Wadau Naombeni Ushauri jamani: Ninayopitia siyo haba

Kigorohe

Senior Member
May 21, 2019
160
253
Habari zenu wana JF

Napenda kumshukuru kwa kunijalia uzima mpaka leo napumua. Najua siyo mara ya kwanza kuona nyuzi zangu kwana hata siku zilizopita niliandika nyuzi kadhaa zilizokuwa nikiomba msaada ila sikufanikiwa kupata. Lakini nashukuru Mungu japo nyuzi zote zilifutwa ila niachane na hayo!

Baada ya kuona hali ya maisha inakuwa ngumu niliamua kufanya juu chini kupata nauli ya kunileta Mwanza na hili nilifanikiwa kwa kuuza maja ya vitu vyangu vya ndani. Niliuza TV yangu kwa Tsh 120000 hivyo nipata nauli ya kunifisha Mwanza. Kabla ya hapo kweli kulikuwa na ndugu yangu hala Mwanza ambaye mwanzo aliniambia nije anipe mchongo wa kiabishara. Kweli jamaa ni mjasiriamali mzuri tu hivyo maisha yake siyo haba kivile.

Niliamua kumuweka wazi kuwa mimi kwa sasa hata mtaji wenyewe sina lakini nilimwambia wazo langu la biashara akanimbia we njoo usijali nitakupa mtaji hivyo usiwe na hofu. Baada ya kusikia hivyo kweli nilianza kusaka nauli kwa udi na uvumba ili nije Mwanza. Na Mungu siyo Athuman kweli nilipata hiyo 120k kwa kuuza mali yangu. Nilitumia nauli na ikabaki 85k.

Sasa baada ya kufika niliongea na huyo ndugu yangu siku ya kwanza akasema tuona cha kufanya hapo ilikuwa J4. Tumeendelea kukaa jamaa naona sasa hasomeki kabisa kuhusiana na michongo hiyo ila yeye kila siku anaamka anaenda kwenye mishe zake ananiacha mie nikiwa nimelala. Akirudi unakuta anaesabu pesa zake mbele yangu mie navunga kama sioni mara ananiruma vitu vya ajabu ajabu kweli ni hatari sana.

Baada ya kuona hata pesa niliyokuja nayo naendelea kuitumia kwa kasi kwa chai na chakula cha mchana huwa najitegea usiku ndo tunakula gheto lakini. Kwa ufupi nilivyo msoma jamaa anataka nikaye hapa kwake kazi yangu iwe ni kumfulia kupika kuosha vyombo na kufanya usafi wa ndani afu malipo n chakula tu. Kweli inauma sana mtu kukuita akaharibu pesa yako, umekaa kwenye basi zaidi saa 13 lakini mtu anataka tu akuoneshe yeye kafanikiwa hivyo ana uwezo wa kukurisha afu ndugu yako.

Wadau inaniuma sana najuta kuja ila hapa kweli nimebakiza 62k wadau nimeenda baadhi mialo hapa Mwanza kama mswahili, Bwiru, na mingine kuangalia harakati hata za uvuvi imeshindika. Naomba ushauri wenu nifanye biasha gani kwa mtaji huo niliobakiza wa Tsh 62k kulala nitalala hata vibarazani ili mwanamme ni kujitesa mpaka ufanikiwe.

Karibuni kwa ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Choma mahindi
Zungusha maji ya kunywa. Zungusha mayai,Karanga na mapochopocho mengine.
Ikifika mwezi wa tano nenda kwenye machimbo ya dhahabu Geita,Shinyanga au Chunya.

Pambana mpaka pumzi ya mwisho. Watu wenye dharau kama huyo ndugu yako(kama ulivyosema) wanabidi wawe sababu ya wewe kupambana kwa nguvu zote kuwathibitishia kwamba wewe ni mwamba.
 
Habari zenu wana JF

Napenda kumshukuru kwa kunijalia uzima mpaka leo napumua. Najua siyo mara ya kwanza kuona nyuzi zangu kwana hata siku zilizopita niliandika nyuzi kadhaa zilizokuwa nikiomba msaada ila sikufanikiwa kupata. Lakini nashukuru Mungu japo nyuzi zote zilifutwa ila niachane na hayo!

Baada ya kuona hali ya maisha inakuwa ngumu niliamua kufanya juu chini kupata nauli ya kunileta Mwanza na hili nilifanikiwa kwa kuuza maja ya vitu vyangu vya ndani. Niliuza TV yangu kwa Tsh 120000 hivyo nipata nauli ya kunifisha Mwanza. Kabla ya hapo kweli kulikuwa na ndugu yangu hala Mwanza ambaye mwanzo aliniambia nije anipe mchongo wa kiabishara. Kweli jamaa ni mjasiriamali mzuri tu hivyo maisha yake siyo haba kivile.

Niliamua kumuweka wazi kuwa mimi kwa sasa hata mtaji wenyewe sina lakini nilimwambia wazo langu la biashara akanimbia we njoo usijali nitakupa mtaji hivyo usiwe na hofu. Baada ya kusikia hivyo kweli nilianza kusaka nauli kwa udi na uvumba ili nije Mwanza. Na Mungu siyo Athuman kweli nilipata hiyo 120k kwa kuuza mali yangu. Nilitumia nauli na ikabaki 85k.

Sasa baada ya kufika niliongea na huyo ndugu yangu siku ya kwanza akasema tuona cha kufanya hapo ilikuwa J4. Tumeendelea kukaa jamaa naona sasa hasomeki kabisa kuhusiana na michongo hiyo ila yeye kila siku anaamka anaenda kwenye mishe zake ananiacha mie nikiwa nimelala. Akirudi unakuta anaesabu pesa zake mbele yangu mie navunga kama sioni mara ananiruma vitu vya ajabu ajabu kweli ni hatari sana.

Baada ya kuona hata pesa niliyokuja nayo naendelea kuitumia kwa kasi kwa chai na chakula cha mchana huwa najitegea usiku ndo tunakula gheto lakini. Kwa ufupi nilivyo msoma jamaa anataka nikaye hapa kwake kazi yangu iwe ni kumfulia kupika kuosha vyombo na kufanya usafi wa ndani afu malipo n chakula tu. Kweli inauma sana mtu kukuita akaharibu pesa yako, umekaa kwenye basi zaidi saa 13 lakini mtu anataka tu akuoneshe yeye kafanikiwa hivyo ana uwezo wa kukurisha afu ndugu yako.

Wadau inaniuma sana najuta kuja ila hapa kweli nimebakiza 62k wadau nimeenda baadhi mialo hapa Mwanza kama mswahili, Bwiru, na mingine kuangalia harakati hata za uvuvi imeshindika. Naomba ushauri wenu nifanye biasha gani kwa mtaji huo niliobakiza wa Tsh 62k kulala nitalala hata vibarazani ili mwanamme ni kujitesa mpaka ufanikiwe.

Karibuni kwa ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna historia inaandaliwa kwaajili yako. Huyo ndugu yako sio kuungwana kabisa, bora angekuacha uteseke ukiwa kwako kuliko kukuringishia.
 
Kuna vitu haukuelewana na ndugu yako huyo ingependeza kama mngemalizana uko. Kama uliuza tu TV kwa 120K rudi kauze na vingine vilivyobakia geto upate mtaji ambao hujui utaufanyia nini kwa sasa nashauri utulie kwanza yaani tafuta mishe ya kukufanya upate buku 2 au tatu Tu kwa siku ama upate sehemu ukae kwa nduguyo usaidie majukumu kwa malipo ya chakula huku ukisoma mishe za eneo husika kama vile saidia fundi nk.

Huwezi kupata mishe za mtaani mapema unavyozani kwanza lazima uanze kutengeneza marafiki na watu wa eneo husika hasa nyumba 3-5 za majirani + kijiweni unaenda unakaa na washkaji siku 3-5 ndio unaanza kupata connection ndogo ndogo huku unamwomba Mungu afungue njia.

Ondoa mindset kuwa jf ndio kuna watu wa kukusaidia pekee hapo ulipo ni njia pia kufika unakotaka tatu usifikirie kuanzia juu sijui mtaji muhimu fikiria chakula na malazi ukifanimiwa mengine yatakuja usijifunge na kukomaa kuandika nyuzi za matatizo mpaka invisible wanazifuta. Ikiwezekana uza na smartphone unanunua simu ndogo ama unabaki na line Tu. Uzuri huna mke wala mtoto uliemwacha geto maisha yako very randomly unaweza kuwa unamlaumu ndugu yako ndio kakuletea ugumu kumbe alikuepusha kifo labda ungevaamiwa na vibaaka na kuuwawa kule ulikokuwa.
 
Back
Top Bottom