Naombeni ushauri wanaJF? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni ushauri wanaJF?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mdau Mkuu, Oct 21, 2010.

 1. Mdau Mkuu

  Mdau Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Heshima nyingi nawapeni Wadau wangu,nashukuru maana ndani ya Jamvi hili nimepata kuelimika kwa mengi,na napenda kuwapa hongera kwa kuendelea kulisongesha gurudumu,kwa leo napenda wadau mnipe ushauri kwa Dadangu ambaye tokea mwaka 1998 hajawahi kuumwa wala ku2mia dawa ya malaria,ila tokea kipindi hicho huwa anakunywa dawa ya mwarobaini(anachemsha majani afu anakunywa lita 1 kila mwezi) na kweli haumwi kabisa,ila me ningependa kujua hakuna -ve effects,kwa ku2mia kinga hii,na kama ipo ni ipi maana hajazaa huyu dadangu isijekuua kizazi!afu kama kunakinga ingine mbadala ya Malaria naomba mnijulishe wadau wangu,ntashukuru sana wadau kwa ushauri wenu!
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  kama anakuwa anakunywa hayo majani ya Mti wa Muarubaini kwa mwezi mara moja haina madhara yoyote ile mwilini mwake. Kwa sababu huwa anatumia huo mti majani yake kama ni kinga ya hayo maradhi, inakuwa ni vizuri isiwe kuwa anakunywa kila siku hapo huenda

  ikamletea matatizo mengine kwani ushauri wangu mtu huwa anatakiwa kuwa anakunywa Dawa mpaka awe ni Mgonjwa lakini kwa jinsi anavyotumia huo muarubaini kwa mwezi mara moja hautamletea madhara yoyote yale. Ushauri wangu mwengine mwambie Dada yako

  awe anakunywa Maji ya Uvuguvugu kiasi cha Glasi moja kila siku Asubuhi anapo amka kabla hajala kitu hii itamsaidia kuondosha Mafuta ndani ya Figo,na kufanya Apate haja kubwa kiurahisi. Na Kitu

  kingine awe anakunywa kijiko kimoja cha Asali mbichi isiyopikwa kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kijiko kimoja cha hiyo Asali mbichi na wakati wa usiku anapokwenda kulala hiyo pia itamsaidia kusafisha ini na figo. Huo ndio ushauri wangu
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kama nimekuelewa vizuri Mkuu mdau nadhani hakuna shida kihivyo, me sio mtaalamu wa dawa lakini hili la kunywa dawa bila kuumwa ni la kwaida kwani linatumika kama kinga. Hata mimi utotoni nilikuwa nikipewa dawa na mamangu hata kama nilikuwa siumwi. Wala usitie shaka!
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  ni kinga nzurim ila mwarobaini unatoa mimba hivyo kama ana ndoa ama akiolewa mshauri asitumie,its serious mwarobaini unatoa mimba
   
 5. Mdau Mkuu

  Mdau Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Namishukuru sana wadau,hakika ntayafanyia kazi mambo yote mlionishauri,Mungu amibariki sana wadau wote
   
Loading...