Naombeni ushauri,nimfanyeje huyu binti

Naombeni ushauri,nimfanyeje huyu binti

Achana naye kaka, maana hata ukimchukua jua anajipumzisha tu huku anatafuta kidume kingine. Mwanzo alikuacha akaenda kwa kidume kingine sasa amemwagwa ndo anarudi kwako kusikilizia
 
Achana nae zwazwa huyo fanya mambo yako umeona wapi ktk mapenz eti kuna utani wakuachana!ukijichanganya kurudiana nae ndo anakupoteza,jini huyo
 
Awe MCHEPUKO wako!Huwa wanaokoa sana hao sometimes hasa kama wife anaumwa!
 
Nilijua baadae,alimpata mjamaa ambae alikua wel off kifedha kuliko mimi,unajua kumiliki binti mzuri mjini huna hela majaribu kama haya yanakua hayakwepeki.

fedha kitu bwana wanawake tutakufa kwa kupendapenda hela mi nmemwacha mtu na hela zake hivihivi na haamini. yaani alitupanga kama utitiri kila nkienda geto nakutana na mara makondom mara saa za kike mara chupi zaid ya mara 2.. khaaa aende huko na hela zake nifupishe maisha kisaa????
 
pole sana bro, ila chakukushaur uclipe kisasi, we achana nae kabisa, inaonyesha ni jinc gan huyo mschana acvyokuwa hata na tone la huruma, m2 uko kwenye msba alaf tena yeye anakutumia sms yakuachana nae, kwa nn acngekusubiria ukamaliza msiba then ndio akuambie ujinga wke, temana nae, Omba Mungu atakupa msichna mwengne mzur tu mwenye huruma, na heshma na upndo
 
Angalia kama anajutia kosa na umsumbue kidogo,ila mrudie,kutenda kosa sio kosa KURUDIA KOSA NDIO KOSA,to err is human,give her a second chance..
 
Mkuu naamini umepata ushauri wa kutosha, hence ufuate ila jua kitu kimoja, revenge is for the weak, just move on na usiangalie nyuma, huyo binti hakufai hata chembe.
 
Nilijua baadae,alimpata mjamaa ambae alikua wel off kifedha kuliko mimi,unajua kumiliki binti mzuri mjini huna hela majaribu kama haya yanakua hayakwepeki.

Kama sababu ni hiyo piga chini mkuu!!! Tena kiroho safi...hakawii kukuliza tena huyo!!
 
Kama huna hisia naye mwambie tuu aendelee ma maisha yake,kwani inaonesha binti hakua na mapenzi ya dhati wala hana hata chembe ya huruma,huwezi jua anarudi kufanya nini moyo ya mtu kichaka aisee,mwambie tuu kua hana nafasi tena kwako,Pole kwa machungu aliyokupa ukiwa kwenye kipindi kigumu,usikate tamaa Mungu atakupatia wa kufanana nawewe asiye na makuu
 
Mkuu @the unknown, achana naye kabisa huyo! Ni mtu mbaya sana, hana mapenzi na wewe nani mtu ambaye hana msimamo, hana utu kabisa kwani alijua upo kwenye msiba na badala ya kusubiri msiba upite ndiyo akupe taarifa za kukuacha yeye akakuongezea msiba mwingine wa kuterminate mapenzi yenu! Achana naye wala usilipize hata kisasi! Dawa aliyoipata huko alikopaparikia hadi akakutumia sms ya kuachana na wewe inamtosha! Msamehe bure na uendelee na maisha yako!
Ilikua jumatatu, tarehe 10 mwezi wa 6 mwaka 2013,niko kwenye msiba wa kaka angu(RIP BRO).. Ilikua kama sa 2 hivi usiku niko kwenye kikao tukijadili na kupanga taratibu za mazishi,kuhifadhi mpendwa wetu.

Nikiwa kikaoni nikasikia mtetemo kwenye sim yangu ikiashiria ujumbe mfupi umeingia,sikua na haraka ya kuusoma,nikijua baada ya kikao ntausoma,ndio ntakua na muda mzuri wa kusoma ujumbe huo,hata hivyo mimi ndie nilikua katibu wa kikao,nikakipa kikao uzito zaidi.

Ilipofika sa 4 kama na nusu hivi kikao kimeisha, nikasikia mlio wa sim,ilikua ni sim yangu ikiita,nikaitoa mfukoni kuipokea,kusoma jina ni la kipenzi cha moyo wangu,nikatabasam kwa mbali nikijua mpenzi wangu kanipigia kujua naendeleaje,ile napokea tu sim ikakata.

Nikajua mamaa kaishiwa pesa,nikaenda hewani,simu ikaita kidogo kisha nikasikia"simu ya mteja uliepiga inatumika" ikiashiria sim imekatwa,nikakata sim,mara kidogo nikapokea ujumbe kutoka mpenzi wangu

"nilitaka kujua kama meseji umeipata,sitaki mapenzi na wewe,futa namba yangu" nikashtuka kidogo,nikajua ni utani,kisha nikataka kujua ni ujumbe gani huo

Nikaenda inbox nikakuta ujumbe uliokua umetumwa haujasomwa ni wake akinijulisha mimi na yeye basi. Nikampigia sim hapokei,nikatuma ujumbe hakujibu. Msiba wa ndugu yangu ukawa mchungu zaidi

Siku zikaenda hivyo nikiwa siamini kilichotokea,bila ugomvi,bila sababu ya msingi nikawa nimeachwa. Nikatumia kila mbinu kumbembeleza na kumshawishi,kupitia kwa ndugu zake,marafiki zangu na ndugu zangu akagoma.

Ratiba zetu ilikua mwezi wa kumi mwaka jana nikajitambulishe rasmi,mwezi wa pili mwaka huu tufunge ndoa . Mipango hiyo ikawa imekufa. Niliyumba sana baada ya hilo tukio,nimejikaza nikasimama kiume ila kwa maumivu makali sana.

Kituko cha mwaka ni kua binti huyo kamwambia rafiki yangu kua bado ananipenda na anatamani turudiane, hadi naandika ujumbe huu huyo binti toka juzi anapiga sim(sijapokea simu yake hata moja) na kutuma ujumbe akiniomba nimsamehe

Wadau,nimrudie kisha nimtende kama alivyonifanya au nimuache aendelee na maisha yake(sina hisia nae tena na wala simpendi,,namchukia sana,natamani kisasi juu yake),ebu nishaurini wandugu.
 
Kwa hiyo mkuu wewe ulimrejesha zizini?

kwangu mimi, Excel, sina tabia ya kuacha mwanamke mazima eti kisa nimegombana nae ama nime-break up..

najua ipo siku nitakaukiwa, hivyo itanilazimu kuchombeza nipate pa kupozea magenye yangu...

nimemrudisha in a dormant way... huwezi amini nikimkuta busy kwenye simu usiku, nikimtext why you were busy?

she call and start crying,... thats how love is crazy man!
 
Last edited by a moderator:
huyo binti achana nae hana mapenzi ya kweli.inawezekana kuna mtu alimdanganya amemuacha .muombe mungu atakakupa mke mwema ambaye hatakuumiza.pole sana kaka
 
Mh taf achana nae narudia achana nae japo co ushaur mzur ss ht kama nikutingisha kibiriti ndo hivyo amekuumiza ukimpa nafas utakuwa umejidhalilisha sana atakuendesha atakavyo kisasi chake nikumpotezea cm msg ucmpigie loh hana adabu bora angekwambia kosa lko usimpe nafas aende kule
 
Atakuwa alipata wakumdanganya akukuona hufai mambo yamevurugika eti samahan fukuza kbs tena mwambie una mtu asikusumbue
 
Mkuu hakujali kuwa ulikuwa na msiba wa kaka yako hakujali kuwa una machungu ya kumpoteza mtu wako wa karibu na juu ya hayo akakuongezea maumivu mengine ya kukumwaga na bila kutoa sababu
Kwa nini hakusubiri hata umalize msiba wa kaka yako ndo akumwage
Amekutingishia kiberiti akitumaini kuwa hakijajaa ila amekikuta kimejaa sasa anarudi kwako kukubembeleza kuwa mrudiane
Aliona nyota akakifikiri ameona mwezi sasa amekuta kile alichotarajia sicho ndo maana anarudi kwako
Kama huna hisia nae endelea na maisha yako na mwambie wazi kuwa yalishapita na maisha ya kuringiana na kujaribiana hayapo
We endelea na maisha yako maana huwezi jua katika hicho kipindi alichokumwaga alikuwa wapi na nani na nini kiliotokea huko
 
Kama bado una maumivu....mkubalie, vaa kondom 2 gonga ile ya hasahasa, kisha mpe mazima kwamba asikujue tena, trust me utapona saa hiyohiyo, kama umeshapona, achana nae na mfanye rafiki tu...inawezekana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom