Naombeni ushauri wa namna ya kukuza ufaulu wangu

Nov 11, 2019
3
4
Ndugu zangu naomba msaada na ushauri wenu katika hili,

Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology. Napenda sana kusoma maana maisha yangu yanategemea sana elimu. Lengo ni kuwa na ufaulu wa juu sana lakini kila nikijitahidi kusoma naishi GPA 3.5. Natamani sana kupata GPA 4.5 mpaka 4.8.

Wapendwa naomba mnishauri nitumie mbinu zipi ili niweze kupata ufaulu kama huo?
 
Zingatia haya:
1. Jiweke ww wa kwanza hasa katika masomo inaama unatakiwa kujifikiria ww kabla ya mtu mwingine
2. Hakikisha unasoma topic/somo/swali zaidi ya mara moja, kwanza ukiwa kwenye kipindi pili ukiwa ww mwenyewe na tatu kwenye group discussion. Itakusaidia kujua vitu vingi na kukumbuka
3. Jaribu kuweka masoma kwenye vitendo hasa ww unasoma computer fanya kwa vitendo kama n programming au web design, ubongo ni rahisi kukumbuka kitu ulichofanya
4. Tumia group discussion kama sehemu ya kwenda present vitu ulivyosoma na kujazia vitu ambavyo haujasoma, usiende kama hauna kitu cha kuchangia au hujui mnaenda kujadili nn, kama ni maswali solve yote kwanza hata kama yatakushinda ila tafuta njia zake kwanza kabla ya disc.
5. Usiwe follower kwenye discussion, tafuta group ambalo ww utakuwa leader itasaidia ku present mawazo yako na kusikiliza mawazo ya wengine na itakujengea base ya kuwa na watu utakao wafundisha
6. Punguza vitu ambavyo haviusiani na masomo, at 75% iwe ni masoma hiyo ndo price ya GPA kubwa
 
hiyo GPA kubwa ya nin ww?? ukimaliza utakuja kujua mGPA mkuubwa hauna maana yyte hasa kwenye fani yako hiyo...
 
hiyo GPA kubwa ya nin ww?? ukimaliza utakuja kujua mGPA mkuubwa hauna maana yyte hasa kwenye fani yako hiyo...

Nyinyi ndio watu ambao hua mnawapoteza wenzenu kwa kuwaambia GPA kubwa haina maana. Hakuna kozi yoyote ile ambayo kufaulu hakuna maana. Kama wewe ulifeli na sasa maisha yamekunyookea, usifikiri kila mtu atakua na bahati kama yakwako. Acha watu wanaotaka kusoma wasome na wafaulu huwezi kujua GPA hiyo kubwa itakuja kumbeba wapi.
 
Asikudanganye mtu GPA kubwa zinaumuhimu wake.... Sikuhizi unashangaa kazi inatangazwa wanataka GPA ya 3.8 huko...... So mtoa mada jitahidi mno kubalance masomo yako pia upate muda wa kupumzika ili akili iwe stable muda wote...... Pia jitahidi solving na group discussion itakusaidia........ Nikiwa chuo nilianza na GPA ya 2.8 ila nilipambana hadi nikatoboa ya 4 kamili things sio rahisi ila stay focused muda wote
 
Back
Top Bottom