Naomi Mtoto wa Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomi Mtoto wa Arusha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chimunguru, Jul 13, 2011.

 1. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Naomi baby! Mitaa ya SEKEI Arachuga hiyo 1999 mwezi wa saba nilikuwa pande hizo. Nlikuwa kwenye ki shop cha cosmetics cha bro wangu! Naomi alikuwa anapita hapo kila asubuhi ananisalimia bila nyodo! akirudi ataingia shop ataangalia mafuta ya nywele! kuna jamaa alikuwa anamsalandia mara nyingi alikuwa akirudi toka town alikokuwa anapeleka maziwa huyo jamaa anaunga tela wananikuta shop wananipa hi wanaendelea zao, siku zikaenda tukazoeana zaidi akawa sasa anaweka kituo pale shop kila akipita kwenda town! story nyingi ilikuwa ni kumponda yule jamaa aliyekuwa anamfukuzia. mara nyingi huwa sina papara ya kuomba issue mapema naangalia kwanza hali ya hewa, nikaanza kupewa maziwa kidogo kidogo, akaanza kuja na rafiki yake ambaye bila kujua akaniita shemeji, Naomi alifadhaika maana sikumtongoza, nikajua njia ipo nyeupe nikaona km ki adventure flani hivi, nikachukua kalamu na notebook nikaandika lile tukio, siku ya pili asubuhi aliona aibu hakupita pale akanipungia tu nikaandika tukio kwenye notebook. Home kwao walikuwa wanambana bana sana ukichukulia alikuwa kamaliza form four, mama yake mzazi alikuwa anaishi Ngara mtoni, kule sekei akiishi na shangazi zake na wajomba zake. Kila nilipokuwa naandika documentary yangu nilianza na 'Naomi baby!'
  Jioni moja alipita kwa mbali nikamwita akaja nikamwambia vipi rafiki mbona umenisusa hupiti tena hapa, hakujibu kitu, nikamchomekea unajua unantesa sana kwa upweke, naomi pitapita basi angalau nikuone tuu na mie niridhike, akaniambia napenda kupita lkn watu wameenda kumwambia shangazi eti wewe unaniduu so shangazi kanikolomea, nikamwambia Naomi usipate shida ya kuteseka na kauli za watu kwani wewe hunipendi, akajibu kwa mahaaaba nakupenda tena nataka uje kwetu kwanza unitembelee, dah wadau i was more than happy, hiyo nayo nikaiweka kwenye notebook yangu.
  Jioni kama saa kumi nikaazima baiskeli ya jamaa nikapita sekei shuleni huyooo kwa kina Naomi, nikamtuma mtoto wa kike mdogo akaenda kumwita, tulipiga sana story baadaye niliporudi shop nika note down adventure yangu!

  Naomi was cute bana! mtoto wa kiarusha, kama ningekuwa na Kazi wakati ule nadhani mamsap angekuwa Naomi coz alikuwa tayari kwa kila kitu. Ndugu zake walipoona sasa mambo yanakuwa si siri tena, wakamrudisha kwa mama yake Ngaramtoni eti nikajitambulishe. Yeye aliniambia anakwenda kukaa wiki moja kwa mama yake halafu atarudi tena kumbe ndugu zake wahamwambia mama yake kwamba kuna kijana anakula mzigo bure, wiki ikapita Naomi kimyaa ya pili akaja akanimabia niende kwao Ngaramtoni nikajitambulishe angalau kwa mama yake tu anataka kuniona, mie ohoo niende huko kazi sina bado mwanafunzi, pale shop nilikuwa peke yangu nikamwambia ntajitahidi nije. Hii nayo ikawa noted down kwenye documentary yangu. zoezi la kwenda Ngaramtoni lika feli, Naomi akarudi tena town. Shangazi yake akawa na mpango wa kufungua saluni mitaa ya mount meru hotel pale Sekei barabarani, nikajua sasa ntapata mwanya mzuri wa kuwa na Naomi. Documentary yangu ilikuwa imesheheni vilivyo sifa kibao za Naomi na mipango tunayopanga, ingawa mie najua kabisa mmh hapa mtoto wa watu anapata hope anaolewa akiona shop kimejaa anajua maisha yatakuwa super, kumbe mwenzie nipo kwenye ki shop cha bro! hata shilingi sina pale hahahaha.

  Bro wangu akaja toka Dar ilikuwa tayari 2000 mwezi wa kwanza huo, nikawa nahitajika kwenda shule, nikamwambia naomi naenda Dar mara moja within a week ntarejea nafwata vipodozi, mtoto wala hakuwa na shaka, nikakwea basi nikarudi town. miezi ikapita Naomi kila siku anapita kwa bro anamuulizia mdogo wako yuko wapi, lini atarudi bro anamwambia yupo shule ntamwambia aje likizo. Niliondoka nikaacha documentary yangu pale shop, huku nyuma bro akaiona alipoisoma ilimwacha hoi vibaya mnoo! pasaka ya 2000 alinitumia kifurushi nikajua zawadi, ndani ya kile kifurushi kulikuwa na kadi ya pasaka kanitumia yeye bro kaambatanisha na kadi ya pasaka toka kwa Naomi na ile DOCUMENTARY yangu pamoja na barua bro kaniandikia eti kijana unajua kupenda lkn Naomi si yule tena unayemjua wewe! sasa hivi wana saluni tayari na watu wanajisevia tu so achana naye hakufai tena. Alimpa Naomi hiyo notebook akaisoma yote akamwambia bro nielekeze mnakaa pande zipi DAR niende, bro akaona hii soo maana huku DAR tena kuna Bro wangu mkubwa zaidi alikuwa ni no Nonsense man angemrudisha binti mlangoni.

  Sijajua Naomi yu wapi tena, kila nikienda Arusha nakuwa chini ya ulinzi wa shemeji yangu au mme mwenzangu, tehetehe sasa kisa cha kuyaandika haya yote nilikuwa napekua box la vitabu vyangu vya miaka mingi nimekuta cover tu la ile notebook na karatasi chache ambazo zilibaki plain hazikuandikwa kitu, na nilishaisahau km ipo bado otherwise ningeshaichana, Mh! nahisi yale mashairi mamsap aliyasoma na story ya Naomi nilishampa lkn doc sikumwambia km niliandika. tehetehe kweli ujana maji ya MOTO!
   
 2. D

  Derimto JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimeipenda unikumbusha mbali sana
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Mkuu,we ni mtunzi mzuri,nakushaur uungane na shigongo...
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu thanx hahahha lkn ni story ya kweli hiyo
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  mkeo anarudi lini? kama unazidiwa mfuate banaaa, manake kama unakumbushia hivi,ukikutana nae leo ubungo sijui itakuwaje!
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  aaah wapi bana mamsap wangu ndo kila kiiitu ni hadithi tu na si kijela kinanisumbua
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha na mie kipajicha nikifufue banaa!
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,658
  Trophy Points: 280
  Nice story!
   
 9. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,689
  Likes Received: 8,221
  Trophy Points: 280
  Nyc one...omba tu usikutane naye huyo Naomi!!!
   
 10. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dh! verynice sijui yukowap sahizi jamani! unanikumbusha mbali sana mkuu!
  Nilimpenda sana, ye ndo alikua dem wangyu wa kwanza, na me ndo nilikua man wake wa kwanza.
   
 11. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #11
  Jul 13, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  dah saafi saana mkuuu.....hii iko kama ya kwangu ila mm bado notebok na barua zipo asee wife anasomagaaa weeee anabaki kusema we ulikua kiwembe ww hahahaha
   
 12. Eshacky

  Eshacky JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 966
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Naomi! Hilo jina naliheshimu sana. Umenkumbusha mbal, n msichana wa kwanza kumpenda kupitiliza ktk maisha yangu, naomi mtoto wa arusha, ngabobo ngalemanyuki.
   
 13. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nice story nice fantasy and good flashback. ila it is best in fatansy. ukikutana nae leo certainly you will be disappointed. zile chichi saa sita hamna tena, ile adolescence complexion gone, wrinkles za maisha na frustrations zake are orders of the day, the charming smile has turned to frustrations za maisha, disappointed love and uchumi mgumu...if we were living in fatansy and flashbacks we would have living heaven in our lives. again nice great teenage love story
   
 14. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sekei kwa vifaa ndio kwake. Ukiibuka pande hizi, nidekeree nikupe ma intro ya kutosha. Utanikuta Big Y counter.
   
 15. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,406
  Trophy Points: 280
  watoto wa arusha noma mkuu...
   
 16. g

  gracious mosha New Member

  #16
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hiyo...Kaka wewe ni mwandishi mzuri kweli, nashauri ufanyie kazi kipaji hicho.......keep it up!!
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kaka unamfahamu KIJANAE? jina halisi anaitwa MOSSES almaarufu saaaana nitaa ile anatembelea mkongojo alikuwa dereva wa tours miaka hiyoo kabla ya kupigwa na ndugu zake?
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ahsante dada yangu, ntafanyia kazi ushauri wako!
   
 19. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kijanaa tuko naye sana Span view. Alianzisha mradi wa kufyetua matofali, jamaa wa halmashauri wakamfisadi pamoja na jamaa kua ni mlemavu flani.
   
 20. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Mzee umenikumbusha mbali sana, when i was in form 2, i loved a girl ,it was so real, you know how the first love look like, i remember one day when we were in a class b/k. the girl didnt make her hair in a way school need. mwalimu akamfukuza out of class, for sure nikajisikia vibaya sana na mimi nikatoka kwa hasira. Tulivyo kwenda likizo ya mid year she didnt come back, nikaja kujua kuwa alihamishiwa WERUWERU. it was so difficult to me. Bahati mbaya weruweru was girls only.
   
Loading...