Naombeni ushauri zaidi katika hili

Naombeni ushauri zaidi katika hili

Anaweza akawa analipia mkopo hajui kilicho baki kweli.

Apige hesabu muda anaotakiwa kumaliza mkopo agawanye kwa fedha anayotakiwa kurudisha. Alichopata atoe alichorejesha ata pata kilichobaki.

Mkuu balance walimwangalizia wao wenyewe kwenye system jamaa akona ipo ndani ya uwezo wake kulipa akaomba kulipa ndio akaambiwa aandike barua yakuomba balance makao makuu Ila mpaka muda huu wanamzungusha jamaa wanamwambia barua haijafika na huwa zinachelewa kufika hata miezi miwili inaweza chukua muda huoo
 
Kulingana na msoto jamaa anaosotea nimejifunza watumishi wakope taasisi zinazoeleweka sioo hizi za kimagumashi bora kwenda kwenye benki zetu kubwa na kongwe zinazoeleweka
 
Ntaleta mrejesho wakuu .

Kwa hivi sasa.

Wameandikiwa waraka wa siku 14 , wawe wamempa jamaa barua yake ya balance , baada ya siku hizo kupita wakiwa bado hawajatoa kesi inaanza mahakamani wakuu.
 
Ntaleta mrejesho wakuu .

Kwa hivi sasa.

Wameandikiwa waraka wa siku 14 , wawe wamempa jamaa barua yake ya balance , baada ya siku hizo kupita wakiwa bado hawajatoa kesi inaanza mahakamani wakuu.
Kila la kheri kwenu mkuu.
 
Habarini wakuu humu.

Naomba kuleta mrejesho wa mada hapo juu.

Jamaa yangu aliwapeleka mahakamani na baada ya amri mahakama alipewa barua yake ya balance ( salio bakia ) ili awalipe.

BancAbc wanatoa siku tatu ukishindwa kuwalipa ndani ya siku hizo unasubiri tena siku 90 zipite ndiooo uombe tena kulipa mkopo wako.

Jamaa akajitutumua akawalipa pesa yao kwa muda uliopangwa .
Na barua ya malipo ( risiti ) akawapelekea ofisini .

Sasa shida imekuja jamaa wamegoma kumpa barua yakuondolewa kwenye makato wanasubiri tarehe 15 ipite ili pay row iwe imeshatumwa ndiooo wampe barua yake yakuondolewa kwenye makato ya mkopo waooo.

Sasa ili apate barua yake mapema kabla ya tareh 15 hiyo anawaomba ushauri zaidi achukue hatua gani haki yake ipatikane mapema na ukizingatia hawa watoa huduma wa hii taasisi ni jeuri, kiburi na lugha za maudhi ( wanajisikia Sana) .
Ushauri wenu muhimu sana wakuu
 
wakuu jamaa aanzie wapi kulingana na post namba 26 hapo juu .

kuna mengi madudu juu ya hiii taasisi ntayafungulia uzi wake maalumu hawa BancABC ni zaidi yamajizi ni wakuogopwa kama ukomaa
 
Back
Top Bottom