Naombeni ushauri niende kubaki Marekani au nirudi nyumbani

Nilijua upo marekani tayari🤣🤣🤣🤣🤣 embu kwanza fika marrkani ndo utuombe huo ushauri.ukiikuta marekani ya blue je
 
Hehe hata kufika hujafika ushaanza kuuliza kama ubaki? Uliza uende au usiende.
Fika marekani ishi kidogo alafu ndiyo ujiulize kama urudi au la, kwanza visa tu jipange kusumbuliwa, sio rahisi kupata working visa na kusurvive marekani hata kama umepanga kuzamia. Visa hiyo ya kuvisit DC kwa muda mfupi kubadilisha kupata working visa ni next to impossible, unless kampuni ikuchukua na iprove kua wewe ni very valuable kuliko wamarekani wenyewe piga ua hawakupi visa watakufukuza. Ukizamia ipo siku utashikwa tu, tena fasta zaidi ya unavyofikiria sababu unaingia na visa halali alafu hawatoona record yako yoyote ile ya kutoka nchini.
 
Sasa mkuu hili joto la jiwe tunalopitia na wewe unataka utukimbie hapana mzee baki na sisi tuisome wote namba
 
Reactions: A3M
Ntaichukua familia nikisettle
 
Kwa kifupi unaweza kuwa na viza lakini ukishia airport na kupanda ndege hiyo hiyo iliyokubeba kurudi nayo iwapo utatiliwa shaka,kwani kuna viswali huulizwa kabla hujagongewa muhuriwa kuruhusiwa kuingia,pia jua digrii yako ya Bongo hakuna anayeijua huko Marekani na mwisho hadi kuja kufanikiwa Marekani inachukua miaka, na Marekani si lelemama kama wengi tunavyodhani huku au tunavyoangalia kwenye FB ,na kwa hali ya mtawala wa sasa aliyepo kwenye jengo jeupe,sidhani kama ni jambo jema kupiga kambi Marekani na kwa sasa sijui hata nafasi za kusomea unesi kama zipo kama ilivyokuwa awali,kwa wengi ukiwa nesi angalau ndio unakuwa na maisha ya uhakika au uwe na skills za kufa mtu ndio mfumo ukuhitaji, na mwisho kaka bila makaratasi utaishia kuuza maji mitaani kwa pesa ndogo. Ni bora uende ukaangalie na urudi tu ,hapa Bongo ni peponi kulinganisha na huko unakotaka kuzamia,maisha si rahisi kama wengi tunavyodhani,Marekani hakuna cha mjomba wala kwenda kuchimba mhogo shambani,usipofanya kazi/kibarua jua hutakuwa na sehemu ya kulala wala kula,yes kila kitu kipo lakini kila kitu ni pesa.Nenda kajionee mwenyewe halafu uje utuambie hapa,lakini jua moja tu huko utaenda kupigika kweli kweli, na utaikumbuka Bongo.Nimeandika kwa uzoefu nilionao wa kuishi Marekani japo si kwa muda mrefu,ikabidi ni Uturn asap.
 
Ni kweli bro unayoyasema au ni unataka kunikatisha tamaa?
 
Ni kweli bro unayoyasema au ni unataka kunikatisha tamaa?
Sikukatishi tamaa,nenda kwanza ndio utaamua mwenyewe,labda kila mtu ana bahati yake,lakini kwa mfumo wa Marekani kazi ipo.Sijui unaenda jimbo gani?
 
We tamba tu.. ila siku mambo yakienda mrama ukweli mpaka kufikia hatua ya kurudi kijijini kwenu sitimbi... uje utuambia apa
 
Hata ardhi yawatu hujakanyaga(kwa trump)jamani ushamkumbuka mkeo tena ashazaa nawanao 3,hofuyako nn?kwenyestori yako sijaona kama unaenda nae....ukifika jipange harafu Fanya mpango mkeo ajehuko,naamini kwenye taarifazako ubalozini navisa(umeoa).kama alivofanya mwezako Dr slaa wilbrod.tangulia kwanzaaa ,sawa eee
 
Baki Awamu ya Tano,Awamu ya kishindo inaibadili TZ kuwa kama USA
 
Marekani kama Marekani,au marekani ya bongo?
 
Marekani wako na system nzuri sana mgeni ukiingia ukikaribia kuoverstay tu kwanza wanaanza kukufuatilia kwa mwenyeji wako mi nashauri nenda the rudi kupata visa tena huwa haisumbui.Rudi ukiwa umeshaset kila kitu kuhusu pa kufikia na mipango mingine ya kazi na vibali.
Ntaichukua familia nikisettle
 

Ushauri mzuri sana
 
Unaenda kufanya nini Marekani?.

Kwanini unajiuliza iwapo urudi ama usirudi.?una visa/papers za kumudu huko?..

US hakikisha una shughuli ya uhakika ya kipato..Kwa muda kidogo niliokaa US sijawahi tamani kuishi nje ya Tanzania...believe me kwetu kuna fursa, upendo wa kifamilia na maisha bado slope sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…