Naonekana sina shukrani hata sijui kosa langu

Ukishakuwa muafrika, kuna mapicha picha fulani lazima kwenye familia yawepo...

Shukuru Mungu kwenye familia yenu hamjaenda mbali kiasi cha kupigana misumari kwa masangoma...
 
Mshukuru sana brother kwa kukupa life experience, kaa nae mbali lakini usimuwekee kinyongo. Kunjua na ikitokea amepigika mpe tafu.
Ni kweli kabisa uliyoyasema na hata alivyoenda msibani ulifanya jambo la maana sana
7bu kama asingetokea msibani ndio angezidi kupata ubaya zaidi na wangeoata la kusema

Tukirudi kwenye COMMENT yako ni kweli kabisa kuna wakat mtu anakufanyia ubaya akiamini anakukomoa kumbe ndio anakujenga kiakili zaidi
huyo SHEMEJI yake ni dizaini ya watu ambao hakuwa amekupenda tangu awali
sasa chuki yake ndio imekufikisha hapo ulipo

hao ndugu wasikuumize kichwa tafuta ela zaidi ukiwa na pesa wote watakuona unafaa
unajua kwann wanamsikiza huyo bro wako
7bu ana pesa so nawewe tafuta zaidi

wewe huyo bro achana naye ila HESHIMA iwepo popote ukimkuta usichoke kumsalimu
zaidi Rudisha fadhila kwa watoto wake
jitahidi kila njia kuwa karibu na watoto wake hao ndio watamueleza ukweli baba yao na ndugu wengne

muhimu komaa na biashara zako
na biashar zitafanikiwa zaidi sababu umerithi urithi halali kabisa wa babayako
naamini MWENYEZIMUNGU atakusimamia zaidi
 
Ushauri wangu ni kaaa mbali na familia ya kaka yako .

Narudi Tena kata mguu kabisa usiende uko .
 
Mkuu kwanza ziba masikio halafu move on yaani usimsikilize mtu yoyote awe brother awe mke wake awe shangazi wala baba wakubwa pambania maisha yako pia jifunze kutokuteleza na kurudia makosa lawama huwa zipo tu aisee wala siyo big deal sana
 
Pole sana Mkuu,Kila jambo ktk maisha Lina Sababu zake,haijalishi ni mbaya au ni nzuri.Mwombe MUNGU atakujalia mema yote Ktk maisha yako.
 
Tunaweza tukawa tunafanana kwa matukio japo lako ni tofauti kidogo. Nikwambie tu mkuu swala la ndugu kukuchukia usijali kabisa mjini sikuizi tunaishi na marafiki ambao tunasaidiana kuliko ndugu.

Pambana na kazi, kuwa mwaminifu kwenye pesa, jenga connection na watu potential alafu jitaidi sana ndugu zako wasiwe na taarifa zako na wewe usiwe na taarifa zao utafurahia maisha. Taarifa pekee ya kuwaunganisha iwe ni msiba au sherehe kama wamekualika .
Kwasababu haijawahi kukutokea au hujawahi ona watu wakipatwa na taabu za namna hiyo.Hii dunia iache km ilivyo.
 
Ndugu yako wa kweli ni mtoto wako tu. Wengine hata uwafanyie nini katika maisha yao ukitegemea upate wema utapata shida tu. You are a real gentleman mkuu, pambana na utatoboa kwa uwezo wa Muumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha haya yaache tu, mama yetu alifariki tukiwa wadogo tulizaliwa watatu, mimi na wadogo zangu wawili wa kike, baada mama kufariki baba alitulea mwenyew kiubishi japo kwa mzee pesa ya kula ilikua haisumbui.

Nilipomaliza darasa la saba akaja kunichukua kaka yangu mtoto wa mjomba tumbo moja na mama angu kuja mjini Arusha kunisomesha huyu brother kiasi flani kakulia kwenye familiar yetu mjomba alimpa mama aishi nae soon to baada ya mama kuolewa.

Nikafaulu kwenda secondary shule za serikali brother akawa anachangia kiasi na mzee akawa nae anachangia kias ili maisha yasonge shuleni, nikiwa naenda kwa brother likizo kwenda tuition nikirudi shule alikua akinipa ada ile ya muhula wa kwanza na uniform pesa ya matumizi kwa nikiwa shule alikua akinipa mzee.

Nikamaliza fm4 nikafaulu kwenda shule ya serikali pia iliyopo uko manyara wakati matokeo yanatoka nilikua nipo kwa brother Arusha. Wakati najiandaa kwenda A level maneno yakaanza kutoka kwa mke wa brother kwamba gharama ni kubwa za kwenda shule hivyo brother mwenyew hatoweza labda asaidiane na mzee.

Ukweli brother yuko vizuri kiuchumi watoto wake walikua wanasoma shule za private ada kuanzia m2 ivi Mimi ada na mahitaji mengine ilikua haizidi laki mbili hivyo ikanilazimu niende kijijin kwa mzee kama anaweza kunitoa chochote mzee akanipa kama laki moja ivi brother akasema atajazia kilichopungua.

Maisha yakawa yanasonga uku nipo A level na madogo nao wanapanda uku chini nao akawa anawapiga kampani ivo ivo, balaa likaja baada ya mzee kufariki nikiwa nipo mwishoni kumaliza A level mambo yakazidi kuharibika

Nikamaliza form6 vzr matokeo yakatok yapo vzr application za chuo zikaanza nikapata chuo dar, kimbembe kikaja kwenye pesa ya usajili mke wa brother akanambia brother hana pesa ya kunilipia kufanya registration apo hatujajua kama mkopo ntapata au vipi.

Nikaenda kijijin nikapigapiga mishe kwenye mali za mzee nikapata pesa kiasi, nikaja mjini na pesa kiasi brother akanambia ataongezea kilichobakia ila nikipata mkopo nirudishe pesa yake nikakubali bahati nzuri nikapata 90% brother akawa ananipigia kila wakt kuhusu pesa yake boom lilivoingia tu nikakata zaid ya nusu nikampa pesa yake,kwa vile hostel nilishalipa na registration nishafanya na ada ile10% ilikua nilishalipa ikawa sio shida

Kila likizo nikiwa narudi zangu Arusha kwa brother kumsaidia shughul zake za hapa na pale na kijijini nikawa naenda kuangalia angalia vitu visiharibike

Nikija likizo nilichokua naambulia kwa brother ni nauli tu ya kunirusha chuo na nikipata boom ndo linaniendesha na wakati mwingine anakuuliza umepata pesa ukimwambia ndio atakwambia niazime laki apo au laki na nusu mzee hata kama mambo ni magumu inabid umtumie lakini sio kwamba alikua na shida nayo saana sema basi tu ikabidi nikomae boom likiisha ukimwambia brother nimepigika naomba ata 20 elfu atakutumia na kukusema oooh wew unatumia pesa vibaya, Basi shule ikaisha

Baada ya chuo ajira mtaani kukawa hakuna nikawa naishi pale nyumbani kwake namsaidia kucmamia biashara zake za hapa na pale maneno yakaanza oooh nakaa tu nyumbn nanenepeana nyumbani kwa mwanaume mwenzangu kwann nictoke nikapambane kivyangu na kibaya zaidi maneno hayo yanatoka kwa shemeji angu mke wa brother .

Basi nikaone isiwe tabu siku hiyo nikaongea na brother nikamwambia nia yangu ya kutaka kuhama kwake kwenda kuishi geto na sikumwambia sababu ya kutaka kuhama kwake, brother alinimind sana akanitukana saana eti unahama ukaishi geto kwan nyumbn umekosa nini nikarib kumuwek sawa kikiwa kimbembe kwel nikaona hili balaa wakati huo nikiwa nyumbani kwa brother ukinunua surual mpya tu au shati jipya shem anakasirika.

Nakumbk nilinunua smartphone kwa mara ya kwanza ya laki na nusu nikakalishwa kikao eti pesa nimepata wapi wakati kazi cna na apo nimemaliza chuo, wakati huo pia pale ndani nipo na wale wadogo zangu wawili wa kike na tulikua haturuhusiwi kukaa pamoja tuongee eti tunawateta

Baasi baada ya mbilinge mbilinge na kuona nmechoka pale ndani nikamuaga brother nataka niende kule kijijini Kuna mashamba ya mzee nikayaangalie akakubali nikaenda kijijini nikakaa kama mwezi ivi kurudi pale nyumbani kwake naona mzigo akawa ananipigia simu kila siku nirudi Arusha moyo ukawa hautaki nikajiona nipo safe kule home,

Pale kijijini Kuna kibiashara mzee alikua anafanya na rafiki ake baada mzee kufariki yule rafiki yk mzee akawa anaendesha biashara peke yake nikiwa namsaidia kidogo nikamwambia anaonaje anipe sehemu ya mzee nikakomae kivyangu akanambia hamna shida ila akasema nimpe miezi 6 nikiona isiwe tabu, nikarud zangu mjini nyumbani tena kwa brother apo miaka miwili ishakata tangu nimalize chuo, nikawa naishi pale nyumbani lakin nikawa nimepanga chumba kwa Siri nikanunua kitanda godoro na vitu vingine vingn, mchana nikiwa sina kazi naenda kutulia geto kwangu ucku nalala nyumbani.

Maisha nikayaona yakazidi kua magumu brother nikaona km kwenye biashara zake akawa anaaza kunikwepa vijana wanaosimamia zile kazi wakaanza kuleta dharau kwangu kuchunguza kwa makini brother kumbe amewaambia nisishike chochote pale kazini kama nikitaka kumuuzia mtu bidhaa sharti kijana awepo na pesa nisikae nazo au nisishike pesa zake

Kuna Dada mmoja anafanya kazi ofisi moja na brother cku hyo akaniita nikaenda kwake akanambia nitoke nifanye niwezavyo nitoke kwa brother akanipa na Siri nyingi brother anazomwambia kuhusu Mimi yule Dada akaniomba in any how nicmtaje kama kanambia chochote niliumia saana ukizingatia Kuna biashara zake nyingine nimezisimamisha Mimi kwa jasho na aliniahidi yeye atoe pesa Mimi nitoe muda na usimamizi ila tutagawana baada ya biashara kusimama vzr, kweli nikamwona mwamba kama anakua mkali ivi kwenye pesa zake mkienda msibani au kwenye sherehe anakuangalia utatoa kiasi gani nikaona hili balaa

Yule mzee kule kijijini akanambia pesa tulokubaliana anipe kwenye ila biashara ya mzee ipo tayari nikaona hii ndo nafasi yangu ya mwisho nikaenda tukaandikishana nikachukua mpunga kama 2.5m nikaingia zangu mjini kwa vile Nishapata experience kiasi na biashara apa mjini nikaenda kufungua biashara yangu moja inayofanana na ya brother na nikamuga na nikamwambia cwez tena kukaa kwake nashukuru kwa msaada wake jamaa hakukunjua nafsi nikavaa moyo wa chuma nikapiga moyo konde

Akawa anapeleleza nimepata wapi mtaji akaja kujua nimechukua sehemu ya mtaji wa mzee kwenye biashara ya mzee ndo apo balaa nikaanza jamaa akawaambia ndgu zangu upande wa baba yaani baba zangu wakubwa na wadogo na mashangazi zangu wote wakaniwashia moto hatari nikaitwa vikao vya familiar nirudishe ile pesa kwa yule partner wa mzee nikagoma nikapewa vitusho vya kila namna nikagoma kurudisha mzigo

Brother akanichukia mazima nikahama nyumbani kwake nikaendeleza mishe zangu, na kwake nikakata mguu tukikutana nikimsalimia haitiki Kuna kipindi alifiwa na mama ake mkwe hakunambia lkn kwa vile watoto wa yule mama tunafahamian nikasafr nao msibani brother kule msibani nimemsalia hajaitikia mke wake ndo kabisaa nimeenda nae kumzika mama ake ata usoni haniangalii

Ndgu woote wanaokuja nyumbn kwa brother pale wanaonifam wanaambiwa kuhusu ubaya wangu na kukosa shukrani kwangu nashukuru biashara inakua inajiendesha napata pesa ya kula na nimeanza ujenzi maisha yanasonga

Ila kinachoniumiza ni ubaya ninaotangazwa nao eti sina shukrani mtu kanisomesha kwake siendi na simsalimii potelea mbali
Changamoto mara nyingi huwa ni hawa viumbe wanaitwa wanawake. Wanawake wengi huwaga hawapendi maendeleo ya ndugu za mume wake. Mheshimu Sana bro wako tatizo kubwa ni shemeji yako
 
Ya walimwengu hautayaweza. Ziba masikio piga moyo konde pambana.

Hakuna ndugu anayependa kuona mafanikio ya mwingine.

Huyo we tupa kule na ukifanya kosa ukarudisha mahusiano kwake andika umefilisika rasmi kabisa.

Kaa nayo hii utakuja kuikumbuka.
 
Niliwachukua mmoja aliolewa send off nlifany mwnyew mahari nikachukua mwnyew mambo yanaenda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom