Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 529
- 909
Na Thadei Ole Mushi.
Nimeangalia Movement za Mh Lazaro Nyalandu zimenifurahisha na zinamfurahisha kila mtu. Kuna wanaozingalia Movement hizo kwa jicho la Kisamaria na kuna Sisi tunaozingalia kwa jicho la kipekee na la Kisiasa.
Niliwahi kusema hapa kuwa ndani ya CCM kuna wabunge wa aina Nyingi mojawapo ni hili kundi analotokea Nyalandu. Kundi la wabunge waliokuwa wanaaminika katika Serikali ya JK na kuteuliwa kuwa mawaziri.
Hawa wanarudi kwa style ya ajabu ni vigumu kuwatambua kurudi kwao kwenye "Power" kama hutajiongeza.
Lazma tukubaliane hawa hawana cha Kupoteza kwa sasa, hawana tofauti na mwanachi anayeweza kuvaa Bomu na kwenda kujilipua katikati ya watu.
Kwa vyovyote Vile Chama kinapaswa kutembea na Nyayo zao kuwaangalia vichochoro wanavyopitia. Kwa siku za karibuni Nyalandu kaanza kutafuta kura za 2020 hizi hazitafutii kule Singida kama tulivyozoea hizi anazitafutia ugenini.
ATAINUFAISHA UPINZANI.
Kama nilivyowaambia kwenye andiko Langu la jana kuwa Mbowe kuna uwezekano mkubwa wa kugombea Jimbo la Moshi mjini. Hii itatoa mwanya wa Kusajili mchezaji mwingine wa kugombea Arusha mjini kwa sababu Mh Lema atalazimika kwenda kugombea Hai.
Nafasi ya Arusha kama Chadema watachanga Karata zao vizuri Mh Nyalandu ndiye mtu Sahihi wa kumsimamisha pale. Kwa kazi aliyopiga Arusha kwa muda huu mfupi tu anaonekana kuwa ni mtu wa kipekee katika Siasa za Arusha. Huwa naamini kwenye Siasa Lolote Linawezekana.
Hii ndio nafasi Pekee ya Mh Nyalandu kurudi Bungeni Bila kutimia Nguvu Kubwa sana. Kama Mipango hii ikienda kama ninavyoiona mimi na kwa ulevi wa siasa za Upinzani ninaoujua mimi kwa kanda ya Kaskazini Nyalandu ana kazi Moja tu ya Kisimama Majukwaani Pale Arusha na Kusalimia wananchi na kuenda Kulala vijana wa Kulinda kura zake wapo wa Kutosha pale Arusha.
Lema akiingia Pale Hai hakuna wa Kumtoa ni mtu mwenye Siasa za Kushambulia "Agressive" kuliko Mbowe. Kama Mbowe alishinda Hai basi ni Raihisi sana kwa Lema kupita pale. Na Lema ataletwa maalum kuja Kupambana na Mkuu wa Wilaya anayeonekana kuwa naye Agressive.
Mbowe Kwa Manispaa ya Moshi anakuja kukamilisha Torati, huyu haendi kuomba kura kwa kuwa kwa CCM kwenye manispaa hii hakuna mtu aliyeandaliwa kuja Kugombea na hakuna mtu anayekaa na wananchi zaidi ya mtu kujitoa mhanga kama Devis Mosha kuja kugombea.....
Majimbo mengine yatabaki kama yalivyo isipokuwa jimbo la Mwanga linaweza kuathirika na mabadiliko haya kama nilivyodokeza jana.
Kosa kubwa walilolifanya Chadema 2015 mwanga ni ukawa Kutuma watu wawili pale mmoja aliitwa Msuya na Wa pili aliitwa Kileo. Hapa waligawanya kura zao wenyewe kama watarekebisha hili 2020 wanaweza kunufaika na mabadiliko niliyoyataja.
Kitu kingine kinachotajwa sana pale Mwanga ni Kileo kutokuwa mzawa wa Jimbo hili. Hivyo Chadema hapa wanapaswa kutafuta mtu ambaye ni mzawa anayetokea Tarafa aidha ya Ugweno au Usangi.
Nimetaja Tarafa hizi mbili kwa kuwa ni tarafa Kinzani kisiasa katika Jimbo hili. Kama wakifanya hivyo na wakiweza kutengeneza mapandikizi tarafa ya Maghembe basi watashinda jua likiwa linawaka.
NI KUJIDANGANYA KUSEMA CHADEMA INAKUFA.
CCM hatupaswi tena kujifungia Ofisini na kusema kuwa Chadema inakufa kwa kutumia tu maneno. Kufanya hivyo hakuna tofauti na mtu anayechoma Nyama kwa kutumia Mwanga wa Tochi haitakaa iive daima.
Takwimu zinatuambia Kuwa Chadema inakuwa kwa kasi kubwa sana kila baada ya Uchaguzi.
MWAKA1995 Chadema walipata Wabunge 4, madiwani 42.
Mwaka 2000, wakashinda wabunge 5 madiwani 75.
Mwaka 2005 wakapata Wabunge 11 madiwani 103.
Mwaka 2010 wakapata Wabunge 48, Madiwani. 467.
Mwaka 2015 wakapata wabunge 70 toka 48 waliopata uchaguzi wa 2010.
Unapata wapi Uthubutu wa kujifungia Chumbani na Laptop na kuandika Chadema inakufa? Huko wanakoelekea wanaenda kupasua Bunge katikati.
MAENEO MAPYA YANAYOWINDWA NA CHADEMA.
Rudia kauli ya Nape aliyoisema aliongea na Lisu kabla ya Shambulio lake.
"Alinimbia wewe ni mjomba wangu, kuna watu wanaonifuatilia na watu hao wanakufuatilia pia hamia Chadema huko CCM unafanya nini?"
Nape hakutuambia alimjibu nini ila Tabia za Nape siku za karibuni zinaonyesha kuwa ni Mbegu mpya ya Upinzani itakayooteshwa kipindi cha Masika kikifika.
Nape kwa Kila Dalili anaonekana atapeleka siasa za Upinzani maeneo ya Kusini huyu naye anatokea kwenye kundi la wabunge ambao hawana mahusiano mema na Serikali kutokana na Kutumbuliwa.
Si mtu sa kubeza kutokana na Ujasiri alionao anaweza kufanya chochote. Kazi kubwa waliyoanayo upinzani ni kuahakikisha Nape anakamilisha ahadi zake kwa wapiga kura. Kama akihamia Upinzani si chini ya majimbo sita na kuendelea ya Kusini yataathirika na kimbunga hicho.
Hapa ndipo tunaposema kuwa Siasa zetu zipo kwenye hatua ya kupata mabadiliko makubwa.
FITNA YA MWISHO YA NYALANDU HII HAPA.
Nyalandu kashajisogeza Nairobi ameenda kuongea na Lisu anatumia mwavuli wa Usingida.
Katika maandiko yake anadai kuwa Lisu anatakiwa akapatiwe matibabu zaidi ili afya yake iimarike zaidi. Zaidi ya hapo alitoa kauli tatanishi kuhusu kasi ya mwelekeo usio Sahihi kama ni mjuzi wa mambo unatakiwa uelewe hili kwa haraka.
Kama Nyalandu akifanikiwa kufanya kile alichokifanya kwa wanafunzi wa Lucky Vicent atakuwa kakonga nyoyo za kila mwanachama wa chadema. Akifanikiwa kumuunganisha Lisu na wale wajamaa basi atapaswa aje tu Arusha kupumzika kura atakuwa anazo za kutosha.
MAENEO MENGINE YATAKAYOWANUFAISHA CHADEMA.
Tafiti ya Mwisho ya Twaweza kuhusiana na maswala ya kisiasa nchini inataja Variable za Elimu na Umri kukinufaisha sana Chadema siku za usoni.
Kwenye utafiti ule unaonyesha asilimia 21 za watu wenye Elimu ya Juu kuiunga mkono chadema. Japokuwa CCM ina asilimia 46 ya kuungwa mkono na watu hao ila hali halisi ya maisha ya watanzania kwa sasa Kundi la wasomi linaongezeka mtaani bila ajira.
Mtu asiyekuwa na ajira huwezi kumshawishi awe mwanachama wa chama Tawala hata siku moja kwa hiyo kwa sasa vyuo vyetu vinapakua wanachama wapya wa Chadema kila Mwaka. Hawa ndio wapiaga Kampeni wakuu 2020 hifadhini maneno yangu.
Kundi hili kwa sasa linatawaliwa na Vijana kwa asilima Kubwa ndio hawa wanaojitokeza kwenye hizi interview za TRA na kuambulia Patupu hiyo ni sample tu huku mitaani wamejaa sana.....
Ole Mushi.