Naombeni Ushauri nimsaidiaje huyu DADA yangu.....????

Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,504
2,250
Wana Bodi Heshima mbele.....

Mimi nina Dada yangu upande Baba amemaliza chuo mwaka juzi kasoma kapata Shahada ya Uchumi,baada ya hapo akaja hapa DSM akaenda Ofisi flani kuomba kazi matokeo yake akaishia Kuolewa na Huyo Boss,kwanza taarifa za kuolewa zenyewe nilisikia kwenye Bomba tu.
Kilicho niuma zaidi ni hili suala la kuolewa KIUNI kwani yule Boss alienda huko mkoani Kufunga ndoa yeye na Sheikh na rafiki yake,wakafungishwa ndoa hapo nyumbani kwa Mama yake bila mimi kujua na ni mimi na kaka yangu ndo tulikuwa tunagharamia expenses zote za Chuo wakati anasoma lakini hatukupewa taarifa ya NDOA!wakafunga ndoa wakarudi mujini.
Kiukweli mi yule jamaa nilishajua ni muhuni tu kwani badae nilikuja kugundua ana Wake wengine WAWILI!Sasa kashampa mimba kajifungua now jamaa home atulii mara yupo nje akirudi hatulii home na majibu ya nyodo kwa wingi yaani kifupi ni kwamba hamjali tena!na sidhani kama hata Huduma muhimu anampatia mpaka sasa anaweza kusafiri hata mwezi na wala hata asimjulishe Mkewe mpaka wawasiliane na yule Sheikh wake ndo amtafute hewani waongee hivi ndo Ndoa zinakuwaga hivi kweli?

Naombeni ushauri wana jamvi Sister yangu NAMPENDA sana na sijui jinsi ya kumsaidia hajawahi kunipigia simu toka muda huo huwa anawasiliana na Baba.nahisi labda ananionea Aibu kwa mambo aliyofanya.NIFANYAJE wanajamvi?
 
ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
5,208
3,835
Kwanini usiliingilie kati suala hili kwa kukaa kitako na hao watu wote(dada yako,mume wake,sheikh,baba na mama wa dada yako) kwa pamoja mlizungumze hili?Nadhani hapo mtapata suluhisho la kudumu kama ndoa ivunjwe kila mtu aende kivyake au vinginevyo.
 
Nashindwa kufanya hivyo kwasababu hakuwahi kunishirikisha ila hayo malalamiko nayasikia kupitia kwa Baba na yeye hajawahi kunipigia simu toka kipindi hicho hata kwa kuniomba ushauri sasa nikiingilia si nitaulizwa nahusikaje hapo?
 
Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,504
2,250
Huyo dada yako amelalamika kuhusu mahusiano yake na mumewe? Chunguza hili maana mapenzi hayana adabu unaweza kuingilia halafu baadaye wewe ndo ukaja kuonekana mbaya. Chunguza vizuri kwanza!
Hayo matatizo alizungumza na Baba yake kama kumwambia tu kinachoendelea
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,508
Ungefungua mlango wa mawasiliano ungeweza kuelewa anahitaji msaada wa aina gani. Kama huna simu yake, muombe baba. Mpigie, muambie unahitaji kubond nae tena na kwamba unampenda. Kitu ninachoamini atafunguka kwako akuambie na utajua unamsaidiaje. Kwa matatizo ya ndoa, hata kumsikiliza tu ni tiba tosha. Ila usimuulize, muacje akuamini na kushare na wewe.

Familia ndo pa kukimbilia wakati umeharibu. Msamehe hata kabla hajarudi, msikilize, muonye na muonyeshe upendo. Hongera kwa kuthamini familia yako, mko wachache sana.
 
Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,712
1,245
Achana nae, wanawake saa zingine mpaka tuone na hivi tuko vijiweni wengi basi tutatolewa na mashetani. subiri akupe hizo habari mwenyewe, mpaka kumpigia baba yako nahisi nae alishiriki kwenye maamuzi hayo ya ndoa yake.

Kaa kimya mpaka akupigie simu yeye mwenyewe akwambie, vinginevyo mwache asikilizie utamu wa kujiuza kwa bei nafuu then atatia akili.
 
Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,519
1,082
Huyo dada yako amelalamika kuhusu mahusiano yake na mumewe? Chunguza hili maana mapenzi hayana adabu unaweza kuingilia halafu baadaye wewe ndo ukaja kuonekana mbaya. Chunguza vizuri kwanza!
Inawezekana dada yake karidhika na anaona sawa tu kuolewa na hata hao wanawake aliwajua kabla hajaolewa ndio maana hana tatizo sana na mumewe.
 
Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,519
1,082
Maliza kwanza matatizo na dada yako ndio uweze kutatua yanayomsumbua kama yapo.
 
SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
2,837
I would also say the same despite the fact that i have learnt something in between!
Thanks for this bonge la ushauri!

Ungefungua mlango wa mawasiliano ungeweza kuelewa anahitaji msaada wa aina gani. Kama huna simu yake, muombe baba. Mpigie, muambie unahitaji kubond nae tena na kwamba unampenda. Kitu ninachoamini atafunguka kwako akuambie na utajua unamsaidiaje. Kwa matatizo ya ndoa, hata kumsikiliza tu ni tiba tosha. Ila usimuulize, muacje akuamini na kushare na wewe.

Familia ndo pa kukimbilia wakati umeharibu. Msamehe hata kabla hajarudi, msikilize, muonye na muonyeshe upendo. Hongera kwa kuthamini familia yako, mko wachache sana.
 
Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,504
2,250
Ungefungua mlango wa mawasiliano ungeweza kuelewa anahitaji msaada wa aina gani. Kama huna simu yake, muombe baba. Mpigie, muambie unahitaji kubond nae tena na kwamba unampenda. Kitu ninachoamini atafunguka kwako akuambie na utajua unamsaidiaje. Kwa matatizo ya ndoa, hata kumsikiliza tu ni tiba tosha. Ila usimuulize, muacje akuamini na kushare na wewe.

Familia ndo pa kukimbilia wakati umeharibu. Msamehe hata kabla hajarudi, msikilize, muonye na muonyeshe upendo. Hongera kwa kuthamini familia yako, mko wachache sana.

Asante sana kwa ushauri wako nitaufanyia kazi pia
 
Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,504
2,250
Achana nae, wanawake saa zingine mpaka tuone na hivi tuko vijiweni wengi basi tutatolewa na mashetani. subiri akupe hizo habari mwenyewe, mpaka kumpigia baba yako nahisi nae alishiriki kwenye maamuzi hayo ya ndoa yake.

Kaa kimya mpaka akupigie simu yeye mwenyewe akwambie, vinginevyo mwache asikilizie utamu wa kujiuza kwa bei nafuu then atatia akili.

Unajua Baba aliitwa tu kwenye kufunga ndoa wala hakua anausika kihivyo na yeye ile hali aliiona toka mwanzo ila,Mama yake ndo aliyekuwa anafanya mambo kienyeji bila kuwashilikisha watu wengine hata Baba yake pia alikuja kuambiwa mambo yashakamilika ni ishu ilifanywa kisiri na ni Aibu ndo ilifanya wamuite Baba
 
Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,504
2,250
I would also say the same despite the fact that i have learnt something in between!
Thanks for this bonge la ushauri!

Mkuu unaweza pia kuniambia labda ni kitu gani hicho,naweza nikajifunza pia kikanisaidia.Asante
 
Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,504
2,250
Inawezekana dada yake karidhika na anaona sawa tu kuolewa na hata hao wanawake aliwajua kabla hajaolewa ndio maana hana tatizo sana na mumewe.

Sidhani kama kalizika coz asingeenda kulalamika kwa Mzazi wake,hilo la kumaliza matatizo nae nitalifanyia kazi,japo sijui kama nimewahi kumkosea kiasi cha kuamua kutonishirikisha kwenye mambo yake
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
49,757
35,821
Ndugu pole sana! Likini haya matatizo dada yako alikueleza mwenyewe? Pengine wewe ukaona tatizo yeye anaona sawa!
Hebu jaribu kuongea na dada yako kwanza!

Alaf swala la kuolewa na mwanaume mwenye wake zaidi ya mmoja huo ni huamuzi wa dada yako na hayo ni mapenzi yake!

Alicho fanya dada yako kuolewa bila kuwa taarifu ndugu si kitendo cha kiungwana japo hajavunja sheria!

Cha muhimu ni kukaa nae chini lakini epuka kuingilia sana mahusiano yao, dada yako ndio akuombe wewe msaada!
 
Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,504
2,250
Ruttashobolwa Mkuu hayo matatizo kamueleza Baba yake mimi hajawahi kuniambia wala hajawahi kunipigia simu kunieleza chochote,ila kinachoniuma ni yule jamaa kumpotezea muda wake sasa sahivi akirudi ni kuangalia mtoto na kuondoka hakuna ndoa tena,sasa mkubwa mi nitaingiliaje haya maswala na yeye hajawahi kuniambia kuhusu ndoa yake na wala sijawahi kugombana nae hata kwa utani tu,sasa alikuwa na maana gani kutoniambia mambo yake.
Kinachoniuma zaidi yule muhuni kwanza anatumia elimu ya dada yangu vibaya kwa kumfanyisha kazi za ndani na pia alienda kumbeba kienyeji na hakuwahi kumwambia kuhusu hizo ndoa nyingine na nasikia anataka kuoa mke mwingine na hao wengine washaanza kumpigia simu za vitisho
Mkuu Ruttashobolwa huyu ndo Dada pekee mi nilie nae Roho inauma mkuu
 
Last edited by a moderator:

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,640
512
Kwanini usiliingilie kati suala hili kwa kukaa kitako na hao watu wote(dada yako,mume wake,sheikh,baba na mama wa dada yako) kwa pamoja mlizungumze hili?Nadhani hapo mtapata suluhisho la kudumu kama ndoa ivunjwe kila mtu aende kivyake au vinginevyo.
ITEGAMATWI kule usukumani kuna msemo kwa wawindaji kwamba 'Lowugu lomo ndo, opuruka'. Umewahi muno kumshauri kuvunja nyumba, mama zetu najua ni wavumilivu sana ndo maana leo hii tunaona familia zao zinadumu. Mimi nafikiri ni swala la kuzungumza tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom