Wapendwa JF nawasalimu,
Kwanza kabisa nishukuru waasisi wa JF na memba wote, naimani kubwa nitapata msaada humu kwa kua kabla ya kua member nimekua nikifuatilia makala na mada moto moto na baadhi zimetoa masuluhisho ya kudumu katika baadhi ya changamoto.
Nina umri wa miaka 35, naombeni msaada wenu kujua dawa ya kutibu mtu aliethirika na punyeto, uume wangu umelegea na hauwezi kufanya kazi kwa ufanisi, nikifanikiwa kufanya tendo la ndoa ni mara moja tu basi siwez kurudia tena mpaka baada ya masaa 10 yani kesho, ikumbukwe nimeoa na hii inanisumbua sana katika ndoa yangu, mke wangu amekua muelewa sana juu ya mimi kutomridhisha lakin anahisi mimi ninawanawake wengine, tatizo hili la kupiga punyeto nilidumu nalo kwa muda wa miaka 10 kabla ya kuacha kwa tabu sana na kuoa, naombeni usaada wenu juu ya vyakula au dawa za kurudisha uwezo wangu wa tendo la ndoa japo haitokua kama mwanzo.
Hechinodemata. Tatizo la nyeto husababisha kitu kikubwa kimoja ambacho ni kuharibikiwa kisaikolojia. Ukipiga nyeto unaudanganya mwili kuwa upo na demu fulani. Ukimchoka unahamia kwa mwingine. Hivyo akili huzoea kuwa na mademu kibao unaobadili kila unapohitaji Kufanya hivyo.
Unapopata mke ama demu wa muda mrefu, huwa unamchoka haraka, kwasababu akili haijazoea kukaa na demu mmoja kwa muda mrefu. Hapo utashindwa Kufanya nae mapenzi ipasavyo.
Tatizo la pili dogo, ingawa kwa Wengine huwa kubwa ni kuathiri mishipa ya Yule(erector mascles). Uume hupoteza nguvu hivyo kushindwa Kufanya mapenzi, ama Kufanya mara moja tu na kushindwa kusimama tena mpaka baada ya mapumziko ya muda mrefu.
Utatuzi
1.Tangawizi mbichi
2.Limao
3.Asali
Zimenye tangawizi zako ujazo wa kiganja kimoja ama viwili,kisha zitwange kwenye kinu mpaka zilainike kabisa. Kata malimao matano ama sita na kukamulia kwenye kinu chenye tangawizi. Chuja mchanganyiko wa limao na tangawizi kupata juice. Changanya asali kwenye juice yako uliyochuja.
Juice hii huwa Strong, hivyo kunywa vijiko viwili asubuhi na viwili jioni. Ukiweza kunywa hata vijiko viwili kutwa mara tatu kulingana na ratiba yako kazini.
Kama pia unataka kuongeza na wingi wa manii na mbegu za kiume, pendelea kula karanga mbichi.
Hii ni tiba asilia na sahihi ya tatizo hilo, kwasababu huongeza hamu ya tendo na pia huimarisha mishipa na misuli ya Uume. Haina madhara hata kidogo kwasabu ni tiba inayohusu vyakula. Na vitu vyote vinapatikana kirahisi. Tangawizi mbichi Ziko sokoni na magengeni, pia malimao yanapatikana kirahisi. Na hata asali. Wala usijisimbue Sijui asali ya nyuki gani, mara Sijui asali mbichi!!! Hapana, wewe nunua asali yoyote.
Jambo jingine la kisaikolojia unaweza kuongezea, mkeo awe mtundu kidogo. Wanaume tuna tamaa. Ukipita barabarani ukamwona mdada kavaa kimini, hata kama utajifanya kumponda lakini Kiukweli anakuwa kakutikisa. Ama akivaa ile half breast ! Matiti unayaona nusu, lazima unapagawa. Vitu hivyo wake zetu hawatufanyii Home. Inabidi siku nyingine unamkuta wife kapiga kimini, siku nyingine kapiga half breast, siku nyingine anakuvalia kanga, ikiwezekana kanga moja. Hapo utamwona mpya na kukupa hamasa kupiga mechi. Mkimaliza anaweza kupiga kanga akajifanya kuandaa kitu fulani huku akiwa kwenye upeo wa macho yako. Kumuangalia tu! Utajikuta unamwita arudi kitandani.
Sumu kubwa kwa mwanaume ni kulaumiwa na mpenzi ama mke kuwa hajamridhisha. Mwanaume akiambiwa hivyo huathirika kisaikolojia. Hujenga hofu ya kushindwa Kufanya mapenzi na Yule aliyemlaumu kwa dhana kuwa atashindwa. Mke anatakiwa asioneshe kumlaumu mumewe kuwa kashindwa. Anatakiwa ampe hamasa. Awe mbunifu.
Kiongozi, ukifuata haya utaniambia baada ya siku si zaidi ya wiki kuwa unatishaaaaaaaaa!. Wakati unatumia dawa maisha yako ya kimapenzi yaendelee kama kawaida, ila pombe usinywe(ukinywa hutakufa ila utaathiri dawa).
Faida nyingine za dawa hii ni:
1.Tiba mujarabu ya kikohozi na mafua
2.Tiba ya kupunguza mafuta mwilini
3.Huzuia kisukari
4.Ukitumia dawa hii na kula karanga mbichi , huongeza manii na mbegu za kiume