Samahani wapendwa, mwenzenu nimechanganyikiwa naombeni ushauri wenu. nilianza kupata maumivu kidogo tumboni sehemu ya uzazi nikaenda kupima hospitalini ni kaambiwa kila kitu kipo sawa ila ni mirija ya uzazi imezibana imeziba karibia na kizazi kabisa. nimerudi leo tena kuonana na Daktari ambaye niliambiwa atanisaidia nimemuona na ameniambia hakuna njia nyingine zaidi ya kupandikiza. Ndugu zangu kupandikiza ni million 12 hadi 15 kiukweli hizo pesa sina. naomba yoyote anayejua njia nyingine ya kuweza kunisaidia na mimi niweze kupata ujauzito. lakini mwaka juzi nilipata ujauzito ila ulitoka ukiwa na miezi 3 na nilisafishwa vizuri nina imani. naombeni ushauri wenu nimechanganyikiwa leo hata kama ni dawa za kienyeji niko tayari.
asanteni natumaini nitashauriwa vema.
asanteni natumaini nitashauriwa vema.