Babu, mimi nilisema haya nikakumbushwa tena kwa sauti kubwa kabisa kuwa mtoto anaenda Feza, siyo shule tu ya uchochoroni. kule wanasoma watoto wa mabilionea kwa hiyo na mtoto wa
Kaunga naye anatakiwa kwenda kama milionea. Well, tupo tofauti. mimi siwezi kujiita ni wa level ya chini, lakini kila ninapompeleka mwanangu shule (boarding) huwa namwuliza matron minimum amount ya kumwachia mtoto as a pocket money, najua matron angeniambia
minimum ni 2M nisingeshindwa kutoa, lakini akiniambia ni elfu 20 huwa naacha elfu 20.
Huyu mtoto yupo shule..... atakula, atalala, ataingia darasani............. akiumwa atatibiwa ikishindikana nitapigiwa simu, kwa nini nimwachie laki? ataifanyia nini? si bora hiyo laki nimwekee kwa account yake ataikuta siku atakapoihitaji?
Pamoja na mzazi kumwelewa mtoto, kitu muhimu pia ni kukaa na mtoto wako na kumwelewesha. kama wazazi hatupaswi kudictate mambo, sawa, lakini tunapaswa kukaa na watoto na kuwaambia hali halisi. na huwa wanaelewa wala hawana shida