Naombeni ushauri wenu

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
814
1,545
Jamani njoeni hapa mnitie moyo, hii ni kawaida au vipi?

Mwenzenu nimehamia nyumba hapa Mwanza nina wiki 2. Shida yanguu sijawahi kuona wapangaji wenzangu ingawa wao wana kazi wanarudi jioni kwa maelezo ya mwenye nyumba, nyumba hii inatenganisha sisi wapangaji na mwenye nyumba kwa ukuta tuu.

Sasa hawa wapangaji jamani wanafua vizuri tuu na usafi ikifika zamu yao wanafanya. Wapo wawili kila mtu na chumba chake, mimi watatu naishi na wanangu wawili, wakifanya utundu sauti zinatoka ndani kuwakataza au kufoka.

Na kama unaenda bafuni kweli unaskia maji yanamwagwa mtu anaoga au anafua. Maji yanalia na mtu anaitika nipo kuoga lakini sijawahi kuwaona hata siku mojaaa. Yaaani nasikia sauti tu, wiki mbili kweli nisione hata mtu anaenda chooni kufuaa, anavorudi kazini, hakunaaa jamani kweli? Ni sauti tuu!

Mshana Jr nahitaji ushauri wako hapa.
 
Dah! kwahyo umekuja kutuanika mpaka huku? Sisi huwa tunakukwepa maana unaonekana ni mmbea sana na una nuksi...Sasa kumbe kazi bure tumefanya maana tayari umeshatuanika humu jf, Tanzania nzima itujue
 
Hata wao hawajawahi kukuona wewe,wanasikiaga sauti yako Tu,wanatamani sana kukuona ila ndo hivyo tena. Mwenye nyumba kawakomesha,hakuna kuonana.
 
Jamani njoeni hapa mnitie moyo, hii ni kawaida au vipi?

Mwenzenu nimehamia nyumba hapa Mwanza nina wiki 2. Shida yanguu sijawahi kuona wapangaji wenzangu ingawa wao wana kazi wanarudi jioni kwa maelezo ya mwenye nyumba, nyumba hii inatenganisha sisi wapangaji na mwenye nyumba kwa ukuta tuu.

Sasa hawa wapangaji jamani wanafua vizuri tuu na usafi ikifika zamu yao wanafanya. Wapo wawili kila mtu na chumba chake, mimi watatu naishi na wanangu wawili, wakifanya utundu sauti zinatoka ndani kuwakataza au kufoka.

Na kama unaenda bafuni kweli unaskia maji yanamwagwa mtu anaoga au anafua. Maji yanalia na mtu anaitika nipo kuoga lakini sijawahi kuwaona hata siku mojaaa. Yaaani nasikia sauti tu, wiki mbili kweli nisione hata mtu anaenda chooni kufuaa, anavorudi kazini, hakunaaa jamani kweli? Ni sauti tuu!

Mshana Jr nahitaji ushauri wako hapa.
Kuna tatizo hapa sio bure.. Kama ni wiki moja inazungumzika kwakuwa watu wanakuwa makazini lakini vipi weekend? Sijawahi kukutana na kisa cha namna hii
 
Back
Top Bottom