Naombeni ushauri zaidi katika hili

Naombeni ushauri zaidi katika hili

k-star

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
541
Reaction score
392
Wakuu habarini.
Naomba niende moja kwa moja katika mada.

Kuna jamaa yangu miaka iliyopita alikopa mkopo katika taasisi ya BancABC sasa anataka kulipa deni lake lililobakia ( salio bakia ) au balance ili amalizane nao aendelee na mambo yake hapa mjini kama Kawaida.

Barua ya kuomba balance ameandika mwezi 6 mwanzoni na mpaka muda huu anazungushwa kupewa majibu yake ya salio bakia ili waweze malizana na taasisi hiyo ya mikopo.

Sasa imekuwa muda mrefu anaomba msaada achukue hatua gani ili aweze pata haki yake mapema maana coordinator wa taasisi hiyooo kila akienda kufatilia anamzungusha anamwambia haijafika mpaka sasa hiyo barua yake na ukitizama ni mwezi mzima umefika tangu aombe balance yake.

Msaada wenu wakuu wakumsaidia Jamaa yetu unahitajika afanyaje kwa muda huu .
 
atafute hela tu akuna namna tumechoka kutoa ushauri (in magufuli's voice)
natania tuu
Pesa IPO mkuu ndioo maana jamaa anataka walipa ili aondolewe kwenye makato ya BancABC.

Ahsante kwa mchango wako pia.
 
Wabobezi wa mambo karibuni mtiririke na kuserereka jamaa yetu akaanzie wapi apate hitaji lake mapema na muda muafaka .

Wengine piaaa watajifunza kupitia michango yenu
 
Mimi naona kama wanamzungusha,awaambie kuwa atawashtaki BOT.
 
Sehemu nzuri yakuwashitaki ni ipi kati ya hizi.

1: Afisa Utumishi.

2: Mahakamani.

3: TAKUKURU
 
Lengo lake ni kulipa ili aondolewe kwenye makato mkuu.

Rejea maelezo hapo juu kabisa
 
Pitieni na hapa wakuu tafadhali
 
Hapo nahis wanataka asilipe deni kwa wakati ili wauze dhamana, mwambie akomae nao ikiwezekana alale huko ofisini kabisa
 
Mkuu akhsante kwa mchango wako.
 
Namshauri aende makao makuu ya benki husika atapata msaada asiende kwenye branches zake kama itasumbua moja kwa moja ni BOT kwenye dawati la maridhiano watatandikwa barua ya kushughulikia swala lako asiogope
 
Sijawahi kuona mdai anayejizungusha unapotaka kumlipa deni lake. Lakini kwa benki wao wanataka profit zaidi ya kulipwa salio. Hapo inabidi umwambie yule mwanasheria aliyesaini mkataba wa mkopo awaandikie intention yako ya kulipa deni lote aweke na tarehe/mwezi unayotaka kulipa hilo salio.

Hapo wanakuwa hawana nguvu maana wakipelekwa mahakamani wanaweza kujikuta wanakulipa badala ya wewe kuwalipa.
 
Nashukuru kwa mchango wako muhimu sana.
 
Akhsante kwa mchango wako muhimu na wenye umuhimu.
 
Anaweza akawa analipia mkopo hajui kilicho baki kweli.

Apige hesabu muda anaotakiwa kumaliza mkopo agawanye kwa fedha anayotakiwa kurudisha. Alichopata atoe alichorejesha ata pata kilichobaki.
 
Back
Top Bottom