu Za misitu, muda mwingine nipo kwenye mtihani maswali yananishinda kujibu.
Sijui hii inaashiria na ni miaka zaidi ya kumi nimesoma sasa ni mtu mzima mwenye familia.
Bila shaka huwa unaota ndoto hizi mwili wako unapokuwa kwenye mazingira fulani ya stress. Kwa mfano mimi nikiwa na homa inayoninyemelea nitaanza kuota natembea kwenye kinyesi au maji machafu. Nikiota tu hivyo baada ya muda nitapata homa. Hata kuota unafanya mtihani maswali yanakushinda bado ni tafsiri ya mwili (ubongo) wako kupambana na mazingira fulani. Kwa kifupi achana na imani za kutafsiri ndoto kama waganga wa kienyeji wanavyodanganya
 
mkuu hizo ndoto zako zinaashiria bado kwenye maisha yako kuna sehemu unapitia magumu sana na pia unahitaji ukae chini uangalie wapi unakosea,pia kuna marafik zako ambayo umesoma nao wana maisha mazuri kupita wewe ingawa uliwazidi kwa vitu vingi kipindi hicho
usiogope hizo ndoto maana mungu bado anakukumbusha kuwa kuna sehemu unakosea namna ya utafutaji wa maisha yako
hizo ndoto zilinisumbua sana mkuu hadi pale mhubiri mw.christopha mwakasege alipoanza kuelezea maana ya ndoto za kusoma shule,hiyo hata kama umeshamaliza chuo hautaota mazingira ya chuo bali zitakupeleka shule ya msingi.
kwa kifupi unafeli sana kwenye ishu za kimaendeleo
Umeeleza vizuri sana mkuu.

Kuna link kweli ya haya mafundisho tuyatafute aisee, nina imani ni wengi sana humu wanaota hizi ndoto za kuwa shule na kufanya mitihani
 
Labda ina maanisha ukawasabah walimu ma wanafunzi wenzio wa shule ulosoma itakua umewasahau kitambo. Hasa mwalim ndo kila kitu usipende kumsahau kabisa
 
Habari Wakuu? Naomba wanaojua tafsiri ya ndoto hii wanisaidie, maana nasikia ukiota ndoto inajirudiarudia inakuwa na maana fulani.
Nimekuwa naota nipo shuleni mara nyingi shule ya msingi au sekondari. Mara zote ndoto ninazoota (nikiwa mazingira ya shule) nakuwa mazingira /sehemu mbaya mfano ninaota sina viatu nipo na wenzangu sehemu kama chooni, wakati mwingine nimevaa mavazi yaliyochakaa, mara nyingine nipo sehemu Za misitu, muda mwingine nipo kwenye mtihani maswali yananishinda kujibu.
Sijui hii inaashiria na ni miaka zaidi ya kumi nimesoma sasa ni mtu mzima mwenye familia.

Nimejitahidi kutafuta mafundisho kutoka kwa waalimu wazuri wa hili somo, kama Gwajima na Mwakasege, nimeweka links hapa chini.

Back
Top Bottom